Kiongozi wa Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa |
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kila mwanachama anapaswa
kuwaunga mkono wagombea watakaopitishwa na chama hicho katika nafasi mbalimbali
katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwani kinyume chake ni kukisaliti na adhabu yake ni
kufukuzwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira alisema mwishoni mwa
juma kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, chama hicho
kinahitaji nguvu za pamoja.
“Sisi bado hatujajiunga na Ukawa, hivyo wanachama wetu
wanapaswa kulitambua hilo na kuepuka kushiriki kwenye ushawishi wa kufanya
kampeni za wagombea wa vyama vingine.
Hata kwenye katiba yetu tunasema sasa
tunalenga zaidi katika kujiimarisha ili kutoa ushindani mzuri wa kisiasa katika
uchaguzi huu,” alisema.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa |
Katiba ya ACT, imeeleza wazi kuwa pamoja na sababu nyingine
na kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote
ambaye atasaidia kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama
kingine au mgombea wakati chama kimeweka mgombea wake kwa mujibu wa sheria za
nchi, atakuwa amepoteza uanachama wake.
ACT- Wazalendo tayari imetoa ilani yake ya uchaguzi
ikionyesha kwamba iwapo itaingia madarakani, itawajibika kwa wananchi kwa
kuweka kipaumbele katika maeneo manne ambayo ni hifadhi ya jamii, uchumi
shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, afya na elimu.
Kauli hiyo ya ACT linakuja huku kambi ya vyama kadhaa vya
upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ikiwa kwenye mchakato
wa kuunganisha nguvu ili kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana
majimbo katika baadhi ya maeneo.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amewahi kunukuliwa
akisema kuwa umoja huo unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD
umehamishia nguvu zake kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Mbatia alisema tayari umoja huo umeunda kamati maalumu
kutafuta namna ya kumsimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa |
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema
tayari kamati zimeundwa na zinaendelea na kazi ya kuratibu mpango huo mahsusi,
unaolenga kuiondoa CCM madarakani.
“Lengo letu ni kuhakikisha Ukawa ina nguvu ya kushika dola
katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na katika mpango huo, vyama vitaachiana majimbo na
viti vya udiwani kulingana na nguvu ya chama katika sehemu husika,” alisema.
Mkakati huo uliopangwa na Ukawa, unaelezwa na wachambuzi wa
masuala ya kisiasa kuwa ni kombora kwa CCM, kwani endapo utafanikiwa, utakiweka
chama hicho tawala katika wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu uliopangawa
kufanyika Oktoba mwaka huu.
Chanzo;Mwananchi.com
No comments:
Post a Comment