Sunday, October 19, 2014

Dua ya kumrehemu Sheikh Dhikir Kiondo

Sheikh wa Bilala (kushoto) Tandika Temeke, Dar es salaam, akiwa katka kisomo cha Muasisi wa Tanzania Ithnashery Community (T.I.C), Nyumbani kwa Marehemu Dhikir Kiondo.

Masheikh ,Wanafunzi na Majirani wa Marehemu Sheikh Dhikir Kiondo, wakimsomea kisomo cha Qur'an ya kumrehemu.

Mwalimu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (kushoto) akiwa na mjunbe wa kata ya Tandika, Temeke wakimsomea kisomo cha Qur'an Sheikh Dhikir Kiondo kwa kumrehemu.

Wanaharakati wa kike,Wanafunzi wa Hauza wa Hauza ya Imam Jafar Swadiq wakiwa pamoja katika kumrehemu muasisi wa T.I.C Sheikh Dhikir Kiondo

Huyu ndio Sheikh Dhikir Kiondo, muasisi wa Taasisi ya Tanzania Ithnashary Community (T.I.C)

Sunday, June 22, 2014

Uganda yapuuzilia mbali vikwazo vya Marekan




Serikali ya Uganda imepuuza vikwazo ilivyowekewa na serikali ya Marekani kutokana na kupitisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja. Ofwono Oppondo, msemaji wa serikali ya Uganda amesema kuwa, vikwazo vya Washington dhidi ya nchi yake, vitakuwa na taathira ndogo tu kwa uchumi wa Uganda. 

Ofwono pia amekadhibisha tuhuma zisizo na msingi zilizotolewa na Marekani kwamba vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi ya watu wa jinsia moja wanaojamiana hasa baada ya kupitishwa sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo vichafu vimeongezea nchini Uganda na kusema kuwa, madai hayo ni ya kipuuzi. Amesisitiza kuwa, kuanzia sasa Waganda watajidhaminia wenyewe mahitaji hayo na hawatakubali kufanywa watumwa wa wafadhili. 

Sheria ya kupiga marufuku liwati na usagaji nchini Uganda ilipasishwa mwezi Februari mwaka huu. Hata hivyo madola ya Magharibi kama vile Denmark, Norway, Uholanzi, Sweden na Marekani zilipinga vikali hatua hiyo. 

Juzi Marekani ilipasisha muswada wa kuiwekea vikwazo serikali ya Kampala na kukata misaada yake ya kifedha kwa nchi hiyo. irib



Friday, June 20, 2014

Umoja wa watu ni kinga kwa Taifa

Hawa ni baadhi ya watu waliohudhuria katika semina hiyo na wakwanza kulia ni Sheikh Omari Sungura.
Semina ya kujenga umoja na mshikamano baina ya Waislamu na dini zote za mbinguni imefanyika usiku huu wa tarehe 18/06/2014 mjini Posta,jijini Dar es Salaam, Katika Semina hiyo viongozi wa kidini wametakiwa kutoa elimu katika jamii kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa ulimwenguni, viongozi hao wametakiwa kufichua njama dhidi ya makundi haramu yaliyojivisha sura ya Uislamu.

Sheikh Hemed Jalal akiwa akionekana kuwa ni miongoni wa wasikilizaji mahiri katika semina hiyo na wakwanza na mwalim mkuu wa chuo cha Jamia-Mustafa kilichopo upanga jijini Dar es salaam

Sheikh Mulaba akiendelea kuwakaribisha wazungumzaji katika semina hiyo akiwa ni Mc ambayo watu waliodhuhuria semina hiyo yakadiriwa kuwa ni 150 kwa uchache

Hawa ni baadhi ya Wanawake ambao waliohudhuria kaitka semina hiyo ambayo wanaonekana kuwa makini katika usikivu wao.Picha na afroshia

Tuesday, April 1, 2014

Serikali yawatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)


Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia bi Prisca Ulomi akitoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam .


Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika  Uandaaji wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mtandao,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.

Habari Kamili
Serikali yawatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuondoa vitendo vya uhalifu hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA wameamua kuandaa muswada wa Sheria  za Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao (Cyber Laws).

Akieleza zaidi Bi Prisca amesema kuwa Muswada wa sheria hizo ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data Protection Bill), Muswada wa Sheria ya Biashara ya Miamala ya Kielektroniki (Electronic  Transaction Bill), na Muswada wa Sheria ya Kuzuia Uhalifu kwa njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber Crimes Bills).

“Sheria hizo zitasaidia kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini kwa kudhibiti uhalifu kwa kutumia mitandao na kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya mitandao”. alisema Bi Prisca.

Bi Prisca aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuweka miundombinu ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha na kuharakisha utoaji wa huduma mbalimbali na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya teknolojia hiyo, hivyo kunaumuhimu wa kuwepo sheria zitakazodhibiti uhalifu kupitia mitandao.


Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  imetoa rai kwa wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri mitandao hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hali inayoweza kuathiri ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Serikali yaweka mikakati madhubuti kupambana na magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini


Meneja Masoko  na Elimu kwa Umma  toka  Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu programu ya upimaji wa Afya kwa wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza inayoendeshwa na mfuko huo hapa nchini.kulia ni Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja na kushoto ni Afisa habari ,Idara ya Habari Maelezo  Bi Fatma Salum. 
Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja  akiwaeleza waandishi waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo  na shinikizo la damu,kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi Anjela Mziray.


Habari kamili
Serikali imeweka mikakati madhubuti kupambana na magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini,hayo yamesema na  Meneja Masoko  na Elimu kwa Umma  toka  Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray  wakati wa mkuatano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.



Akieleza Bi Anjela amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya imekuwa ikichukua juhudi za maksudi katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na Saratani za aina mbalimbali.

Akifafanua zaidi Bi Anjela amesema programu hiyo imekuja kutokana na ukweli kwamba magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka na yamekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi nchini na duniani ambapo takwimu za shirika la afya Duniani za mwaka 2012/2013 watu zaidi ya milioni 35 hufa kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Bi Anjela aliongeza kuwa kati ya waathirika wa magonjwa yasiyoambukiza milioni 28.1 wanatoka katika nchi zinazoendelea ambapo kwa Tanzania magonjwa hayo husababisha vifo mara 4 zaidi mijini ambavyo ni sawa na  asilimia 12.8 wakati asilimia 3.1 wapo vijijini.

 Akitolea Mfano Bi Anjela alisema katika zoezi la upimaji lililofanyika Dodoma Septemba, 2013 jumla ya watu 591 walipimwa kati yao 14  sawa na asilimia 2.3 waligundulika kuwa na kisukari, na 28 sawa na asilimia 5 walikuwa na shinikizo la damu, wakati  watu 128 sawa na asilimia 22 walikuwa na uzito uliokithiri.

Bi Anjela aliongeza kuwa katika zoezi lililofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam ocktoba, 2013 watu 450 walipimwa, nusu yao waligundulika kuwa na uzito uliokithiri na katika zoezi lililofanyika Zanzibar watu 273 walipimwa ambapo kati yao watu 10 sawa na asilimia 3.6  waligundulika kuwa na kisukari, watu 83 sawa na  asilimia 30.4 walikuwa na uzito uliokithiri.

Naye  Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja  alitoa wito kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi  na kuzingatia lishe bora ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo  na shinikizo la damu.

Katika jitihada za Kutoa huduma bora kwa wananchi  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebuni mkakati maalum ambao unajulikana kama Afya Bonanza ambayo ni Kampeni ya kupima afya na kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza  na inakusudiwa kufanyika mikoa yote hapa nchini ambapo  Zoezi hilo lilizunduliwa rasmi Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam  mwezi machi 2014.

Friday, March 21, 2014

TFF Na Benki Ya CRDB Zimeunda Kikosi Kazi Kwa Ajili Ya Kushughulikia Ya Tiketi Za Elektroniki




Afisa Mawasiliano Shirikisho la Soka Tanzania Boniface Wambura  amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB zimeunda kikosi kazi (task force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi za elektroniki ambayo yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza.

Amesema TFF na CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya uboreshaji matumizi ya mfumo huo.



Aidha amesema Kikosi kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.



Hatahivyo amesema Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao akiongoza timu yake.





amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.