Monday, January 11, 2016

Donald Trump aendelea kuushambulia Uislamu

Donald Trump aendelea kuushambulia UislamuDonald Trump, anayewania kuteuliwa na chama cha Repubalican kugombea urais wa Marekani ameendelea kutoa maneno ya jeuri na yaliyojaa chuki dhidi ya Waislamu kwa kudai kuwa eti Waislamu ndio waliofanya jinai ya Cologne, Ujerumani.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo leo na kusema kuwa, Trump ametoa madai hayo katika kampeni za uchaguzi kwenye jimbo la Iowa nchini Marekani na kudai kuwa, hadi hivi sasa Ujerumani ilikuwa haijawahi kushuhudia matukio hayo, lakini tangu nchi hiyo iliporuhusu wakimbizi Waislamu kuingia nchini humo, matukio hayo yameanza kutokea.

Ameongeza kuwa, kuruhusiwa kuingia wakimbizi Waislamu katika nchi za Magharibi kutaziletea matatizo nchi za bara hilo na amezitaka zisiruhusu Waislamu kuingia barani Ulaya.

Itakumbukwa kuwa, katika mkesha wa mwaka mpya wa 2016, wanawake wasiopungua 100 waliporwa na kudhalilishwa kijinsia na watu wasiojulikana mbele ya kanisa kuu la mji wa Cologne, nchini Ujerumani.

Kabla ya hapo pia, Trump aliitaka serikali ya Marekani isiruhusu Waislamu kuingia nchini humo baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Ufaransa, na kuua watu 130.chanzo irib

No comments: