Saturday, April 9, 2016

Waislam Hongereni kwa Kuzaliwa Imam Baqir (a.s) Khalifa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Jina : Muhammad
Kuniya : Abu Ja’afar
Lakabu yake : Al-Baqir
Baba yake : Ali Ibn Hussein
Mama yake : Fatimah Bint Hassan
Kuzaliwa kwake : 1 Rajab, Mwaka wa 57, Madina
Nasaba ya Imam Muhammad Ibn Ali (a.s) ni ya kipekee sana, kwa sababu yeye ndie Imam pekee amabe ameunganishwa  na Fatima Zahra(a.s) Bint Muhammad (s.a.w.w) kupitia kwa Baba na Vile vile kwa Mama, Baba yake ni Mtoto wa Imam Hussein Ibn Ali (a.s) na Mama yake ni Mtoto wa Imam Hassan Ibn Ali (a.s). Kwa sababu hiyo alikuwa akijulikana mtoto wa Wema wawili pia akijulikana “Al-Baqir” mchunga (wa Elimu ya Mtume).

Mwaka wa 57 baada ya hijra ya Mtume (s.a.w.w) kuelekea Madina, katika siku ya kwanza ya mwezi uliojaa fadhila wa Rajab, ulimwengu ulipambazuka kwa kuzaliwa nuru. Katika siku hii yenye baraka, mtoto kutoka Nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizaliwa na kama walivyokuwa Ahlul Bayt wengine wa Mtume (s.a.w.w), akawa tawi katika matawi maridadi katika historia ya Uislamu.

Uimamu wa Imam Mohammad Baqir (a.s) ulianza katika kipindi ambacho, ummah wa Kiislamu ulikuwa unakabiliwa na changamoto kubwa za kiitikadi na kifiqhi baina ya makundi mbali mbali ya Kiislamu. Kuwepo Imam Baqir (a.s) katika medani kulipelekea kuchukuliwa hatua muafaka katika kubainisha mitazamo ya Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w.w).

Katika kipindi cha Imam Baqir (a.s), hujuma ya kiutamaduni iliyokuwa imeratibiwa kwa mpangilio maalumu na Bani Umayyah ililenga kuvuruga itikadi za kidini za ummah wa Kiislamu. Aidha katika kipindi hicho, jamii ya Kiislamu ilishuhudia kuibuka nadharia zisizo sahihi za kifalsafa kuhusu misingi ya itikadi.
Licha ya shughuli nyingi za kielimu na kiutamaduni alizokuwa nazo, Imam Baqir (a.s), hakughafilika na masuala ya kisiasa na alikuwa akiwakosoa sana watawala wa kiimla na madhalimu wa zama zake. Katika harakati zake za kuwazindua Waislamu kisiasa, Imam alibainisha sifa za viongozi wema ili kuwafanya watu waweze kuwatia kwenye mizani watawala na kufahamu udhaifu na upotofu wao.
Sheikh Tousi, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu amewataja wanafunzi bingwa wa Imam Baqir (a.s) kuwa ni watu 462. Vigogo na shakhsia wakubwa wa kielimu wa zama hizo wote walifika mbele ya Imam Baqir (a.s) ili kupata angalau tone moja la bahari yake pana ya elimu. Watu kama vile Jabir bin Yazid Ju'fi, Zuhri , Abu Hanifa, Anas bin Malik na Shafi ni kati ya wanazuoni walionufaika na hazina kubwa ya kielimu ya Imam Baqir AS. Muhammad Ibn Talha Shafi'i katika kuelezea sifa za Imam Baqir anaandika: “Alikuwa mwenye kuchana na kunawirisha elimu.
Imam Baqir anasema: “Uongozi wa jamii unamustahiki mtu mwenye sifa tatu. Kwanza ni ucha Mungu ili takwa iweze kumkinga na mitihani na madhara ya madaraka kama vile kutumbukia katika mtego wa ufisadi. Pili awe mstahimilifu ili aweza kuzuia hasira zake. Tatu aamiliane na watu anaowatawala kama baba mkarimu na awe na tabia nzuri”.
Imam anasema katika sehemu nyingine: "Hakuna mja yoyote muumini asiye na nukta nyeupe na yenye nuru kwenye moyo wake. Kila mara anapofanya dhambi nukta nyeusi hudhihiri kwenye nukta hiyo nyeupe. Kwa hivyo iwapo atatubu baada ya kufanya dhambi nukta hiyo nyeusi hutoweka, la sivyo akidumu kwenye maasi nukta nyusi huongezeka na kuenea hadi kufunika kabisa nukta hiyo nyeupe. Baada ya kufunikwa kabisa nukta hiyo nyeupe mtu aliye na moyo kama huo kamwe hatawezi kuona uso wa saada."
Wapenzi wasomaji kwa mara nyingine ninatoa mkono wa pongezi, kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Baqir (a.s), Imam wa Tano katika Maimam aliowataja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa Makhalifa baada yake, wakwanza akiwa ni Imam Ali Ibn Abu Taalib (a.s), Wapili ni Imam Hassan Ibn Ali (a.s), watatu ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s), wa nne ni Imam Ali Ibn Husein -Sajjad (a.s) na Wa tano ni Imam Muhammad Ibn Ali al Baqir (a.s).
Imetolewa na
Twalha Zuberi Ndiholeye
Kiongozi Mkuu wa Baqir Media
Tarehe 09/04/2016, Sawa na 2, Rajab, 1437

Monday, April 4, 2016

Watoto wenye Usonji wanamahitaji kama watoto wa Kawaida Tusiwatenge

Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kutoa elimu bora na Bure kwa watoto wote wa kitanzania bila kubagua rangi,kabila wala dini huku mkazo mkubwa sasa ukielekezwa pia kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanapata elimu sawa.

"Aidha niwatake  wazazi, walezi na jamii bila ya kujali tofauti za kimaumbile kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya elimu, pia jamii inapaswa kuwachukulia watu wenye mahitaji maalumu kama ni sehemu muhimu ya jamii na wanasshirikishwa kikamilifu katika nyanja zote za Maendeleo" amesema Dr. Manyanya

Kauli hiyo hizo zimetolewa na Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dr. Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaamMaandamano hayo yameratibiwa na shule ya Al Muntazar na kushirikisha matabibu, waalimu wanafunzi, Changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo miongoni mwa jamii kuhusu ulemavu huo.

Huku wengine wakiuchanganya ulemevu huo na mtindio wa ubongo, wengine wanauhusisha na imani za kishirikina,jambo ambalo limesababisha ugumu katika matunzo ya watoto wenye Usonji" anasema Dr Stella Rwezaura, rais wa chama cha watu wenye Usonji Tanzania.

Usonji ni upungufu wa kibaiologia anaopata mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake na dalili zake huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea ambapo.

Maadhimisho ya watu wenye usonji huazimishwa kila tarehe 2, ya mwezi april ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE.Picha zaidi Bofya chini.
 
Hatahivyo Dr. Manyanya amesema kuwa Serikali kwa ikishirikiana na sekta binafsi na wadau wa elimu imekuwa ikipanua fursa za upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuandaa walimu, kuboresha miundombinu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika elimu.

"Napenda kuipongeza Taasisi yenu ya Almuntazir kwani imekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia watoto wenye usonji na wenye mahitaji mengine maalumu kwa kuwapatia elimu na huduma nyingine za Kijamii" amesema Dr. Manyanya

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam



Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam

Sunday, March 20, 2016

Iran na Uturuki zasisitiza ushirikiano wa pande mbili

Iran na Uturuki zasisitiza ushirikiano wa pande mbiliMawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Istanbul na kujadili masuala ya uhusiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa.

Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko nchini Uturuki kwa ziara rasmi amefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake, Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki. 

Dakta Zarif amesema, misimamo ya Iran na Uturuki kuhusiana na matukio ya Mashariki ya Kati inakaribiana sana na kwambva, Tehran na Ankara zinasisitiza juu ya kulindwa umoja wa ardhi ya Syria.
Waziri Zarif amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga baadhi ya njama za kutaka kuigawa ardhi ya Syria na kuongeza kuwa, siasa za Tehran zimesimama juu ya msingi wa kuheshimu umoja na mamlaka ya nchi zingine.
Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililotokea leo katika mji wa Istanbul na kubainisha kwamba, shambulio hilo lililo dhidi ya ubinadamu limezidi kuonesha sura mbaya ya ugaidi.
Kwa upande wake Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki sambamba na kuashiria kwamba, Uturuki ina wakimbizi zaidi ya milioni tatu kutoka Syria amesema kuwa, Tehran na Ankara zitafanya hima ya kuhakikisha umoja wa ardhi ya Syria unahifadhiwa.Chanzo irib

Hawzat Imam Swadiq-Yafanya Kumbukumbu ya Kifo cha Jafar Ibn Abu Talib (r.a)

kwa sura na mwenendo. Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimwambia:Jafar ibn Abu Talib “Umefanana na mimi kwa tabia na maumbile”.
Yeye ni Ja'far ni mtoto wa tatu wa Abu Talib bin Abdul Muttalib na Fatima binti Asad, hivyo ni binamu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ndugu zake wakubwa walikuwa Talib na Aqil; ndugu zake wa kiume walikuwa Ali na Tulay  na dada zake walikuwa Fakhita, Jumana na Raita.
Wakati kulikuwa na ukame hapo Makka, Abu Talib hakuweza kumudu kusaidia familia yake. Kwa hiyo ndugu yake Abbas alichukua malipo ya vijana Ja'far. Ja'far alikuwa mfuasi wa awali wa Uislamu. Mke wake ni   Asma bint Umays.
Wakati habari kufikiwa Muhammad, alilia na kuomba kwa ajili ya nafsi Ja'far Yeye baadaye  malaika Gabriel alishuka kuwafariji , akisema: ". Jafar alikuwa jasiri na waaminifu askari. Mungu amempa uzima wa milele, na badala ya mikono yake ambayo kukatiwa katika vita, Bwana amempa jozi ya mabawa (Atwayyar)

Jaafar akainyakuwa bendera kwa mkono wake wa pili na makafiri wakamzonga sana na walipofanikiwa kumkata mkono wake wa pili, Jaafar akaikumbatia bendera kwa mabega yake huku akiwa amesimama na na makafiri wakawa wanaendelea kumpiga kwa panga zao mpaka alipokufa shahidi.

Anasema Abdillahi bin Omar (Radhiya Llahu anhuma):
“Nilikuwa pamoja na Jaafar katika vita vya Mu-utah, na baada ya kumalizika vita hivyo tulimuona akiwa na majeraha ya panga na mikuki zaidi ya tisini, yote yakiwa sehemu ya mbele ya mwili wake”.
Kadhalika mapokezi ya kauli ya Mtume (s.a.w.) na kukiri kwake juu ya kufaa kulia kwa ajili ya wafu ni mengi. Mojawapo ni siku alipopata Shahada Bwana Jaafar bin Abi Talib (At-Tayyaar), Mtume (s.a.w.w) alikwenda kwa mkewe (Jaafar) Bibi Asmaa bint Umais ili kumpa faraja, naye Bibi Fatma aliingia pahala hapo huku analia na kusema:
"Ewe Ami yangu". Basi Mtume (s.a.w.) akasema:
"Na walie wenye kulia kuwalilia mashujaa mfano wa Jaafar."





Uongozi wa Baqir Media-Watoa Pole kwa Waislam wote kwa Kifo cha Jafar Ibn Abu Talib (r.a)

Jaafar bin Abu Talib (r.a), yeye alifanana naye Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa sura na mwenendo. Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimwambia:Jafar ibn Abu Talib “Umefanana na mimi kwa tabia na maumbile”.
Yeye ni Ja'far ni mtoto wa tatu wa Abu Talib bin Abdul Muttalib na Fatima binti Asad, hivyo ni binamu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ndugu zake wakubwa walikuwa Talib na Aqil; ndugu zake wa kiume walikuwa Ali na Tulay  na dada zake walikuwa Fakhita, Jumana na Raita.
Wakati kulikuwa na ukame hapo Makka, Abu Talib hakuweza kumudu kusaidia familia yake. Kwa hiyo ndugu yake Abbas alichukua malipo ya vijana Ja'far. Ja'far alikuwa mfuasi wa awali wa Uislamu. Mke wake ni   Asma bint Umays.
Wakati habari kufikiwa Muhammad, alilia na kuomba kwa ajili ya nafsi Ja'far Yeye baadaye  malaika Gabriel alishuka kuwafariji , akisema: ". Jafar alikuwa jasiri na waaminifu askari. Mungu amempa uzima wa milele, na badala ya mikono yake ambayo kukatiwa katika vita, Bwana amempa jozi ya mabawa (Atwayyar)
Hijra ya mwanzo
Idadi ya Waislamu ilipoanza kuongezeka, na Makureshi walipoanza kuwatesa Waislam na kuwafanyia kila aina ya vitimbi pamoja na kuwazuwia wasifanye ibada zao ili wawarudishe katika dini yao ya kua

“Itakuwa bora kama baadhi yenu mtaondoka na kuhamia nchi ya Uhabeshi, maana huko yuko mfalme ambaye hakubali mtu kudhulumiwa ndani ya nchi yake, na ni nchi ya ukweli. Kwa hivyo hamieni huko mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapoleta faraja Yake."

Wakaondoka Makka watu wapatao kumi wakiwemo Jaafar na mkewe na Othman bin Affan na mkewe pamoja na Waislamu wengine na kuanza safari ndefu ya kuhamia nchi ya Uhabeshi katika Hijra ya mwanzo. Kisha idadi yao ikaongezeka na kufikia watu themanini na tatu, na walipowasili huko walipokelewa vizuri na An Najashi  mfalme wa Uhabeshi.
Katika Vita vya Mu’uta majeshi mawili hayo moja likiwa na wapiganaji elfu tatu na lingine likiwa na watu zaidi ya mia moja elfu, yakaanza mapambano makali sana na hatimaye Zayd (r.a) akauliwa na kuanguka juu ya farasi wake.Wakafanya kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alivyousia, Jaafar (r.a) akainyakuwa bendera kabla ya kuanguka chini na akawa yeye ndiye anayeongoza mapigano hayo.

Vita vikali vikaendela, na Warumi walipoona majeshi ya Kiislamu yaliyokuwa na idadi ndogo ya watu kuliko wao yakipigana kwa ujasiri mkubwa, mkuu wa majeshi yao akatoa amri kuwa mshika bendera lazima auliwe.

Warumi wakaanza kuzielekeza nguvu zao zote kwa mshika bendera aliyekuwa Jaafar bin Abu Talib, huku wakirusha mikuki na mishale kwa nguvu moja na kuwaelekeza wapiganaji wao wakubwa wote upande wake, mpaka walipofanikiwa kumjeruhi na kumuangusha kutoka juu ya farasi wake huku akiwa ameishika bendera kwa mkono wake mmoja na huku akipigana kwa mkono wa pili.

Jaafar alimkata miguu farasi wake kwa kuogopa asije akachukuliwa na Warumi na kumtumia katika kuwashambulia Waislamu.Jaafar akawa anapigana akiwa anakwenda kwa miguu yake bila ya farasi na kusonga mbele huku akiwakata makafiri vichwa vyao huku na kule na huku akisoma mashairi ya kuisifia Pepo. Akawa anapigana nao mfano wa jeshi la mtu mmoja mpaka alipokatwa mkono wake uliokuwa umebeba bendera.

Jaafar akainyakuwa bendera kwa mkono wake wa pili na makafiri wakamzonga sana na walipofanikiwa kumkata mkono wake wa pili, Jaafar akaikumbatia bendera kwa mabega yake huku akiwa amesimama na na makafiri wakawa wanaendelea kumpiga kwa panga zao mpaka alipokufa shahidi.

Anasema Abdillahi bin Omar (Radhiya Llahu anhuma):
“Nilikuwa pamoja na Jaafar katika vita vya Mu-utah, na baada ya kumalizika vita hivyo tulimuona akiwa na majeraha ya panga na mikuki zaidi ya tisini, yote yakiwa sehemu ya mbele ya mwili wake”.
Kadhalika mapokezi ya kauli ya Mtume (s.a.w.) na kukiri kwake juu ya kufaa kulia kwa ajili ya wafu ni mengi. Mojawapo ni siku alipopata Shahada Bwana Jaafar bin Abi Talib (At-Tayyaar), Mtume (s.a.w.w) alikwenda kwa mkewe (Jaafar) Bibi Asmaa bint Umais ili kumpa faraja, naye Bibi Fatma aliingia pahala hapo huku analia na kusema:
"Ewe Ami yangu". Basi Mtume (s.a.w.) akasema:
"Na walie wenye kulia kuwalilia mashujaa mfano wa Jaafar."

Imeandaliwa na
Twalha Zuberi Ndiholeye,
Kiongozi Mkuu wa Baqir Media.
Tarehe 19/03/2016, Sawa na 10, Jamadal Akhir 1437.