Tuesday, September 8, 2015

Baadhi ya Wananchi wa Karatu hawajaridhishwa na Maamuzi ya Dr. Slaa

Wananchi katika jimbo la Karatu wamekosoa uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk Slaa kumshambulia mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa.
Wakazi hao wa Karatu wamemkataa Dk Slaa kwa kudai kuwa uamuzi aliouchukua hausaidii katika harakati za kuikondoa CCM madarakani bali inazirudisha nyuma juhudi hizo.
Kwa mujibu wa The Citizen, wananchi waliofanya mahojiano kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa hawatabadili msimamo wa kuiunga mkono ngome ya Ukawa kama alivyotaka Dk Slaa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15 tangu mwaka 1995.
“Ni bora tuwe na mafisadi wachache walioko upinzani kuliko kuwa na mafisadi zaidi ya 100 ambao bado CCM inawakumbatia,” alisema Isack Philip, mkazi wa kata ya Rhotia, Karatu.
Wananchi wengine walifika mbali kwa kuonesha jinsi wasivyounga mkono CCM wakidai wako tayari hata kuchagua jiwe badala ya chama hicho tawala.
“Tuko radhi kuchagua jiwe badala ya CCM ambayo tangu tupate uhuru imekuwa ikituangusha katika kupata maendeleo,” alisema muendesha bodaboda aliyejitambulisha kwa jina la Emanuel Bayo na kuongeza kuwa madai ya Dk Slaa hayana mashiko wakati huu.
Wananchi wengi waliofikiwa na gazeti hilo walieleza kuwa nia yao ni kuhakikisha wanaona CCM ikiondolewa madarakani na sio vinginevyo.
Hata hivyo, mwenyekiti wa zamani wa CCM katika wilaya hiyo, alimtetea Dk Slaa na kueleza kuwa anatoa mawazo na mtazamo wake kwa lengo la kuwaonesha watanzania hali halisi.
Hivi karibuni, Dk Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema alijitokeza hadharani na kupinga uamuzi wa chadema kumpokea Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais licha ya kukiri kuwa yeye ndiye aliyelipeleka wazo hilo kwa uongozi wa chama chake ambacho kilikuwa kimemteua yeye kugombea nafasi hiyo. Chanzo, http://dar24.com/karatu-yamwaga-dk-slaa/



Bw Alkado Ntagazwa"Mpigieni Kura Muslim Hassanali wa UKAWA"

Muslim Hassanali, Mgombea ubunge jimbo la ilala kwa Tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA
Wakati kampeni za uchaguzi mkuu zikiwa zimepamba moto katika maeneo mbalimbali nchini chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika manispaa ya Ilala kimewataka wakazi wa manispaa hiyo  kukipa ridhaa ya kumchagua mbunge wake anayekiwakilisha ili kiweze kuwaletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na mzamini wa chama hicho Bw Alkado Ntagazwa wakati wa mkutano wa chama hicho wa kumnadi mgombea wa  chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vinanyounda ukawa Bw HASSANARI maarufu kama ROFA WA ILALA  uliofanyika katika viwanja vya soko la karume jijini Dar es salam,
 Bw ntagazwa amesema kuwa wananchi wa eneo hilo hawapaswi kukosea tena na kukichagua chama cha mapinduzi kwa kuwa kimewaletea umasikini mkubwa ambao wanauona hadi sasa.Bw ntagazwa aliwambia wakazi wa eneo hilo kuwa miaka ya nyuma elimu ilitolewa bure kwa watu wote kwanini isiwe sasa? Bw ntagazwa alihoji.
 Ntagazwa amewaomba wakazi wa manispaa ya ilala kutokosea kama ambavyo uwa wanafanya miaka mingine.Kwa upande wake mwenyekiti wa  wa vijana wa chama cha chadema Bw mwita amesema kama wananchi wa eneo hilo wataamua kukipigia kura chama chake katika nafasi zote watakuwa wamejiondoa kwenye matitizo mabalimbali kama kitendo cha kufukuzwa mara kwa mara na mgambo wa jiji kwenye maeneo yao ya kufanyia shughuli zao.

Mwita alibainisha kuwa watanzania wengi wana maisha magumu huku akiwataka polisi waache kutumika na badala yake wasimamie kanuni na taratibu za utekelezaji wa majukumu yao tofauti na ilivyo sasa Kwa upande wake mgombea wa ubunge wa jimbo hilo bw Hassanari amesema kuwa uwa anajisikia vibaya sana pale anapoona kuwa wakazi wa emeo hilo wananyanyasa na mgambo wa jiji huku wakiwa na uhalali wa kuishi kwa uhuru na haki katika maeneo yao.

Bw Hassanali ameongeza kuwa jambo la kwanza atakalolifanya kama atapewa ridhaa na wana ilala ni kuhakikisha kuwa fedha za maendeleo zinawafikia walengwa bila kuguswa na wajanja wachache.Huku akishangiliwa na wafanyabiashara na wananchi waliohudhuria mkutano huo bw hassanari alijinasibu kuwa yeye ndo muarobaini wa matatizo yote ya wakazi wa eneo hilo hivyo wana ilala hawakiwi kufanya makosa tena katika uchaguzi wa mwaka huu

Wednesday, September 2, 2015

Raisi Jakaya Kikwete Aagwa Na Vyombo VyA Ulinzi Na Usalama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo.
[Picha na Ikulu.]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (wan ne kushoto) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kupokea salamu ya heshma ya kwaride la Vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa ulipopigwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa rasmi leo.

Askari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete alipoagwa rasmi na Vikosi hivyo leo,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (wan ne kushoto) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kupokea salamu ya heshma ya kwaride la Vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa ulipopigwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa rasmi leo.

Dk. Wilbroad Slaa Astafu Siasa,hamkubali Lowassa

Hatimaye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa ametangaza kustaafu rasmi siasa baada ya chama hicho kumpokea Edward Lowassa na timu yake anayodai ni timu ya mafisadi.
 Alifafanua kuwa alihoji maswali mengi na kutaka majibu kama wangetaka akubaliane na mapendekezo yao. Suala kubwa alilohoji ni iwapo ujio wa Lowassa na watu wake ni mtaji kwa chama hicho au ni mzigo kwa chama hicho lakini hakupewa majibu.

 Amesema baada ya viongozi hao wa Chadema kumshawishi kuwa Lowassa angekuja na timu kubwa ya wabunge 50 walioko madarakani hivi sasa kwa tiketi ya chadema pamoja na wakuu wa wilaya kadhaa, aliwataka wamletee majina yao pamoja na sharti la kuwataka kutangaza kuhama CCM kabla ya mchakato wa kura za maoni za kuwapata wabunge.
 Amesema hata hivyo walishindwa kufanya hivyo na kisha kuamua kushiriki mchakato wa kura za maoni huku wakihama baada ya majina yao kukatwa jambo ambalo amedai limefanya Chadema kuendelea kupokea ‘makapi’ ya CCM.

Alisema Lowassa ndiye kinara aliyelazimisha kampuni hewa la Richmond kupewa tenda ya kufua umeme wa dharura ingawa Tathmini ya Tenda ilionesha kuwa kati ya makampuni 8 yaliyofikia hatua ya tathmini, kampuni hiyo ilikosa vigezo na kupata marks 0. Kwamba alitumia uwaziri mkuu kuhakikisha wanapata tenda hiyo iliyoitia hasara kubwa serikali.
Aidha, Dk. Slaa amesisitiza kuwa kamati Mwakyembe ilitoa ripoti ya kweli na kwamba yapo baadhi ya mambo ambayo hawakuyaweka wazi na vielelezo anavyo kwa kuwa vigogo 27 walihusika na wizi huo.
Amemtaka Lowassa kujitokeza hadharani na kutaja kwa majina ya viongozi wa ngazi za juu anaodai kuwa walishinikiza kusainiwa kwa mkataba wa Richmond badala ya kuendelea kuwaficha.

“Ajitokeze asema kwa majina hao viongozi wa ngazi za juu zaidi ya waziri mkuu ni nani na nani, aseme kwa majina kwa sababu waio juu ni Rais na makamu wa rais, nani aliyeelekeza? Amtaje,” amesema Dk. Slaa.
 Dk. Slaa alihitimisha kwa kutangaza rasmi kustaafu siasa za vyama na kueleza kuwa ataendelea kushiriki katika harakati za kulikomboa taifa bila kujihusisha na chama chochote cha siasa huku akimtaka Lowassa kujitokeza hadharani kujibu alichokisema na kwamba akifanya hivyo atamrudia tena na mengine ambayo hajayatoa hadharani.

Tuesday, September 1, 2015

Watanzania Wote kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa Amani

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza 
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana  
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
Habari Kamili

GLOBAL  Peace  Foundation Tawi
la  Tanzania  (GPFTZ), kwa kushirikiana  na
Mshirika  wake, Baraza  la  Wadhamini  la
Taasisi  ya  Viongozi  wa  Dini  Tanzania (IRCPT),  
wamezindua  kampeni  ya
kuhamasisha  Amani  nchini  Tanzania  katika
kipindi  hiki  kuelekea  uchaguzi  mkuu  ,
jina  la  kampe
ni  ni  “Amani Kwanza”.  
Lengo  kuu  la  kampeni hiyo  ni  kuhamasisha  watanzania  wote
kushiriki    katika  Uchaguzi  Mkuu  kwa
Amani  ambao  unatarajia  kufanyika  siku  ya
25/08/2015.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi  alisema Walengwa  wakuu  wa
Kampeni  hiyo  ni  Wanawake  na  Vijana 
ambao  ni  wengi
zaidi  ukilinganisha  na  rika  na  makundi
mengine,  na  pia  Wanawake  wamekuwa
wakihathirika zaidi  endapo  inapotokea  machafuko
hali kadhalika  Vijana  wamekuwa  chanzo
        cha  uchochezi  wa
machafuko  katika  nchi  mbalimbali  duniani.
 
“kampeni  hii  haina lengo  lolote  la  kuunga  mkono    ama
kupinga  Chama  chochote  cha  Kisiasa  au
mgombea  wake,  na  wala  haina  mahusiano
yoyote  ya  kisiasa na kauli k
auli  mbiu  yake ni “KURA  YANGU  UZALENDO
WANGU,  AMANI  YA  NCHI  YANGU  NI  JUKUMU
LANGU” alisema Nghambi.
Nghambi alisema Kampeni hiyo  imeandaliwa
maalumu  kwa  malengo  ya k
uwahamasisha  Wanawake
na  Vijana  kuwa  mabalozi  wazuri  wa
kulinda  na  kuitetea  Amani  ya  nchi
yetu  hasa  katika  kipindi  hiki  kuelekea  uchaguzi
Kujiepusha  na  vitendo  mbalimbali    ambavyo
vinaweza  kuchochea  uharibifu  wa  Amani
nchini Kuhamasisha  
kila  mmoja  ashiriki
uchaguzi  kwa  amani Ili  kuhakikisha.  
Alisema kampeni hiyo inafanikiwa  kutokana na Shirika  la Global  Peace kushirikiana kwa
karibu  na  vyombo  vya  habari  nchini
vikiwemo  Radio,  Luninga,  Magazeti,  na
mitandao  mbalimbali    ya  Kijamii  ikiwemo 
Twitter,  Face  Book,
instagram  na  YouTube.  
Alisema  shirika hilo ni Tawi la  Taasisi  ya  Kimataifa  isiyo ya  Kiserikali  na
isiyotengeneza  faida  Global  Peace  Foundation
(GPF)  yenye  makao  makuu  yake
Washington  DC,  nchini  Marekani.    
Alisema  shirika  hilo linahamasisha  kutetea  na  kulinda  Amani  dunia
,    shirika  hili  linaamini  ya  kuwa “ 
Kwa  Mungu  sisi
wote  ni  familia  moja” GPF  inafanya  kazi
kwa  karibu  na  mitandao  ya  kiserikali
na  watu  binafsi  katika  kuendeleza  jamii,
taifa  na  katika  kujenga  na  kulinda  misingi
na  maadili  katika  jamii  husika.
GPF  ina  rekodi nzuri  ya  kufanya  kazi  kwa  karibu  na
kwa  mafanikio  makubwa    kuhamasisha  na
kulinda  Amani  katika  nchi  mbalimbali  dunia
katika  bara  la  Afrika,  Asia,  Ulaya  na Amerika.
Kwa  upande  wa Afrika,  shirika  hili  limekuwa  likijihusisha
na  maswala  mbalimbali  ya  kijamii  katika
nchi  za  Kenya,  Uganda  na  Nigeria
kudumisha  Amani  kwenye  ukanda  wa  Afrika.


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na  Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.Chanzo Habari24

Wednesday, August 26, 2015

Mh. Makufuli akiwa Mbeya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI BLOG