Uongozi wa Klabu ya soka ya Yanga unakanusha taarifa zilizotolewa na wachezaji kugomea mazoezi.
Kaimu katibu mkuu Deusdedit Baraka,anapenda
kuwaeleza wanachama,mashabiki na wapenzi wa Yanga kuwa hakuna mchezaji
aliegoma na wachezaji wote wanaendelea na mazoezi yao na hakuna mgogoro
wa malipo ya mishahara.
Aidha,Bw Baraka amefafanua kuwa utaratibu wa mfumo wa malipo ndio umebadilika na mishahara inaendelea kutolewa kama kawaida.
Imetolewa na Idara ya Habari na
Mawasiliano Yanga Makao Makuu
20-12-2016
No comments:
Post a Comment