Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, imemtaka Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi afike mahakani hapo kutoa utetezi
wake, kwanini mahakama hiyo isimhukumu kufungwa jela kwa kushindwa
kutekeleza hukumu ya kuwalipa shilingi bilioni 1.2 watu watatu.
Mengi
aliamriwa kuwalipwa kiasi hicho cha fedha wafanyabiashara waliotajwa
kwa jina la Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo. Malipo
hayo yalitokana na uamuzi wa Mahakama kuhusu mgogoro wa hisa
uliokuwepo katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa
inaitwa Handeni Gold Inc. Hukumu hiyo awali ilitolewa Januari 28 mwaka
huu na Jaji Agathon Nchimbi.
Walalamikaji wamewasilisha maombi ya
mahakamani hapo wakiitaka mahakama hiyo kuchukua hatua dhidi ya Mengi
ikiwa ni sehemu ya hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa awali ya kuwalipa
watu hao.
Hati ya kiapo ya wafanyabiashara hayo imeoenesha kuwa
mmoja wa watu hao anaidai kulipwa fidia ya $428,750, mwingine $100,000
na mwingine $70,000.
No comments:
Post a Comment