Wednesday, August 26, 2015

Mh. Makufuli akiwa Mbeya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI BLOG


Tuesday, August 25, 2015

Said Nkumba arudi CCM, Kutoka CHADEMA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo (kulia) akikumbatiana na Said Nkumba baada ya kurejea katika chama hicho siku chache baada ya kukihama na kujiunga na Chadema walipohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa CCM, uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuz
Aliyekuwa Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alihamia CHADEMA hivi karibuni ameamua kurejea katika chama chake cha zamani kwa madai alikosea njia.

Nkumba ambaye alihamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni kugombea ubunge Sikonge, aliteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA lakini wanachama wa chama hicho walipinga kitendo cha Kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani kumteua wakitaka mgombea wao, Hijja Ramadhan arudishwe jambo lililofanya Nkumba kuondolewa na kukosa nafasi ya kugombea ubunge. 

Nkumba alipojitoa CCM alisema alikipenda kwa dhati chama hicho lakini hakuona sababu ya kuendelea kubaki kwa kuwa hasikilizwi na hakina mapenzi na watu.

Lakini akizungumza Dar es Salaam jana, Nkumba alisema amerudi nyumbani kwa kuwa alipotea njia na hakuona kama kuna mwelekeo CHADEMA

Alipoulizwa kuhusu kupewa jimbo na CHADEMA alisema hayo yaachwe, amerudi nyumbani kwa kuwa ni kama rebound katika mchezo wa kikapu na watu wanaendelea kucheza.

Mh.Lowassa akiwa ndani ya daladala alilopanda Kituo cha Gongolamboto mwisho kuelekea Chanika

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.

PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI




Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu yaMabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.


Mafuriko Nyumbani kwa Mh.Pinda


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitiaChama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Chama hicho uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi  leo ambapo amehutubia mikutano ya hadhara mitatu katika mkoa huo  katika maeneo ya Mishamo, Katumba na Mpanda mjini.
Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili ashinde na  shughulika na matatizo ya wananchi  kwakuwa  anayaelewa matatizo na shida nyingi za watanzania, Dr. Magufuli ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara za Kasulu -Mpanda,  Sumbawanga – Mpanda , Mpanda -Tabora ili zikamilike kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia wananchi katika shughuli mbalimbali za kiuchumi mkoani humo PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KATAVI






Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akiwa ameketi meza kuu pamoja na Mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni eneo la Katumba mkoani Katavi kushoto ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Ndugu William Likuvi. PICHA NA HABARI24

Sunday, August 23, 2015

ACT-Wazalendo wavuna Wanachama 500 kutoka CHADEMA

Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.


Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Hata mara baada ya wanachama hawa kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA. chanzo EATV



Friday, August 21, 2015

Mh.Mbatia awaonya Viongozi wa UKAWA

Wakati Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA ukikumbwa na changamoto ya ugawanaji wa majimbo baada ya maeneo mengi nchini Tanzania kuibuka migogoro mara baada ya majimbo ya uchaguzi kugawanywa kwa vyama hivyo,hatimaye mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI ambaye ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo ameibuka na kutoa onyo kali kwa viongozi ambao wanakuwa wabinafsi wa kutokutaka kuachiana majimbo na kusema kuwa ubinafsi ni jambo ambalo halitaendekezwa ndani ya umoja huo.

Akizungumza na wanahabari leo jioni hii Dar es salaam amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa kazi ya kugawana majimbo kwa vyama vinne vinavyounda umoja huo kumeibuka sintofahamu ya baadhi ya watu kungangania majimbo ambayo tayari wamepewa watu wengine jambo ambalo amesema kuwa sio makubaliano ya umoja huo na hawatavumilia viongozi wa namna hiyo.

Amesema kuwa moja ya maazimio makubwa ya umoja huo ni kuepuka ubinafsi na kuhakikishya kuwa mambo wanayoyahubiri kwa wananchi wanayatekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na amani na umoja hivyo hawako tayari kuona chama au mtu yoyote anaanzisha vurugu ndani ya umoja huo.

Amesema Tayari leo jioni viongozi wakuu watakutana kuona ni jinsi gani wanaweza kushughulikia jambo hilo ili ndoto za watanzania za kuhakikisha kuwa wanauondoa mfumo dhalimu wa CCM uliopo kwa sasa zinatimia na nchi inakuwa na amani na utulivu mkubwa.