MBUNGE
wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata
wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na
chama hicho.
Lissu
ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa
Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio
wa Lowassa ndani ya Chadema.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa
Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi
kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Mfumo
tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu
ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.
Tunamkaribisha
kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu
tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia
Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.
Akizungumza
kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga
na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka
Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa
bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”
“Alijiuzuru
uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya
mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais
“tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo
tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga
nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.
No comments:
Post a Comment