Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei |
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametahadharisha kuhusu njama za adui zenye lengo za kuudhihirisha Uislamu kuwa ni tishio.
Akizungumza hii leo katika Akademia ya Jeshi ya Imam Ali mjini Tehran, Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa wenye nia mbaya duniani na
wanaotumia mabavu wanataka kutumia sanaa, siasa, nguvu za kijeshi na njia
nyinginezo kuzuia sauti ya Uislamu isisikike na hilo linathibitishwa na woga
unaokua wa madola ya kibeberu.
Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa hii leo, madikteta wa kimataifa wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na nguvu za Uislamu na ndiyo maana wanatumia uwezo wao wote kueneza chuki dhidi ya dini hii tukufu duniani.
Kuhusiana na wanamgambo wa kundi la kitakfiri la Daesh wanaosababisha machafuko huko Iraq na Syria, Kiongozi Muadhamu amesema magaidi hao wamefanya uhalifu mkubwa katika nchi hizo, ikiwemo mauaji ya umati ya raia pamoja na wanajeshi na maafisa wa usalama.
No comments:
Post a Comment