Monday, March 2, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s) Yahimiza Hijab kwa Bint wa Kiislam.

Waschana wenye umri kati ya Miaka 9 hadi 15 wakisoma Duatul Huja baada ya Kupewa mafunzo ya Dini Kiislam, kwa Mnasaba wa kuzaliwa Bibi Zayanab Bint Ali (a.s).

Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala akiwaswaisha kwa Vitendo waschana waliohudhuria katika kusherekea kuzaliwa kwa Bibi Zaynab Bint Ali.
Hawazat Imam Swadiq imesheherekea mazazi ya Bibi Zaynab Bint Ali (a.s)  kwa kuwachukua wasichana 50 wenye umri wa miaka kuanzia 9 hadi 15, pamoja na wazazi wao kwa kuwapatia elimu na mafunzo juu ya Unuhimu wa Hijabu, Swala na sheria zingine za Kiisalamu.

Katika Mafunzo hayo, Samahat Sheikh Hemed Jalala aliwasalisha swala ya jamaa kwa vitendo na kuwataka waschana hao waishi kwa misingi ya Kiislamu,na Wapambike na hijjab kama walivyokuwa Fatma Bint Muhammad (s.a.w.w) na Zaynab Bint Ali (a.s)

Bibi Zainabu Baba yake ni Sayyedina Ali  Ibn Abutwalib (a.s), Mama Yake ni Fatuma Bint Muhammad, Babu yake ni Muhammad Ibn Abdallah na Bibi yake ni Khadija Bint Khuwailid


Sheikh Hemed Jalala akiwapa neno la umuhimu wa Hijab na Ibada zingine kwa bint wa Kiislam.

Waschana wakiwa pamoja na wazazi wao wakiwa makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali

Waschana wa Kiislam wanatakiwa kupambika kwa kuvaa Stara,Ibada, Elimu na Tabia Njema kama alivyokuwa Bibi Zaynab Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Sunday, March 1, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s), yafanya Mhadhara wa Wazi

Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa makini katika kusikiliza Wahubiri wa Mhadhara siku ya kwanza.Mhadhara huo ukiwa na ujumbe wa "Uislam ni Dini ya Amani" uliofanyika katika Viwanja vya Round About ya Kigogo, Viwanja vya Super Sanif.



Waumini wa Kike wakiwa makini katika kuandika nukta muhim za Wahubiri wanavyosema.

Vijana mbalimbali wa dini ya kiislamu wakiwa katika ufatiliaji wa mada mbalimbali zinazowasilishwa na masheikh mbalimbali kutoka Hawzat Imam Swadiq (a.s)



Kulia ni Samahat Sheikh Hemed Jalala, pembeni yake ni Sheikh Muhammad Abdi wakiwa katika maandalizi ya kuwahubiria waumini wa Dini ya Kiislam.


Wednesday, January 21, 2015

Sheikh Jalala "Waislam na Wakristo ni Wamoja"



Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Kigogo Post Sheikh Hemed Jalala amesema Taifa la Tanzania linajulikana kama kisiwa cha amani na wakiristo na waislam wanaishi kama ndugu moja. 

Sheikh Hemed Jalala akiwa anaelezea jambo wakati wa kongamano hilo la Takfiri

Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Kigogo Post Sheikh Hemed Jalala amesema kongamano hili limewakusanya viongozi wa dini zote kwa upande wa wakristo hasa wale wenye waumini wengi na kujadiliana  juu ya amani ya nchi na taifa kwa ujumla.

Amesema
Viongozi wa Dini hawatofumbia macho kuona dalili zozote za uvunjifu wa amani kwani .
 
"Wakristo na Waislam ni kitu kimoja na tupo tayari kumpiga vita mdudu hatari atakaye kututenganisha kwani vita vitakapo tokea hasara haitakua ya Dini moja tu bali kwetu sote,"alisema Jalala

Hayo yamesemwa  jini Dar es Salaam na Sheikh Hemed Jalala wakati w a Kongamano la kidini likiwa na Ujumbe, Madhara ya Misimamo mikali ya imani za kidini (Takfiri) katika jamii na Taifa. Kongamano hilo likiwa limeandaliwa na Taasisi ya Imam Bukhary ambyo mwenyekiti wake ni Sheikh Khalfan Khamis.





Askofu wa Kanisa la Galiya Evangilist Asseblies Of God (EAGT) Msasani,Askofu Philbert Mbepera   

 Kwaupande wa askofu wa Kanisa la Galiya Evangilist Asseblies Of God (EAGT) Msasani,Askofu Philbert Mbepera amesema viongozi wa dini zote awapaswi kubezana kwa kile wanacho kiabudu.

Amesema imani ya nchi aiwezi kujengwa kwa chuki na uwasama bali ni kwa kufuata misingi ya vitabu vya Mungu ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na upendo na kuvumiliana kwa imani tofauti.

"Kwaupande wetu sisi tumefunga siku 40 kwa ajili ya kuombea amani ya nchi hasa kutokana na jukumu kubwa la kitaifa linaloikabili nchi yetu kwani viongozi wa kisiasa wanaushawishi mkubwa wa kusababisha upotevu wa amani kwa wale wanaotumia majukwaa ya dini kujinadi,"alisema Mbepera





Friday, January 16, 2015

"Kitendo cha Jarida La Charlie Hebdo kumdhalilisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kitendo cha Kifedhuli”.



Harakati ya hawza Imam Swadiq chini ya Uongozi wa Samahat Sheikh Hemedi Jalala inaungana na Waislamu wote duniani na Wapenzi wa Amani kokote walipo kupinga kwa Kauli thabiti hatua zozote zinazochukulia na Serikali za nchi za Magharibi na Marekani kuchochea vitendo venye lengo la kuamsha chuki na machafuko ya Kidini ulimwenguni.


Jalala alisema kitendo cha kumtusi Muhammad (s.a.w.w) ni Kashfa na Matusi ya wazi kwa Mtume wetu Kipenzi chetu Muhammad (s.a.w.w) Waislamu wote bali na wapenda Amani duniani kote. Ni kitendo kisichovumilika na hakuna Musialmu aweze kustahamili ghadhabu zake kwa kitendo hichi.

Kauli hivyo imetolewa baada tu ya Jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris nchini Ufaransa Charlie Hebdo lilisema katika toleo lake la hapo kesho siku ya Jumatano(14/01/2015) litachapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wa mbele, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote”.
Aidha alisema kuwa vitendo hivi vinafanywa na makundi ya Watu waovu, Wasio na Imani ya Dini wala Ubinaadamu, wanaopata kinga ya kulindwa na ufadhili wa Idara za Kijasusi za Mataifa na dola za Magharibi kwa lengo lao ovu la kutaka kuupaka Matope Uislamu na Waislamu duniani.
Samahat Sheikh.Hemed Jalala.




 “Kuheshimu Imani, Mila, Tamaduni na Matukufu ya Imani za Dini tofauti tofauti ni kanuni ya Msingi ya Umoja wa Kimataifa, tunawataka wakuu wa Dola za Magharibi na Amerika kuwa Vinara kuziheshimu na kutekeleza kwa vitendo kanuni na Haki hizi”alisisitiza Jalala. 

Alisema kuwa Maamuzi yasio ya Upendeleo wa kiimani na yenye Maslahi sawa kwa raia wa Imani tofauti tofauti wa Mataifa yao. Kwani ni kwa Maamuzi wanayoyafanya yenye upendeleo wa Makusudi kwa Upande mmoja wa Imani ya Dini na kukandamiza upande mwingine ndio chanzo cha kuzuka makundi yenye misimamo mikali na yenye mikakati ya kulipiza kisasi na kufanya vitendo vya Kigaidi. 

“Wanatumia gharama kubwa kukandamiza maandamano ya Amani yanayoitishwa katika nchi zao kulaani Vitendo viovu na vya kigaidi vinavyofanywa na Taifa ghasibu la Israel? Sambamba na hili tunaungana na Ulimwengu mzima kupinga Vitendo vyovyote vya kigaidi vinavyofanyika duniani kote dhidi ya Nchi na au binaadamu yeyote asiye na hatia”alisema Jalala.

Jalala aliongeza kuwa Hakuna uhuru usio na Mipaka, Matumizi mabaya ya Vyombo vya habari na Mawasiliano, Imani na Misimamo inayokiuka mipaka ya Dini na Sheria za Nchi, Mauaji na Udhalilishaji wa Viongozi wenye kuheshimiwa wa Dini na Nchi, Kukashifu na Kutakana Matukufu ya Dini na uvunjaji wa Alama za dini zinazoheshiwa na waumini wa Dini hizo, ni Vitendo Viovu.

Sunday, January 11, 2015

Grace Mugabe aziacha familia 200 bila ya makazi



Bi Grace Mugabe mke wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametumbukia katika sakata la ardhi baada ya kuzihamisha kwa nguvu familia zaidi ya 200 katika makazi yao bila ya kuzipatia makazi mbadala. 

Grace Mugabe aliwaamuru maafisa polisi waliokuwa wamejizatiti kwa silaha, kuziondowa kwa nguvu familia hizo katika eneo lao la mashamba ya Anold wilayani Mazowe mashariki mwa Harare mji mkuu wa Zimbabwe bila ya kuwapatia sehemu nyingine ya kuishi katika kipindi hiki ambapo mvua nyingi zinaonyesha.

Mkulima mmoja ambaye hakutaka kujulikana alisema kuwa baada ya polisi kufikia katika mashamba yao, waliharibu nyumba zao na kusema kuwa wanaondolewa hapo ili kutoa fursa kwa Grace Mugabe ya kujenga bustani ya michezo. 

Baadhi ya familia hizo zimenukuliwa zikilalamika kwamba, wameamriwa kuondoka katika makazi yao hayo hata hivyo bila ya serikali kuwapatia eneo jingine la kuishi. 

Wakati huo huo Taasisi ya Mawakili wa Haki za Binadamu ya Zimbabwe imetuma timu ya wanasheria huko Mazowe ili kusitisha zoezi la kuzifukuza familia zilizokuwa zikiishi hapo.