Jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa
Syria vimekomboa misikiti mitatu iliyokuwa chini ya udhibiti wa kundi
la kigaidi na kitakfiri la Daesh, mashariki mwa mji wa Damascus.
Duru za kijeshi zimeripoti kuwa, misikiti iliyokombolewa na
jeshi la Syria ni ile ya al-Noman, al-Hussein na al-Qassem, iliyoko
katika eneo la al-Qaboun, mashariki mwa Damascus.
Habari zaidi zinasema kuwa, magenge hayo ya kigaidi yamekuwa yakiitumia misikiti hiyo kupanga njama na harakati zao za kigaidi.
Wakati huo huo, jeshi la Syria limefanikiwa kutibua shambulizi la
kigaidi ambalo Daesh ilikuwa inataka kutekeleza katika mkoa wa mashariki
wa Dayr al-Zawr. Mashambulizi ya mabomu yalitokea mjini
Damascu Jumamosi ikliyopita na kuua na kujeruhi makumi ya raia wasio na
hatia.
Haya yanajiri katika hali ambayo, duru ya tatu ya mazungumzo ya
Astana inatazamiwa kuanza leo Jumatano kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa
Iran, Russia na Uturuki pamoja na mwakilishi wa Jordan, Bashar
al-Jaafari anayeiwakilisha serikali ya Syria na mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa.
Duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria ya Astana ilifanyika
tarehe 23 na 24 Januari na ile ya pili ilifanyika tarehe 15 na 16
Februari katika mji mkuu wa Kazakhstan.
No comments:
Post a Comment