Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran
amesema kuliunga mkono kundi la kigaidi la Munafiqina ndio mpango mpya
wa mabeberu na Uzayuni wa kimataifa dhidi ya taifa la Iran.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo katika jiji la Tehran
Ayatullah Ahmad Khatami ameashiria njama za Marekani na Saudia kwa ajili
ya kulihuisha kundi la kigaidi la Munafiqina na kutumia mabilioni ya
dola katika uwanja huo na kubainisha kuwa, kwa mujibu wa makubaliano
yaliyofikiwa kundi hilo la MKO litapewa fedha na silaha kutoka Saudi
Arabia ili kuendesha harakati dhidi ya nchi za kanda hii ikiwemo Iran.
Ayatullah Khatami amesema kuwa Munafiqina ni moja kati ya makundi ya
kigaidi yaliyopitwa na wakati na kugawanyika na kuongeza kuwa, Marekani
na nchi waitifaki wake wa Ulaya na katika eneo la Mashariki ya Kati
kamwe hawataweza kulifufua kundi hilo linalouwa watu wasio na hatia
ambalo tayari limeangamizwa na kusambaratika.
Ayatullah Khatami amesisitiza kuwa kundi la kigaidi la
Munafiqina lina faili jeusi zaidi mbele ya taifa la Iran na kueleza
kuwa magaidi wa kundi hilo wamewauwa shahidi raia elfu 17 wa Iran.
Imam wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tehran ameashiria nafasi
kubwa ya kundi hilo katika kuwauwa Washia na Wakurdi wa Iraq kwa agizo
la dikteta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein na kueleza kuwa, kundi hilo
hivi sasa pia linaendelea kuwauwa Waislamu huko Iraq na Syria
likishirikiana na kundi la kigaidi la Daesh.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran pia amewanasihi viongozi wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwahudumie vyema na kwa nguvu
zote wananchi.chanzo:parstoday
No comments:
Post a Comment