Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi Gaudensia Simwanza akiwaeleza waandishi wa Hababari leo Jijini Dar es salaam kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi ya chakula kisicho salama. Kulia ni Meneja Uchanganuzi wa madhara yatokanayo na chakula bi Candida Shirima.PICHA NA FRANK MVUNGI-MAELEZO |
Afisa Elimu kwa Umma wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na
Serikali ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa ambazo hazijasajiliwa hapa
nchini kwa maslahi ya Taifa.kulia Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa
Umma wa Mamlaka hiyo Bi Gaudensia Simwanza
………………………………………………………………………………………………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali yajidhatiti kuwalinda
wananchi kwa kuzuia athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na
matumizi ya chakula kisicho salama kote nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa mamlaka ya chakula
na Dawa (TFDA) bi Gaudensia Simwanza.
“Uchafuzi wa chakula food
contamination) hufanya chakula kisiwe salama na hivyo kusababisha
madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu na hata vifo kwa mlaji
pamoja na athari za kiuchumi”alisisitiza Simwanza
AkifafanuaSimwanza amesema kuwa
Serikali imekuwa ikichukua hatua madhubuti kukabiliana na tatizo hilo
ikiwemo kutathmini bidhaa za chakula ili kuhakikisha kuwa zinakizi
vigezo vya ubora na usalama kabla ya kusajiliwa.
Hatua nyingine ni usajili wa
maeneo ya utoaji wa vibali vya biashara ya vyakula na kufuatilia ubora
na usalama wa vyakula ndani na nje ya nchi.alibainisha simwanza.
Pia mamlaka hiyo imekuwa ikifanya
uchunguzi wa sampuli za chakula katika maabara ili kutambua hali ya
ubora na usalama wake pamoja ufuatiliaji wa usalama wa chakula ikiwa ni
pamoja na uchafuzi wa sumu,kemikali,viuatilifu,vimelea,mabaki ya dawa za
mifugo na mimea katika chakula.
Hatua nyingine ni kutoa elimu kwa
jamii kuhusiana na shughuli za udhibiti wa chakula ili kuhakikisha
usalama wa chakula hicho kwa wananchi watakaokitumia.
Mkakati mwingine ni wa kuanzishwa kwa mpango wa ufuatiliaji na ukusanyaji wa takwimu za magonjwa yatokanayo na chakula nchini.
Kwa upande wake Afisa Elimu kwa
Umma Bw. James Ndege almetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa
mamlaka hiyo ili iweze kutimiza majukumu yake kwa maslahi ya Taifa .
TFDA ni Taasisi iliyopo chini ya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na ilianzishwa
kwa mujibu wa sheria ya chakula , dawa na vipodozi sura 219 ambapo ina
jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora na usalama wa
chakula hapa nchini.
No comments:
Post a Comment