Friday, October 24, 2014

BILAL MUSLIM MISSION YA TANZANIA YALAANI HUKUMU YA KIFO KWA SHK. NIMR

aasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania inaungana pamoja na watafuta haki na usawa wote duniani kuonesha mshituko wao kwa hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqr Al-Nimr kwa madai yake ya kutaka haki na usawa kwa wananchi nchini Saudi Arabia 


Tunaomba muungano wa wapenda haki na usawa duniani kote kuitaka mamlaka ya Saudi Arabia kufuta hukumu ya kifo kwa Sheikh Al-Nimr. Na kuwa serikali nchini humo imuachie kwa moyo wa kidemokrasia, maadili na kanuni kama zilizoanishwa katika tangazo la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa.

Kusiwe na Taifa katika Umoja wa Mataifa ambalo litajiwekea utawala wa kisiasa ambao si wa Jamhuri ya kidemokrasia. Vinginevyo ni uvunjwaji wa haki za binaadamu. 

Asibughudhiwe mtu kwa kusimama kwake na kutete haki za binaadamu kwa kiasi cha uhuru wake wa kidemokrasia, kujitegemea na usawa wa watu na haki zao. 

Binadamu wawe ni familia moja katika kuhifadhi haki ya utu wao, Haki ya uhuru wa kujieleza, Haki ya Kidemokrasia, Matakwa binafsi na Utawala wa kujitegemea. Chanzo cha habari.
chanzo afroshia.

JA'FARI: TANZANIA NI LANGO LA KUINGIA AFRIKA MASHARIKI.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema kuwa, Tanzania ni lango la kuingizia bidhaa za Kiirani katika eneo la Afrika Mashariki.
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania Mehdi Agha Ja'fari
 
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amezungumzia uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi muhimu mno kwa ajili ya kusafirisha na kupeleka nje bidhaa za Iran zisizo za mafuta na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa lango la kuingiza bidhaa za Kiirani huko Afrika Mashariki.
 
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amesema, Tanzania na bandari ya Dar es Salaam kuwa pambizoni mwa bahari ya Hindi na kuwa kwake karibu na maeneo ya kiuchumi ya magharibi mwa Asia hususan Ghuba ya Uajemi ni sifa nzuri zinazotayarisha mazingira bora ya kufanyika biashara kati ya Tanzania na Iran. 
 
Balozi wa Iran mjini Dar es Salaam amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa, usafirishaji wa bidhaa zisizo za mafuta za Iran kuelekea Tanzania umeongezeka mno katika kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni. Chanzo cha habari:
chanzo Afroshia
Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania inaungana pamoja na watafuta haki na usawa wote duniani kuonesha mshtuko wao kwa hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqr Al-Nimr kwa madai yake ya kutaka haki na usawa kwa wananchi nchini Saudi Arabia
Tunaomba muungano wa wapenda haki na usawa duniani kote kuitaka mamlaka ya nchini Saudi Arabia kufuta hukumu ya kifo kwa Sheikh Al-Nimr. Na kuwa serikali nchini humo imuachie kwa moyo wa kidemokrasia, maadili na kanuni kama zilizoanishwa katika tangazo la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa.
Kusiwe na Taifa katika Umoja wa Mataifa ambalo litajiwekea utawala wa kisiasa ambao si wa Jamhuri ya kidemokrasia. Vinginevyo ni uvunjwaji wa haki za binaadamu.
Asibughudhiwe mtu kwa kusimama kwake na kutete haki za binaadamu kwa kiasi cha uhuru wake wa kidemokrasia, kujitegemea na usawa wa watu na haki zao.
Binadamu wawe ni familia moja katika kuhifadhi haki ya utu wao, Haki ya uhuru wa kujieleza, Haki ya Kidemokrasia, Matakwa binafsi na Utawala wa kujitegemea.
- See more at: http://www.dunialeo.com/sw/posts/browse/local-news/bilal-muslim-mission-ya-tanzania-yalaani-hukumu-ya-kifo-kwa-shk-nimr-1#sthash.M7BGl1Aw.dpuf

Thursday, October 23, 2014

Mamia ya Waislamu Waandamana

Mamia ya Waislamu jana walifanya maandamano makubwa mkabala wa Ubalozi wa Saudi Arabia mjini London, Uingereza wakipinga adhabu ya kifo iliyotolewa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo dhidi ya Sheikh Nimr Baqer al Nimr mwanachuoni mashuhuri wa nchini Saudi Arabia. 
Sheikh Nimr Baqer al Nimr. 

Waandamanaji hao walipiga nara za 'Mauti kwa utawala wa Aal Saud' na ' Sheikh Nimr aachiliwe huru' sanjari na kubeba mabango na maberamu yaliyo dhidi ya utawala wa kifalme wa Saudi Arabia, walisisitiza juu ya kuachiliwa huru mwanachuoni huyo.

 Waandamanji hao sanjari na kuutaja utawala wa Saudi Arabia kuwa mvunjaji mkuu wa haki za binadamu na unayaunga mkono makundi ya kigaidi, wameitaka serikali ya Riyadh kumuachilia huru Sheikh Nimr Baqer al Nimr. 

Kijana mmoja wa Kimarekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo amelalamikia jinsi nchi zinazojinadi kuwa watetezi wa haki za binadamu kama vile Marekani na Uingereza kwa kunyamazia kimya hukumu hiyo ya kidhuluma 

Na kusisitiza kwamba kimya hicho kinaonyesha wazi kuwepo mashirikiano kati ya madola hayo ya Magharibi kwa utawala huo wa kifalme katika kutenda jinai na kuwakandamiza wananchi wa Saudia. Kijana huyo amesema na hapa tunamnukuu:

 ' Mimi siyo Muislamu na wala Mwarabu, lakini naamini kwamba Sheikh Nimr ni kiongozi huru ambaye amedhulumiwa na utawala katili na wa kifalme wa Saudi Arabia', mwisho wa kunukuu. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yamelaani vikali hukumu hiyo ya kidhuluma iliyotolewa dhidi ya mwanachuoni huyo. Chanzo cha habari:

Monday, October 20, 2014

Mubahala, ushindi mkbwa

Wanafunzi, wanaharakati na jamii wakiwa katika kusikiliza kwa makini tukio la Mubahala (Maapizano) leo Tandika Temeke Dar-es-slaam.




Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Khom Samahat Sheikh Hemed Jalal akifafanua juu ya Tukio la Maapizano yalitokea kipindi cha mtume (s.a.w.w)

Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Khom Samahat Hemed Jalala akipeana mkono na Sheikh Abdullatwif Issa Swalehe (kushoto) wa Bilala Muslim Mission of Tanzania.

Sheikh Abdullatwif Issa Swalehe wa Bilal Muslimu Mission of Tanzania akielezea umuhimu wa maapizano kati ya mtume (s.a.w.w) na wakristo.

Habari Kamili

Waumini wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah leo wameungana na Waislam wenzao ulimwenguni kote kusherehekea Ushindi wa tukio la Mubahala, Sherehe hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Marehemu Sheikh Dhikir Kihondo Temeke jijini Dar es Salaam.

Sheikh Hemed Jalala amesema katika sherehe hiyo : kitendo cha Mtume (s.a.w.w) kutoka na watu wanne na asiwachague watu wengine wakawaidia akakae meza moja na Manaswara baada ya kushindwa Manaswara na Mtume (s.a.w.w) akaacha kuwatoa manaswara katika ardhi ya Madina wakabakia kuishi katika mji wa Najiran 

 Amesema Waislam watashinda Waislamu wataonekana watendaji wazuri watakapokuwa wamekusanywa na mwamvuli wao mmoja Waislam watakuwa tishio duniani na wataheshimiwa ndani ya nchi zao.

jalala amesema Watakapoitumia falsafa na hekima ya Mtume (s.a.w.w) ya kukaa na watu ambao wanatofautiana nao kiitikadi wakakaa nao meza moja wakazungumza nao Mtume (s.a.w.w) alikuwa na uwezo wa kuwafukuza Wakristo wa Najiran .

Aidha amesema Mtume (s.a.w.w) alikaa nao meza moja akakaa nao Madina Mtume (s.a.w.w.)hajawalazimisha Wakristo wa Najiran waingie katika Uislam ambapo alikuwa na uwezo wa kunyanyua upanga na kuwaambia tamkeni shahada mbili akuwalazimisha kwa sababu hakuna kulazimishana katika dini.
 
Amesema ni makosa makubwa kuwepo fikra kwamba ni lazima kuwasilimisha watu kwa nguvu wawe Waislam ni makosa makubwa hakuna katika Uislam, Uislam hausemi ya kwamba twende tukawauwe watu hili wawe Waislam.

Ameongeza kuwa  vita vyote alivyopigana Mtume (s.a.w.w) vilikuwa ni vita vya kujilinda Warabu walimkataza Mtume (s.a.w.w) asitangaze neno la Mungu kwa makatazo hayo alipambana nao Mtume (s.a.w.w) hajatoka kuwapiga watu waingine.

"Wakristo wa Najiran waliposhindwa Mtume (s.a.w.w) hajawaambia kwamba ingieni katika Uislam kwamba lazima muwe Waislam au nitawauwa bali Mtume (s.a.w.w)" amesema Jalala.

Kasisitiza kuwa Mtume aliwaambia mkiingia katika Uislam mna haki zote kama Waislam wengine wakawaida katika kumbukumbu ya kuukumbuka ushindi wa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul Bayt (a.s) kwa manaswara wa Najiran tujifunze hekima hii kubwa ya kuvumilia kuweza kukaa pamoja na adui bali na mtu ambaye unatofautiana naye kukaa katika meza moja

Sunday, October 19, 2014

Dua ya kumrehemu Sheikh Dhikir Kiondo

Sheikh wa Bilala (kushoto) Tandika Temeke, Dar es salaam, akiwa katka kisomo cha Muasisi wa Tanzania Ithnashery Community (T.I.C), Nyumbani kwa Marehemu Dhikir Kiondo.

Masheikh ,Wanafunzi na Majirani wa Marehemu Sheikh Dhikir Kiondo, wakimsomea kisomo cha Qur'an ya kumrehemu.

Mwalimu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (kushoto) akiwa na mjunbe wa kata ya Tandika, Temeke wakimsomea kisomo cha Qur'an Sheikh Dhikir Kiondo kwa kumrehemu.

Wanaharakati wa kike,Wanafunzi wa Hauza wa Hauza ya Imam Jafar Swadiq wakiwa pamoja katika kumrehemu muasisi wa T.I.C Sheikh Dhikir Kiondo

Huyu ndio Sheikh Dhikir Kiondo, muasisi wa Taasisi ya Tanzania Ithnashary Community (T.I.C)

Sunday, June 22, 2014

Uganda yapuuzilia mbali vikwazo vya Marekan




Serikali ya Uganda imepuuza vikwazo ilivyowekewa na serikali ya Marekani kutokana na kupitisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja. Ofwono Oppondo, msemaji wa serikali ya Uganda amesema kuwa, vikwazo vya Washington dhidi ya nchi yake, vitakuwa na taathira ndogo tu kwa uchumi wa Uganda. 

Ofwono pia amekadhibisha tuhuma zisizo na msingi zilizotolewa na Marekani kwamba vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi ya watu wa jinsia moja wanaojamiana hasa baada ya kupitishwa sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo vichafu vimeongezea nchini Uganda na kusema kuwa, madai hayo ni ya kipuuzi. Amesisitiza kuwa, kuanzia sasa Waganda watajidhaminia wenyewe mahitaji hayo na hawatakubali kufanywa watumwa wa wafadhili. 

Sheria ya kupiga marufuku liwati na usagaji nchini Uganda ilipasishwa mwezi Februari mwaka huu. Hata hivyo madola ya Magharibi kama vile Denmark, Norway, Uholanzi, Sweden na Marekani zilipinga vikali hatua hiyo. 

Juzi Marekani ilipasisha muswada wa kuiwekea vikwazo serikali ya Kampala na kukata misaada yake ya kifedha kwa nchi hiyo. irib



Friday, June 20, 2014

Umoja wa watu ni kinga kwa Taifa

Hawa ni baadhi ya watu waliohudhuria katika semina hiyo na wakwanza kulia ni Sheikh Omari Sungura.
Semina ya kujenga umoja na mshikamano baina ya Waislamu na dini zote za mbinguni imefanyika usiku huu wa tarehe 18/06/2014 mjini Posta,jijini Dar es Salaam, Katika Semina hiyo viongozi wa kidini wametakiwa kutoa elimu katika jamii kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa ulimwenguni, viongozi hao wametakiwa kufichua njama dhidi ya makundi haramu yaliyojivisha sura ya Uislamu.

Sheikh Hemed Jalal akiwa akionekana kuwa ni miongoni wa wasikilizaji mahiri katika semina hiyo na wakwanza na mwalim mkuu wa chuo cha Jamia-Mustafa kilichopo upanga jijini Dar es salaam

Sheikh Mulaba akiendelea kuwakaribisha wazungumzaji katika semina hiyo akiwa ni Mc ambayo watu waliodhuhuria semina hiyo yakadiriwa kuwa ni 150 kwa uchache

Hawa ni baadhi ya Wanawake ambao waliohudhuria kaitka semina hiyo ambayo wanaonekana kuwa makini katika usikivu wao.Picha na afroshia