Wednesday, August 26, 2015
Tuesday, August 25, 2015
Said Nkumba arudi CCM, Kutoka CHADEMA
Aliyekuwa Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alihamia CHADEMA
hivi karibuni ameamua kurejea katika chama chake cha zamani kwa madai
alikosea njia.
Nkumba ambaye alihamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni kugombea ubunge Sikonge, aliteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA lakini wanachama wa chama hicho walipinga kitendo cha Kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani kumteua wakitaka mgombea wao, Hijja Ramadhan arudishwe jambo lililofanya Nkumba kuondolewa na kukosa nafasi ya kugombea ubunge.

Nkumba alipojitoa CCM alisema
alikipenda kwa dhati chama hicho lakini hakuona sababu ya kuendelea
kubaki kwa kuwa hasikilizwi na hakina mapenzi na watu.
Lakini akizungumza Dar es Salaam jana, Nkumba alisema amerudi nyumbani kwa kuwa alipotea njia na hakuona kama kuna mwelekeo CHADEMA
Alipoulizwa kuhusu kupewa jimbo na CHADEMA alisema hayo yaachwe, amerudi nyumbani kwa kuwa ni kama rebound katika mchezo wa kikapu na watu wanaendelea kucheza.

- Taarifa hii imenukuliwa kutoka gazeti la MWANANCHI
Mh.Lowassa akiwa ndani ya daladala alilopanda Kituo cha Gongolamboto mwisho kuelekea Chanika
![]() |
| Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala. |
Mafuriko Nyumbani kwa Mh.Pinda
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitiaChama cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa
kampeni wa Chama hicho uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi leo ambapo amehutubia mikutano ya hadhara mitatu katika
mkoa huo katika maeneo ya Mishamo, Katumba na Mpanda mjini.
Dr.
Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili ashinde na
shughulika na matatizo ya wananchi kwakuwa anayaelewa matatizo na
shida nyingi za watanzania, Dr. Magufuli ameahidi kukamilisha ujenzi wa
barabara za Kasulu -Mpanda, Sumbawanga – Mpanda , Mpanda -Tabora ili
zikamilike kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia wananchi katika
shughuli mbalimbali za kiuchumi mkoani humo PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-KATAVI
Monday, August 24, 2015
Sunday, August 23, 2015
ACT-Wazalendo wavuna Wanachama 500 kutoka CHADEMA
Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani
Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.
Zaidi
ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani
Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.
Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.
Hata mara baada ya wanachama hawa kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA. chanzo EATV

Friday, August 21, 2015
Mh.Mbatia awaonya Viongozi wa UKAWA
Wakati Umoja wa Katiba
ya wananchi UKAWA ukikumbwa na changamoto ya ugawanaji wa majimbo baada ya
maeneo mengi nchini Tanzania kuibuka migogoro mara baada ya majimbo ya uchaguzi
kugawanywa kwa vyama hivyo,hatimaye mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI ambaye
ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo ameibuka na kutoa onyo kali kwa viongozi
ambao wanakuwa wabinafsi wa kutokutaka kuachiana majimbo na kusema kuwa
ubinafsi ni jambo ambalo halitaendekezwa ndani ya umoja huo.
Akizungumza na
wanahabari leo jioni hii Dar es salaam amesema kuwa mara baada ya kukamilika
kwa kazi ya kugawana majimbo kwa vyama vinne vinavyounda umoja huo kumeibuka
sintofahamu ya baadhi ya watu kungangania majimbo ambayo tayari wamepewa watu
wengine jambo ambalo amesema kuwa sio makubaliano ya umoja huo na hawatavumilia
viongozi wa namna hiyo.
Amesema kuwa moja ya
maazimio makubwa ya umoja huo ni kuepuka ubinafsi na kuhakikishya kuwa mambo
wanayoyahubiri kwa wananchi wanayatekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na amani
na umoja hivyo hawako tayari kuona chama au mtu yoyote anaanzisha vurugu ndani
ya umoja huo.
Amesema Tayari leo
jioni viongozi wakuu watakutana kuona ni jinsi gani wanaweza kushughulikia
jambo hilo ili ndoto za watanzania za kuhakikisha kuwa wanauondoa mfumo dhalimu
wa CCM uliopo kwa sasa zinatimia na nchi inakuwa na amani na utulivu mkubwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)