Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amekosoa uteuzi wa
Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Arusha.
Jana, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda na kumteua Gambo kushika nafasi hiyo
akitarajiwa kuapishwa rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
uteuzi huo, Lema amesema kuwa Gambo hakustahili kupewa nafasi hiyo
kutokana na namna alivyokuwa akifanya kazi alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya
Arusha.
“Hajui taratibu, amefanya makosa mengi kinyume cha
taratibu wakati akiwa Mkuu wa Wilaya, hakustahili kuteuliwa kuwa mkuu wa
Mkoa,” Lema anakaririwa na gazeti la Nipashe.
No comments:
Post a Comment