WIZARA ya Katiba na Sheria imeanza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuhamia mjini Dodoma kabla ya Februari mwakani.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome awamu
ya kwanza ya watumishi wa wizara hiyo inategemea kuondoka jijini Dar es
Salaam Januari kwenda Dodoma.
“Kuhamia Dodoma haina mjadala, si sisi tu, ni wizara zote, awamu ya
kwanza watawasili Dodoma kabla ya Februari.
Watumishi wakaobaki
watakwenda katika awamu zitakazofuata ambazo mtajulishwa baadaye,"
amesema Profesa Mchome.
Katibu huyo, aliwataka watumishi wote wa wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma.
Awali, tangazo la wizara hiyo lilisambaa katika mitandao ya kijamii
kuhusu orodha ya watumishi wake wanaohamia Dodoma kuwa ipo tayari na
wataondoka Januari.
Profesa Mchome alisema mambo mengine ni ya ndani na asingependa
kuyazungumza wazi lakini alisisitiza kuwa, kikubwa kuhamia Dodoma ni
lazima na itafanyika kwa awamu hadi kukamilika mwaka 2018.Chanzo Habarileo
No comments:
Post a Comment