Aliyekuwa Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alihamia CHADEMA
hivi karibuni ameamua kurejea katika chama chake cha zamani kwa madai
alikosea njia.
Nkumba ambaye alihamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni kugombea ubunge Sikonge, aliteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA lakini wanachama wa chama hicho walipinga kitendo cha Kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani kumteua wakitaka mgombea wao, Hijja Ramadhan arudishwe jambo lililofanya Nkumba kuondolewa na kukosa nafasi ya kugombea ubunge.

Nkumba alipojitoa CCM alisema
alikipenda kwa dhati chama hicho lakini hakuona sababu ya kuendelea
kubaki kwa kuwa hasikilizwi na hakina mapenzi na watu.
Lakini akizungumza Dar es Salaam jana, Nkumba alisema amerudi nyumbani kwa kuwa alipotea njia na hakuona kama kuna mwelekeo CHADEMA
Alipoulizwa kuhusu kupewa jimbo na CHADEMA alisema hayo yaachwe, amerudi nyumbani kwa kuwa ni kama rebound katika mchezo wa kikapu na watu wanaendelea kucheza.

- Taarifa hii imenukuliwa kutoka gazeti la MWANANCHI
No comments:
Post a Comment