Monday, April 13, 2015

Mufti asema unaweza 'kumla' mkeo Saudia



'Ni sawa kumla mkeo unapohisi njaa nchini Saudi Arabia lakini tu iwapo unahisi njaa kali'.
Mufti mkuu wa Saudia Abdul Azizi bin Abdullah

Mufti-kiongozi wa dini ya kiislamu aliye na uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu maswala ya kidini-ametoa idhini ya ulaji wa mtu.

Kulingana na gazeti la Metro nchini Uingereza na mtandao wa Alalam nchini Saudia Abdul Azizi bin Abdullah alishtumiwa kufuatia tamko lake kulingana na mitandao mingi ya kiarabu.

Mtandao wa A Tayyar uliripoti:Mufti mmoja wa Saudi Arabia alitoa agizo ambalo linamruhusu mwanamume aliye katika ndoa kumla mkewe iwapo anahisi njaa kali.


Mufti huyo amesema kuwa hatua hiyo inaonyesha vile mwanamke anafaa kumheshimu mumewe.

Lakini mamlaka ya kidini yamekana kwamba kiongozi huyo alitoa matamshi kama hayo.


Chanzo http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2015/04/150411_grand_mufti?ocid=socialflow_facebook
Jamani huo sio mtazamo wa Kiislamu, kwani katika mafundisho ya Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Maimamu 12 (a.s) hawajafundisha hivyo. 

Avigdor Lieberman ataka Wapalestina wote wauawe



Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametaka Wapalestina wote wauawe. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa IsraelAvigdor Lieberman

Shirika la habari la Palestina limemnukuu Avigdor Lieberman akisema hayo leo na kuongeza kuwa, hatarejea kwenye Baraza la Mawaziri la serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, hadi pale Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itakapofutwa kikamilifu na wanachama wake wote kuuawa. 

Lieberman ambaye ni mkuu wa chama cha Yisrail Beiteuni pia amemlaumu Benjamin Netanyahu kwa kukwepa mazungumzo ya muungano unaounda serikali ya utawala wa Kizayuni katika kuunda Baraza la Mawaziri. 

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa bunge la utawala wa Kizayuni "Kneset" wa tarehe 17 mwezi uliopita wa Machi, chama cha Likud kilipata viti 30, muungano unaojulikana kwa jina la "Umoja wa Kizayuni" ulipata viti 24 na muungano wa vyama vya Waarabu ukapata viti 13 kati ya viti 120 vya bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Israel, Baraza la Mawaziri linaundwa na chama kikuu lakini kiongozi wa kila chama atakayeweza kuunda muungano wenye viti vingi zaidi bungeni, hupewa yeye jukumu la kuunda serikali na Baraza la Mawaziri.
Chanzo http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/48042-avigdor-lieberman-ataka-wapalestina-wote-wauawe

Saturday, April 11, 2015

sherehe kuzaliwa kwa Fatma (a.s)

Sheihkh wa Hawzat Imamu Swadiq (a.s) Abdullatwif Swalehe akimshukuru Allah (swt) kwa kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bibi Fatma (a.s) Fatma alizaliwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Bibi Khadija, tarehe 20, Jamadul Akhirah..
Wanafunzi wa Hawzat Imamu Swadiq (a.s) waiimba Qawsida ya kuelezea namna Bibi Fatma (a.s) alivyozaliwa.Sherehe hizo zimeandaliwa na Hawzat Imam Swadiq (a.s), Kigogo-Post, Dar es salaam.

Waumini wa Dini ya kiislam, wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq(a.s) waikiwa makini kusikiliza mawaidha ya masheihjuu ya tokio la kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bibi Fatma Zahra (a.s)

Keki ilyoandaliwa kwa kusherehekea kuzaliwa kwa Mwanamke bora Kuliko mwanawake wote Ulimwenguni Bibi Fatma (a.s)

Sheikh wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Said Othmani akikata Keki Iliyoandaliwa kwa Mnasaba wa Kukumbuka Kuzaliwa kwa Fatma (a.s)

Thursday, April 9, 2015

Kukaguliwa vituo vya kijeshi, mstari mwekundu Iran



Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kukaguliwa vituo vya kijeshi ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya IranBrigedia Jenerali Hussein Dehqan

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan ameelezea madai ya uwongo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Magharibi likiwemo gazeti la Guardian la Uingereza ya kukaguliwa vituo vya kijeshi vya Iran 

ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya Lausanne nchini Uswisi na kusisitiza kwamba, kamwe hayakufikiwa makubaliano kama hayo. 

Brigedia Jenerali Dehqan amesisitiza kwamba, suala la kukaguliwa vituo vya kijeshi hapa nchini, ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya Kiislamu. 

Hivi karibuni yalifikiwa makubaliano kati ya Iran na kundi la 5+1 ambapo moja kati mafanikio makubwa iliyoyapata Iran kwenye makubaliano hayo, ni kwa nchi hizo sita zenye nguvu duniani kuitambua rasmi miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani.





Wednesday, April 1, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s) yakumbuka Kifo cha Jafar Ibn Abi Twalib

Mwalimu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Sheihk Saidi Athumani akitoa hutuba juu ya kifo cha Jafar Ibn Abu Twalib.     Kumbuumbu hizo Zimeandaliwa Na Hawzata Imam Swadiq (a.s) na zimefanyika leo Msiitini Ghadir, Kigogo-Post, Jijini Dar es salaam.  

Waumini mbalimbali pamoja na Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakiwa makini kusikiliza simulizi yenye majonzi ambayo Jafar Ibn Abu Twalib, aliuliwa katika Vita Vya Muu'tah, kwa kukatwa mikono yake Miwili.
Sheikh Saidi Athumani akionesha kwa mfano njia aliouwa akipigania Jafar Ibn Abu Twalib, kuwa ni njia iliyonyoa, ambayo ni  ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Jafar Ibn Abu Twalib alipewa jina na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Baba wa Masikini, kwani alikuwa anawapenda, kuwasikiliza pamoja na kuwasaidia, na uwahurumia Masikini.

Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq pamoja na Waumini wakiwa makini kusikiliza historia ya Jafar Ibn Abu Twalib.

Katika Vita Vya Mu’utah Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali. Alipigana kishujaa na kwa muda mrefu, akiwaua maadui wengi kiasi kwamba miili yao ilijipanga kama kamba ya kuni kumzunguka yeye.

Lakini baadae askari wa Kirumi alitambaa kutoka nyuma, bila ya kuonekana, na akampiga kwa upanga wake kwenye mkono wake wa kulia, na akaukata kabisa. 

Jafar hakuiachia bendera ianguke chini, na alizidi kumbana adui.
Baadae kidogo, Mrumi mwingine akaja kutokea nyuma, na kwa pigo la upanga wake, akaukata mkono wa kushoto pia. 

Shujaa huyu, akiwa bado hajakata tamaa, aliishikilia bendera chini ya kidevu chake, na akaendelea kusonga mbele.
.