Saturday, April 11, 2015

sherehe kuzaliwa kwa Fatma (a.s)

Sheihkh wa Hawzat Imamu Swadiq (a.s) Abdullatwif Swalehe akimshukuru Allah (swt) kwa kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bibi Fatma (a.s) Fatma alizaliwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Bibi Khadija, tarehe 20, Jamadul Akhirah..
Wanafunzi wa Hawzat Imamu Swadiq (a.s) waiimba Qawsida ya kuelezea namna Bibi Fatma (a.s) alivyozaliwa.Sherehe hizo zimeandaliwa na Hawzat Imam Swadiq (a.s), Kigogo-Post, Dar es salaam.

Waumini wa Dini ya kiislam, wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq(a.s) waikiwa makini kusikiliza mawaidha ya masheihjuu ya tokio la kuzaliwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bibi Fatma Zahra (a.s)

Keki ilyoandaliwa kwa kusherehekea kuzaliwa kwa Mwanamke bora Kuliko mwanawake wote Ulimwenguni Bibi Fatma (a.s)

Sheikh wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Said Othmani akikata Keki Iliyoandaliwa kwa Mnasaba wa Kukumbuka Kuzaliwa kwa Fatma (a.s)

Thursday, April 9, 2015

Kukaguliwa vituo vya kijeshi, mstari mwekundu Iran



Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kukaguliwa vituo vya kijeshi ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya IranBrigedia Jenerali Hussein Dehqan

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan ameelezea madai ya uwongo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Magharibi likiwemo gazeti la Guardian la Uingereza ya kukaguliwa vituo vya kijeshi vya Iran 

ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya Lausanne nchini Uswisi na kusisitiza kwamba, kamwe hayakufikiwa makubaliano kama hayo. 

Brigedia Jenerali Dehqan amesisitiza kwamba, suala la kukaguliwa vituo vya kijeshi hapa nchini, ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya Kiislamu. 

Hivi karibuni yalifikiwa makubaliano kati ya Iran na kundi la 5+1 ambapo moja kati mafanikio makubwa iliyoyapata Iran kwenye makubaliano hayo, ni kwa nchi hizo sita zenye nguvu duniani kuitambua rasmi miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani.





Wednesday, April 1, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s) yakumbuka Kifo cha Jafar Ibn Abi Twalib

Mwalimu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Sheihk Saidi Athumani akitoa hutuba juu ya kifo cha Jafar Ibn Abu Twalib.     Kumbuumbu hizo Zimeandaliwa Na Hawzata Imam Swadiq (a.s) na zimefanyika leo Msiitini Ghadir, Kigogo-Post, Jijini Dar es salaam.  

Waumini mbalimbali pamoja na Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakiwa makini kusikiliza simulizi yenye majonzi ambayo Jafar Ibn Abu Twalib, aliuliwa katika Vita Vya Muu'tah, kwa kukatwa mikono yake Miwili.
Sheikh Saidi Athumani akionesha kwa mfano njia aliouwa akipigania Jafar Ibn Abu Twalib, kuwa ni njia iliyonyoa, ambayo ni  ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Jafar Ibn Abu Twalib alipewa jina na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Baba wa Masikini, kwani alikuwa anawapenda, kuwasikiliza pamoja na kuwasaidia, na uwahurumia Masikini.

Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq pamoja na Waumini wakiwa makini kusikiliza historia ya Jafar Ibn Abu Twalib.

Katika Vita Vya Mu’utah Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali. Alipigana kishujaa na kwa muda mrefu, akiwaua maadui wengi kiasi kwamba miili yao ilijipanga kama kamba ya kuni kumzunguka yeye.

Lakini baadae askari wa Kirumi alitambaa kutoka nyuma, bila ya kuonekana, na akampiga kwa upanga wake kwenye mkono wake wa kulia, na akaukata kabisa. 

Jafar hakuiachia bendera ianguke chini, na alizidi kumbana adui.
Baadae kidogo, Mrumi mwingine akaja kutokea nyuma, na kwa pigo la upanga wake, akaukata mkono wa kushoto pia. 

Shujaa huyu, akiwa bado hajakata tamaa, aliishikilia bendera chini ya kidevu chake, na akaendelea kusonga mbele.
.

Sunday, March 22, 2015

Hali ya mvua Dar es salaam ni tete.

Haya ni matokeo ya Mvua ambayo imefiksha siku ya tatu, na bado inaendelea,

Picha hizi ni za maeneo ya Barafu, Mburahati, Dar es salaam, kwa wakazi wanaoshi mabondeni.




Zitto aongea na Waandihi wa Habari, juu ya kung'atuka ubunge na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo

Mwanamuzi wa Muziki wa Kizazi kipya, Suleiman Msindi (Afande Sele) amejiunga pamoja na Mhe. Zitto Kabwe katika Chama cha ACT-Tanzania.

Mhe. Zitto Kabwe akiongea na Waandishi wa Habari leo hii asubuhi katika ukumbi wa Serena,Dar es salaam.

Mhe. Zitto Kabwe akiwa na baadhi ya Wanachama Wezake wa chama cha ACT-Tanzania, wakionesha kadi zao za Uanachama.Pembeni yake kulia ni Msanii Afande Sele.

Zitto Kabwe Ajiunga Rasmi Na Chama Cha ACT

Mhe.  Zitto Kabwe akivalishwa Skafu ya ACT mara baada ya 

kupokea rasmi kadi ya chama hicho.Tumeisimamia pamoja 

Serikali na ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge hili la kumi.. Na 

Mungu akipenda tutakuwa pamoja mwezi November… 

Kwaherini.. Asanteni sana– Zitto Kabwe.
Na hii ndio kadi rasmi ya Mhe. Zitto Kabwe aliyokabidhiwa na 

chama cha ACT

Mhe. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na Viongozi wa Chama cha ACT, mara baada ya kupokea kadi hiyo.
Mhe.Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya Uanachama wa ACT.
tukio hilo litafanyika katika ukumbi wa Serena Hotel saa tano 
kamili asubuhi.

ACT-Tanzania: kirefu chake ni :  Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.



Saturday, March 21, 2015

Sheikh.Abdi “Umuhimu wa usomaji Qur’an Nyumbani”

Naibu Mkuu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) akihutubu jana katika swalat Jumaa.
Naibu Imamu Sheikh Muhammed Abdi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kujibidisha na kujikurubisha katika Usomaji wa Qur’an.

Hayo aliyasema jana katika Hutuba ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam.

Sheikh.  Abdi alisema  umuhimu wa nyumba inayosomwa QUR'AN, Allah huifanya Nyumba hiyo kuwa pana na Nyepesi riziki yake pamoja , huiweka katika Ulinzi wake na chini ya Ngome yake.

Aliongeza kuwa allah (swt) huwakinga na Umasiki na Ufukara watu wake na Huwaepusha na Mabalaa na Kila aina Shari zinazosababishwa na majini pamoja na watu.

Waumini wa Dini ya Kiislam, dhehebu la Shia wakiwa msikikiti wakiomba dua baada ya kumaliza swala ya Ijumaa

Waumini wakiwa katika hali ya Utulivu mbele ya Mwenyezimngu (swt) wakijiandaa kufanya Nyurad (Tasbih) mbalimbali za baada ya swala ya Ijumaa