Monday, August 3, 2015

Mauzauza kura za Maoni

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa kura za Moniwa Kata ya Kisukulu B,Christopher Masinde akionyesha kadi ya mpigakura halali kwa wajumbe wa mkutano huo jana wakati wa kuhakiki majina kabla ya kupiga kura kuchagua wagombea udiwani na ubunge kwenye jimbo la Segerea ,Dar es Salaam .Picha|SALIM SHAO 
Mauzauza jana yalitawala mchakato wa kura za maoni kwa ajili ya kupata wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM kutokana na kuwapo kwa vitendo vya rushwa, vurugu, kura kuchomwa moto, makada kukamatwa, wanachama kutoruhusiwa kupiga kura na kugundulika kwa karatsi zilizokwishapigwa kura.
Kwenye baadhi ya maeneo kazi hiyo iliahirishwa hadi leo kutokana na vifaa kuchelewa na pia tatizo la kugundulika kwa shahada ambazo zimeshapigwa kura zikiwa ndani ya maboksi.
Lakini matukio yaliyotawala kura za maoni ni makada kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kugawa fedha au kuchapisha karatasi bandia za kupigia kura. Chanzo-Mwananchi.

RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI AUSTRALIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka  Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida  alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove. 
PICHA NA IKULU
……………………
Akiwa nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.
Rais Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia  namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.
Rais Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

Thursday, July 30, 2015

Umeskia Alichosema LISSU

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.

Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.

Sunday, July 26, 2015

Mwanamuziki 'Bongo Fleva' Khadija Shabani 'Keisha' ashinda CCM

MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya 'Keisha' ameibuka mshindi kwenye kura za maoni za Ubunge wa viti maalum kundi la Walemavu MKoa wa Dodoma na kuwa mshindi wa kwanza.
Keisha amepata kura 340 huku Stella Fueda akiibuka na kura 112, Anna Fungo kura 100 na Graceana Kavishe kura 54.

Jumla ya kura 721 zilipigwa ambapo kura 75 ziliharibika na kura za halali zilikuwa 646.

Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari na kubainisha kuwa japo ni mlemavu wa ngozi lakini anajikubali anajipenda kujiamini na amekuwa akipigania amani ambayo wanastahili kuipata kutoka nchini.

Alisema alipoanza kuweka picha zake za siasa kwenye mtandao kuna baadhi ya watu walimpongeza na wapo waliosema kuwa hana uchungu na wenzake kwani waliamini anaingia kwenye siasa kwa nia ya kujinufaisha “Wapo wanaohisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi
ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu” alisema.

Alisema fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa akimaanisha kuwa lazuima kusimamia sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima kuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.
  • Taarifa ya Sifa Lubasi, Dodom 
  • Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu mashabiki zangu na media zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia kitu.

    Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.

    Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.

    this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza kuchangia humo na kwa upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo ahsanteni shukrani.

Saturday, July 25, 2015

Kenyatta Amgomea Obama Kuhusu Ushoga

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametofautina mtazamo kuhusu ushoga na ndoa za jinsia moja na mgeni wake ambaye ni Rais wa Marekani, Barack Obama mbele ya waandishi wa habari. 

Akiongea mbele ya idadi kubwa ya waandishi wa habari katika eneo la Ikulu ya Kenya, Rais Obama alipinga kwa nguvu ubaguzi dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini Uhuru Kenyatta alikuwa ngangari na kumueleza kuwa utamaduni huo hauna nafasi nchini Kenya. 

Rais Kenyatta alifafanua kuwa suala la ushoga sio suala muhimu nchini humo na kwamba nchi hiyo inahitaji kujikita katika maeneo mengine ambayo ndiyo maisha ya kila siku ya wananchi. 

Obama aliingia nchini Kenya Julai 24 usiku na kupata mapokezi ya kihistoria katika nchi hiyo inayomchukulia kama mtoto wa nyumbani aliyerudi na taji la ukuu wa nchi kubwa yenye nguvu zaidi duniani.

Waislamu Marekani waandamama kuipinga Saudia

Waislamu wanaoishi Marekani wameandama mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington wakilalamikia jinai za nch hiyo na hatua ya nchi hiyo ya kuunga mkono ugaidi. 
Shirika la habari la Tasnim limeripoti kutoka Washington kuwa, maelfu ya Waislamu wanaoishi katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa Marekani jana walikusanyika kwenye maidani ya Watergate mjini Washington na kisha kuandamana hadi mbele ya ubalozi wa Saudia na kupiga shaari dhidi ya serikali ya Riyadh. 
Wafanya maandamano hao walikuwa wakipiga nara na shaari kama 
"utawala wa Aal Saud si tu si mwakilishi  wa Uislamu, bali ni muungaji mkono wa kundi la kigaidi la Daesh, machafuko na misimamo ya kufurutu ada.” Katika maandamano hayo, Hujattul Islam wal Muslimin Sheikh Abduljalil Imam wa msikiti wa Jaafariya huko Maryland Marekani ametoa hotuba na kulaani jinai za Saudi Arabia. 
Sheikh Abduljalil ameendelea kuhutubia kwa kusema wamekusanyika ili kuwaambia walimwengu kwamba iwapo wanatafuta chanzo cha magaidi basi wanapasa kukipata ndani ya utawala wa Aal Saud. 
 Amesema chimbuko la ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, huko Iraq na Syria ni utawala huo wa Aal Saud.
Chanzo Irib.

Angalia Obama alivyowasili Kenya

Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na dada yake Auma Obama huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwaangalia.

Mtoto Joan Wamaitha, 8, ndiye Mkenya wa kwanza kumkaribisha Rais Barrack Obama nchini humo kwa kumpa shada la maua na kupiganae picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya kwenda kulakiwa na mwenyejiwake Rais Uhuru Kenyatta.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Obama aliwasili nandege yake ya Air Force One.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.

Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.

Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.

Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.

Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiria mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.

Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi.

Siku yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani.

Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia. Source:BBC Swahili & AFP