Sunday, May 31, 2015

Ugaidi Hauna Mahusiano na Dini ya Uislamu-Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA akifafanua jambo kuhusu suala la Ugaidi, Sheikh Jalala alisema ugaidi unaotajwa hauna mahusiano kabisa na mafundisho ya Dini ya kiislamu. 
Imeelezwa kuwa mafundisho ya Dini ya kiislamu  hayana uhusiano kabisa na matendo ya kigaini kwani uislamu umejikita kufundisha watu masula ya Amani.
Suala la dhana iliyojaa katika nafsi za watu kwamba waislamu wanafundisha uhasama kati ya  kundi, mtu ama watu, kuwa wauaji kama inavyotafsriwa na watu walio wengi  ni batili na inalenga kuuchafua uislamu na wafuasi wa mafundisho ya dini hiyo.
Akizungumza na ummati wa watu waliohudhuria kikao cha pamoja ya viongozi wa dini mbalimbali waliokutana kujadili mienendo ya ugani Barani Afriaka, Kiongozi wa kiroho wa dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA hapa nchini Sheikh Hemed Jalala alisema lazima umma ufahamu kuwa uislamu haufundishi ugaidi.
 Sheikh huyo alisema kuwa vitendo vya ugaidi na mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali barani  Africa na duniani kwa ujumla hayahusiani hata kidogo na dini ya kiislam kama ilivyokua ikielezwa na wadau mbalimbali.
Mmoja wa viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho Pastor PRINCE ERASTO IKONGO kutoka pentecoste akifafanua jambo kwa jamii. Pastor Ikongo alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa kiroho wa kikristo na waumini kwa ujumla wasiowaogope waislamu kwani mafundisho yao ni mazuri.Katikati ni sheikh HemedJalala na wa mwisho ni sheikh Juma mbukuzi.
 
Sheikh Jalala Ameongeza kusema kuwa ugaidi katika bara la Africa umekuwa ukitafsiriwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa katika msukumo wa dini ya kiislam jambo ambalo amesema kuwa watanzania wanapaswa kuelewa sio sahihi kuwatuhumu waislam kwa ugaidi kwani hakuna kitabu chochote kinachoruhusu muislam kufanya mauaji kwa mwadamu mwenzake.
Amefafanua kuwa mivutano na Ugaidi uliyopo barani Africa umekuwa ukisababishwa na mambo matatu ambayo ameyataja kuwa ni ugaidi wa kifikra,kiuwezo na ugaidi wa kudai haki.

Aidha Ameongeza kuwa dini zote duniani hakuna hata ushaidi wa dini moja ambayo inaruhusu ama kushabikia vitendo vya mauaji ya kigaidi yoyote yanayotokea afrika..
Katika hatua nyingine sheikh JALALA akizungumzia swala ambalo limekuwa likitamkwa na serikali kuwa viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakiwafundisha vijana wao wa mbinu na njia za ugaidi ameitaka serikali kuacha kauli hizo kwani ni kauli za kichochezo na zisizo na ushahidi wowote na badala yake wafwatilie swala hilo kiundani pasipo kuitaja dini yoyote kuhusika.
Sehemu ya Umma uliohudhulia kikao hicho
 Akizungumza katika kikao hicho muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO IKONGO kutoka pentecoste Tabata amesema kuwa viongozi wa dini za kikiristo wamekuwa na hofu kubwa juu ya ndugu zao ambao ni waislam hofu ambayo wamejengewa kuwa viongozi wa dini za kiislam pamoja na waumini wao ni watu wa mauaji na ugaidi jambo ambalo amewatoa wasi wasi wakristo na kuwataka kujenga umoja na mshikamano juu ya waislam na dini zote Tanzania ili kuidumisha amani ya nchi.
 Amesema kuwa hofu iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili waweze kudumisha umoja wanchi.

Saturday, May 16, 2015

Huzuni kwa Fmilia ya Muhammad (s.a.w.w)

Sheikh Abdullatwif Swalehe wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s) akielezea kifo cha Imam Mussa Al- Kadhim (a.s) namna alivyouwawa na Harun bin Rashid.

Kumbukumbu hii imeandaliwa na Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s), Kigogo-Post, Dar es salaam, chini ya Uongozi wa Mawlana Sheikh Hemed Jalala.

Siku ya leo ni siku ya huzuni kwa wafuasi wa Ahlul Bayt (as) kwa kufariki Imam Musa Al-Kadhim(as) katika mwaka wa 183hijria kwa vitimbi vya Haruna Rashid, Imam Kadhim(as) aliaga Dunia baada ya matatizo mengi yaliomtokea kama kufungwa na kuagiza watu katika Jela ili wamuudhi Imam Musa Al-kadhim(as) na kumuekea sumu katika chakula chake.



Walimu wa Hawzat Imamu Jafari Swadiq (a.s) wakiwa katika 
majlisi ya kukumbuka kifo cha Imam Mussa al-Kadhim.


Imam Kadhim AS alisisitiza kuhusu ufahamu na uono wa mbali katika dini kwa kusema: ‘Ifahamu dini, kwani kuifahamu dini ni ufunguo wa uono wa mbali na ubora wa ibada na ni njia ya kufika kwenye nafasi ya juu na adhimu katika dini na dunia.

Ubora wa kufahamu dini ikilinganishwa na kufahamu ibada ni sawa na namna jua lilivyo katika nafasi ya juu kuliko nyota. Kila ambaye hafuatilii suala la kuifahamu dini, Mwenyezi Mungu hafurahii ibada yake.

Wanafunzi wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s) wakiimba kaswida ya kuhuzunisha juu ya tukio la kuuwawa Imam Mussa al-kadhim (a.s)


Viongozi pamoja na Walimu wa Hawzat Imam Jafar Swadiq nao wakijumuika pamoja na Ahlulbayt wa Mtume katika kuuadhimisha kumbukumbu cha kifo cha Imam Mussa al-Kadhim.

Tuesday, May 12, 2015

Mawlana Sheikh Jalala"Bingwa wa Amani ni Imam Ali (a.s)

   
Sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s)  zimeandaliwa na Hawzat Imam Jafar Swadiq, Kigogo-Post, Dar es salaam.

Friday, May 8, 2015

Tuwasaidie Wahanga wa Mafuriko

Hali ya Mvua katika jiji la Dar es salaam.athari ya mafuriko:baadhi ya nyumba za watu zikiwa zimezingirwa na maji

Maulana Sheikh Hemedi Jalala: Imam wa Masjid Ghadiir Kigogo Post-Dar es salaam
 Katika khutba ya leo ijumaa tarehe 8/5/2015, katika masjid Ghadiir –kigogo Dar es salaam, Maulana sheikh Hemedi Jalala amewataka waislaam, waumini na jamii  kwa ujumla, kuwasaidia na kuwaenzi  watu waliokumbwa na mafuriko, 

alisema:          ” sehemu kubwa ya Jiji la Dar es salaam limekumbwa na mafuriko na mvua kubwa, zilizosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha na wengine kukosa makazi na malazi, ni wajibu wetu kuwasaidia , kwa sababu ni ndugu zetu,na jamaaa zetu,  tufahamu yakua tukio lolote linalotokea duniani  lina maagizo ya  mwenyezi mungu”. 

Maulana aliendelea kusema, “kuwasaidia waliopatwa na matatizo ni katika ibada, ibada ni tukio lolote linalomkurubisha mtu na mungu, kuondoa adha, miba, chupa, misumari njiani, ni ibada , navilevile kuwasaidia, kuwapa pole, 

kuwatembelea na kutoa misaada ya kihali na mali na kuwafariji ni ibada kubwa.ukitambua kuna mtu anamatatizo, shida , mitihani, fanya  haraka kuyatatua matatizo yake, kwani mwenyezi mungu ana sema fanyeni haraka kutaka msamaha wa mwenyezi mungu.”

Monday, May 4, 2015

Waziri mkuu aunda kamati kushughulikia kero ya usafiri nchini

Waziri mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo Pichani.
Waziri Mkuu Peter Pinda ameunda kamati maalumu ya kudumu ya kusimamia Usafiri wa barabarani nchini ili kutatua changamoto zinazoikabali sekta ya Usafiri.

Katika kamati hiyo mwenyekiti wake atakuwa katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi, Katibu akiwa kamishna wa polisi barabarani na Mkurugenzi wa SUMATRA huku wajumbe wakiwa ni pamoja na katibu mkuu wizara ya kazi ya na ajira, katibu mkuu ujenzi, mwanasheria mkuu wa serikali na naibu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu.

Mkuu wa ratibu wa idara ya maafa toka ofisi ya waziri mkuu, mwenyekiti wa TABOA na TATOA, CHAKUA na wanatakiwa kuanza kufanya vikao leo na kila mwezi watakutana kujadili na kutatua changamoto zote kasoro zile za kisheria ambazo zitapelekwa serikalini kwa mchakato zaidi wa kuzirekebisha.

Wakati huo huo umoja wa vyama vya madereva nchini Tanzania umesema hauna taarifa juu ya wao kutakiwa kukutana na waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kwa ajili ya mazungumzo kama inavyozungumzwa na kusisitiza kuwa wao wataendelea na mgomo wao ulioanza leo mpaka masuala yao yatapofanyiwa kazi.

Akizungumza na East Africa Radio leo Makamu Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya Madereva Abdallah Lubala amesema kauli ya kuwa wamekubaliana kukutana na Mh. Pinda ni za kisiasa na hazina ukweli wowote hivyo wataendelea na mgomo wao. 

Wakati huo huo mgomo huo ambao umetangazwa kwa nchi nzima athari zake zimejitokeza katika mikoa mingine tofauti ambapo madereva wa mabasi ya abiria wamegoma huku wasafiri wakitumia usafiri mbadala wa bajaji pamoja bodaboda.

Sunday, May 3, 2015

Mrema Ataka Rais Kikwete Aongeze Muda Wa Kuwa Rais ili akamilisha Katiba

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongoza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Hivi karibuni viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema ni miezi mitatu imebaki kabla ya kampeni za uchaguzi, lakini mpaka sasa ratiba, majimbo yaliyogawanywa, watumishi wala vituo vya uchaguzi bado haviwekwa bayana na wala haifahamiki kazi ya uandikishaji katika Daftari la Wapigakura halijakamilika katika mikoa miwili

Shule na intaneti, Serikali kuzifuta kampuni zisizofikisha mawasiliano vijijini

Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
MIKAKATI ya serikali ya kutoa wataalamu wengi wa sayansi imeendelea kutetekelezwa kwa kasi, ambapo imetia saini mikataba kusambaza huduma za mtandao kwenye shule mbalimbali nchini.

Mikataba hiyo iliyotiwa saini jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, iko miwili ya kupeleka huduma za mawasiliano vijijini na kuunganisha mtandao wa intaneti katika shule utakaogharimu sh. bilioni 26.28.

Katika mikataba hiyo, serikali imeonya kuwa itazifuta kampuni ambazo zitashindwa kutekeleza makubaliano ya kufikisha mawasiliano kwa wakati katika vijiji 480 vilivyoainishwa.

Onyo hilo la serikali linatokana na kampuni hizo kushindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wa kupeleka huduma za mawasiliano vijijini, ambapo nyingi zimetekeleza kwa asilimia 50 tu.

Akizungumza wakati wa kutia saini mikataba hiyo, Profesa Mbarawa alisema awamu ya tatu ya kupeleka mawasiliano vijijini utahusisha kata 102 ambapo vijiji 480 vitanufaika nayo.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ulihusisha kata 52, ambao ulitekelezwa mwaka 2013 na umekamilika kwa asilimia 99.05 na awamu ya pili ilihusisha kata 86 na ulitakiwa kukamilika mwaka jana na hadi sasa umetekelezwa kwa asilimia 50.

“Awamu ya kwanza kuna kata nne kati ya 52 ambazo bado hazijamazilizika, jambo ambalo halikubaliki na kama mtu ameshindwa kutekeleza mkataba wake afungiwe na katika hili sitakubali,” alisema.

Mkataba wa mradi huo ambao utahusisha kata 102 na kugharimu sh. bilioni 14.02 umesainiwa kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF) na kampuni za utoaji huduma za mawasiliano.

Kampuni zilizotia saini mkataba wa utoaji huduma ya mawasiliano kwa awamu ya tatu na idadi ya kata katika mabano ni Tigo (42), Vodacom (36), TTCL (19) na Airtel (5).

Alisema bado kuna changamoto kubwa ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini, hivyo kuzitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatekeleza mikataba ili kila mwananchi apate huduma popote alipo.

Waziri huyo alisema katika kuhakikisha huduma ya mawasiliano inawafikia wananchi wote, serikali ilianzisha utoaji wa ruzuku kwa kampuni zinazotoa husika ili kupeleka mawasiliano kwenye maeneo yenye uchumi hafifu.

Alisema serikali kupitia UCAF itatoa ruzuku ya asilimia 100 ambayo inatolewa kulingana na eneo yakiwemo maeneo ya mipakani ambayo ni lazima yawe na mawasiliano wakati wote ili kuimarisha ulinzi na usalama.

Alisema UCAF ilianzishwa mwaka 2006 ambapo hadi mwaka 2010 anaingia katika wizara hiyo hakukuwa na kazi yoyote iliyotekelezwa ambapo alilazimika kubadilisha uongozi jambo ambalo limeleta mafanikio na sasa mawasiliano yanaendelea kufika kwa wananchi.

“Ni mafanikio makubwa yaliyopatikana itakuwa kichekesho kwa waziri atakayekuja ashindwe kufanya vizuri zaidi, na akishindwa kuna tatizo kwa sababu sasa teknolojia imebadilika,” alisema.

Awali, Mtendaji Mkuu wa UCAF, Mhandisi Peter Ulanga, alisema mbali na kutia saini mkataba na kamapuni za mawasiliano, pia waliingia mkataba na kamapuni ya Avanti inayotoa huduma za mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuziunganishia shule 250 za serikali. 

Pia alisema wataanzisha vituo 25 vya kufundishia walimu wa masomo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, mradi unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya UCAF, Profesa John Nkoma, aliwaomba wananchi wabadilike na kutumia huduma ya intaneti kwa faida na si vinginevyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. John Mngodo, alisema huduma ya kuunganisha intaneti katika shule za serikali itasaidia kuboresha elimu.
 l