Serikali ya Bulgariia imetangaza kuwa itawatoza faini wanawake wa Kiislamu wanaoheshimu kikamilifu vazi lao la hijabu.
Serikali ya Bulgaria imetangaza kuwa itatoa adhabu na kuwatoza
faini ya euro 150 kwa mara ya kwanza na euro 500 kwa mara ya pili kwa
wanawake wanaovaa hijabu kamili ya Kiislamu katika maeneo ya umma.
Kiasi
hicho cha pesa kimetajwa kuwa ni zaidi ya mshahara wa kiwango cha
wastani wa kila mwezi nchini Bulgaria.Kupigwa marufuku vazi la hijabu nchini Bulgaria kumewafanya wanawake Waislamu kutoka majumbani mwao kwa nadra sana.
Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni viongozi wa serikali ya
Bulgaria wamechukua hatua kali dhidi ya wanawake wa Kiislamu nchini
humo.
No comments:
Post a Comment