Friday, August 7, 2015

Ilani ya vyama vya ACT, ADC sasa hadharani, Ukawa na CCM Bado.

Wakati joto la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu likiendelea kupanda, vyama viwili vya ACT-Wazalendo na ADC ndivyo vilivyokamilisha ilani zake na kutangaza kwa umma, huku viongozi wa vyama vingine wakitangaza kukamilisha kazi hiyo kabla ya kuanza kampeni.
Kitabu hicho cha ilani kwa kila chama, hubeba ahadi za kuwatumikia wananchi.
Vyama vya UDP, PPT-Maendeleo, Sau na CCK, jana walisema watakachokifanya kwa sasa ni kuboresha ilani zao kwa ajili ya uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Sau, Ali Kaniki alisema wameshanza kufanya maboresho ya ilani yao kwa baadhi ya vipengele.
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Joackim Mwakitinga alisema sehemu ya ajenda katika kikao cha ndani cha Agosti 15, mwaka huu ni kupiti ilani ya chama.
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Nasoro Dovutwa alisema chama kinaendelea na maandalizi ya kupitia ilani ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muhabi alisema ilani ni sehemu ya ajenda katika vikao vya kamati kuu ya chama hicho vitakavyoanza leo, ili kupitisha jina la mgombea urais, ubunge na udiwani.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alijinadi akisema chama chao ndicho pekee kilichokamilisha kuandaa ilani.
Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema tangu mwaka 2005, chama hicho kimekuwa kikifanyia maboresho ya ilani yake.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alisema hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika ilani ya mwaka huu kutokana na ubora wake.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hivi karibuni, alibainisha kuwa ajenda ya kuandaa ilani itakasimishwa kutoka mkutano mkuu kwenda kamati kuu, ambayo itaanza vikao leo.
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa baada ya kukamilika kwa ilani hiyo, itapitiwa na vyama vingine vinavyounda Ukawa ili kuijadili kabla ya kuitangaza rasmi kwa umma.
“Hiyo ndiyo itakuwa ilani ya Ukawa baada ya kupitiwa na chama na baadaye vyama vingine ndani ya Ukawa,” alisema Makene na kuongeza:.
“Kwa sababu tumeamua kuungana kwenye uchaguzi huu, basi kile tunachokusudia kufanya lazima tuwape na wenzetu wapitie kisha ndipo nasi tutangaze kwa umma.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete hivi karibuni alisema halmashauri kuu ya chama hicho itabeba jukumu la kushughulikia maandalizi ya ilani.Chanzo.Mwananchi.

Vyama Pinzani Vyalia, Magufuli akaribishwa Ikulu

Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mhe. John P. Magufuli mara baada ya kuwasili katika hafla iliyoandaliwa.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mhe. Nape Nnauye, Mhe. Abdulrahman Kinana, Mhe. John P. Magufuli na Mhe. January Makamba wakijumuika kwa pamoja katika hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana na Mhe. January Makamba wafika kwenye hafla maalum ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kumkaribisha Mhe. John P. Magufuli.
Mhe. John P. Magufuli akisalimiana na Mhe. Stephen Wassira baada ya kuwasili kwenye makao makuu madogo ya CCM Lumumba.

CUF Kilio, ADC Sherehe

Mgombea urais wa jamhuri ya muungangano wa Tanzania LUTALOSA YEMBA katikati akiwa na mgombea urais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar HAMAD RASHID kulia na kushoto ni mwenyekiti wa chama hicho ambaye sasa ni mgombnea mwenza wa urais bwana SAID MIRAJ wakifurahia mara baada ya mkutano mkuu kupitisha majina yao kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuuu ujao nchini Tanzania
 Mwenyekiti wa chama cha ADC ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais akizngumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu leo
Naye mgombea wa Urais katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambaye hapo awali alikuwa ndani ya chama cha wananchi CUF mh HAMAD RASHID  amesema kuwa sasa Zanzibar  hakuna upinzani kwani chama Tawala CCM pamoja na CUF wameungana na kuunda serikali hivyo chama cha ADC kimekuja kutoa upinzani wa kweli na bhatimaye mwaka huu kufanikiwa kuchukua dola hiyo.


Aidha katika hatua nyingine mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho chief liembe amemteua mwenyekiti wa chama hicho bwana SAID MIRAJ kuwa mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi ujao
 Maadhimio hayo yamefikiwa leo jijini Dar es salaam katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo wanachama walipiga kura ya kuwa na imani na wagombea hao kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 25 ya mwezi wa kumi mwaka huu.
Akizngumza na wanachama mara baada ya kuchaguliwa kunai nafasi hgiyo kubwa ya uongozi katika jamhuri ya muungano wa Tanzania chief liemba amesema kuwa ana imani kubwa sana kuwa atafanikiwa kushinda nafasi hiyo huku akitamba kuwa hadi sasa hajaona mgombea kutoka chama chochote nchini ambaye ana uwezo wa kupambana naye katika uchaguzi huo.

 Hamad Rashid Pamoja na Chifu Yemba mara baada ya kuchaguliwa kugombea nafasi za juu ya nchi katika uchaguzi mkuuu ujao
 Wakati vyama mbalimbali viukiendelea kujiweka sawa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nacho chama kipya katika uchaguzi huu chama cha ,,,,,,,,,ADC leo kmimetangaza wagombea wake wan a fasi ya urais wa Zanzibar pamoja na mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Baada ya mchakato mrefu wa kupitia na kusikiliza hoja za watia nia mbalimbali katika nafasi hiyo mchakato uliopitia katika vikao vyote vya chama hicho  hatimaye mkutano mkuu uliofanyika leo umepitisha jina la chief liemba kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muun gano wa Tanzania huku jina la mlezi wa chama hicho HAMAD RASHID likipita bila kupingwa kuwania nafasi ya urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia chama cha ADC.

Pro. Lipumba atoa Sababu za kunga'atuka leo hii

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.
Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

Thursday, August 6, 2015

Picha hii imezua shangwe kwa wanachadema muda huu,itizame

Picha hii inaweza kuwa ndiyo picha inayoenea kwa kasi sasa katika mitandao mbalimbali picha ambayo inamuonyesha katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo chadema Dk wilbrod Slaa akiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambapo imeelezwa kuwa ni baada ya kikao cha mashauriano ya kumshauri katibu huyo kurejea ofisini na kuendelea na majukumu yake.

Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa kikao hicho kimemalizika na katibu huyo atarejea ofisini muda wowote kuendelea na jukumu kubwa la kupanga wagombea ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.

Mtandao huu unafwatilia kwa ukaribu habari hizi tutawajuza zaidi

Wednesday, August 5, 2015

"ADC" Uchaguzi Oktoba ni baina ya CCM na CCM

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj akizngumza na wajumbe wa mkutano huo Akizngumza wakati akifungua mkutano mkuu wa bodi ya wanachama wanaokutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kupitisha majina ya wagombea urais wa chama hicho,mwenyekiti wa chama hicho  cha ADC Mhe. Said Mirajamesema kuwa kwa hali ilivyo sasa uchaguzi unaokuja mwezi wa kumi utakuwa kati ya ccm na ccm wenyewe huku upinzani ukiwa hauna nguvu kutokana na kuwapikea baadhi ya makada wa chama chama mapinduzi na kuwapa dhamana kubwa ndani ya vyama hivyo.
 Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj Akisalimiana na  mlezi wa chama hicho ambaye sasa ndiye mgombea wa urais 

zanzibar  kwa tiketi ya chama hicho wakisalimiana wakati wa 
 ufumnguzi wa mkutano huo
 Wakati macho na maskio ya watania yakiwa yanaangalia mnyukano wa kisiasa unaoendelea nchini baina ya chama cha mapinduzi na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA nacho chama kipya kinachokuja kwa kasi chama cha ADC wameibuka na kusema kitendo kilichofanywa na vyama vya upinzani kuwachukua baadhi ya viongozi wa chama tawala na kuwapa madaraka ni muendelezo wa kuwasaliti watanzania na kuendelea kuipa nafasi CCM .
 Wajumbe wakiwa katika mkutano huo
Amesema kuwa kwa hali inayoendelea sasa nchini Tanzania ni wazi kuwa hakuna mtanzania aliye na nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania ila ni ADC pekee kwa kuwa wao hawako tayari kuwapokea makada wa chama chochote waliokatwa na kuwapa madaraka kwani nao ndio wanaweza kuwarudisha watanzania tena kule ambapo wanakupinga.

Kauli hii inakuja ikiwa waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mh EDWARD LOWASA amekihama chama chake na kuhamia cha cha democrasia na maendeleo chadema huku makada kadhaa wa chama hicho wakiendelea kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani.

Tizama ya magufuli leo akichukua form ya Urais

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar.
   Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Mgombea Mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi akiwapungia mkono wananchi na wafuasi wa chama hicho nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu  ya CCM mtaa wa Lumumba wakishangilia wakati Mgombea alipokuwa ikielekea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.