Friday, April 22, 2016

Utawala wa Dr. Magufuli kwa mbali unafanana na Utawala wa Imam Ali – Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq Sheikh Hemed Jalala amesema hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli zinafanana kwa mbali na Utawala wa Imam Ali (a.s) ambaye mara nyingi alikuwa anachukizwa na watu kutowajibika katika majukumu yao na waliokuwa tayari kuwatumikia watu badala ya matumbo yao.


Sheikh Jalala ambaye pia ni Kiongozi mkuu wa Waislamu dhehebu la shia Ithnasheria amesema hayo leo ,Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, wakati akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali (a.s) na kusema kuwa kama linakuja suala la kufafanisha uongozi basi kwa mbali utawala wa Magufuli unaonekana kufuata nyayo za Utawala wa Imam Ali (a.s). 

“Utawala wa Imam Ali (a.s) ni utawala uliogubikwa na Utawala bora ambao ambao ulikuwa unapinga watu au mtu kujilimbikizia pesa, kufanya ufisadi, kutomtanguliza mungu kwa kila jambo, kufuja mali za umma na kuhakikisha watu wote wanakuwa na hali sawa” amesema sheikh Jalala.

"Imam Ali alizaliwa tarehe 13 Rajab mwaka wa 30 wa 'amul-fil' katika Alkaaba takatifu,mjini Makka, Mama yake ni Fatmah bint Asad, Baba yake ni Abu Taalib Ibn Abdul-Muttalib, Kuniya ni Abul-Hassan na Abu -Turab, yeye ndie Khalifa na Imam wa kwanza baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)"

Amesema Ukimsoma Imam Ali utagundua kuwa katika utawala wake hakupenda wananchi wa hali ya chini kunyanyasika, na pia alitilia mkazo wa watu wake kutafuta elimu popote pale na kwa hali yoyote


“Jambo hilo pia limeonyesha kwa vitendo na Rais wa awamu ya Tano Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli hususani pale alipotangaza kuwa Elimu bure hadi kidato cha nne. Ambapo imepelekea watanzania wa hali ya chini kupeleka watotowao Shuleni” amesema sheikh Jalala

Aidha Shekhe Jalala ametaja  baadhi ya mambo muhimu ambayo unaweza kuyapata katika utawala wa Imam Ali (a.s) ni jinsi ambayo Imam Ali (a.s) alikuwa akiongoza umma wa watu huku akimtanguliza Mungu.

“Utawala wa Imam Ali ulitawaliwa na hofu ya Mungu jambo ambalo lilisaidia kupunguza vitendo vya ufisadi, vitendo vya kuminya haki za binadamu na watu wengi kuwa na moyo wa kuwajibika” ameongoza Sheikh Jalala

Hatahivyo Shekh Jalal amemaliza kuongea na Waandishi wa Habari kwa kwa kuwataka watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini kuhakikisha wamuombee sana Rais wa Tanzania ili aweza kufanikisha lengo lake la kuifikisha Tanzania katika mafanikio ya kimaendeleo.

“Ndugu zangu nataka nitumie fursa hii kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli, bila shaka kwa kasi anayoenda nayo taifa litapiga hatua kubwa na kufanya wananchi wa hali ya chini kunufaika na rasilimali zilizopo” amesema sheikh Jalala.

Monday, April 11, 2016

Pole Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Waislam Wote kwa Kifo cha Khalifa wa Mtume, Ali Naqi (a.s)


Kiongozi Mkuu wa Baqir Media Mr.Twalha Zuberi Ndiholeye akionyesha Huzuni katika Maadhimisho ya Kifo cha Imam Ali Ibn Muhammad al-Naq (a.s), Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam

Jina : Ali Ibn Muhammad
Kuniya : Abul Hassan ath-Thalith
Lakabu yake : An-Naqi, al-Hadi
Baba yake : Muhammad  Ibn Ali at-Taqi
Mama yake : Samana.
Kufa kwake : 3, Rajab, Mwaka 254 B.H, Samarra, Iraq.

Imam Ali bin Muhammad (a.s.) ni Imam wa kumi kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Kama Maimam tisa wateule wa Mungu waliotangulia kutoka katika kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imam Ali bin Muhammad (a.s.) alikuwa ‘Masoom.’ (asiyefanya dhambi wala kukosea).

Alikuwa ni mwakilishi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wa Allah katika ulimwengu huu. Kwa wafuasi wake anajulikana zaidi kwa majina yake ya lakabu (majina ya sifa), Naqi (twahiru) na Hadi (mwongozaji) kuliko jina lake halisi. Majina yake mengine ya sifa ni pamoja na Nuseh (mshauri), Ameen (mwaminifu), Faqueeh (mwanasheria), Tayyib (mtakatifu) and Murthadha (mwenye kuridhiwa).

Kama walivyokuwa Maimamu wengine wateule wa Mungu kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imam Naqi (a.s.) alikuwa hodari na mjuzi wa akili na hekima ya kipekee, ambayo huakisi kutoka kwenye mwenendo wake kwa kipindi chake kifupi cha maisha.

Kusema kweli, Imam (a.s.) mwenyewe ananukuliwa akisema kwamba Maimam wote wateule wa Mungu (pamoja na yeye) wamebarikiwa ilmu ya kipekee waliyojaaliwa kwao na Mwenyezi Mungu; ilmu hii iko katika sehemu 73 ambazo kwazo sehemu 72 wamepewa Maimam 12 na Allah (s) anamiliki sehemu
zote 73.

“Ulimwengu huu ni soko: baadhi wanavuna faida, wengine
wanapata hasara.” Amesema Imam Ali Naqi

“Yule ambaye ana hofu ya Allah, watu humuogopa, na yule anaye
mtii Allah, watu humtii.” Amesema Imam Ali Naqi

“Husda hutafuna matendo mema na kuleta adhabu (kwa hasidi).” Amesema Imam Ali Naqi

“Kuwachukiza wazazi, hupunguza riziki na kuleta udhalilishaji.” Amesema Imam Ali Naqi

“Hasira ni ufunguo wa shida, lakini chuki ni mbaya zaidi kuliko
hasira.” Amesema Imam Ali Naqi


Kipindi cha uimamu wa Imam Ali Naqi (a.s.) ilikuwa ni “njia panda”muhimu ya kihistoria; kipindi hiki kimekuwa ni mwanzo wa kukoma kwa utawala wa Banu Abbas ambao ulianzishwa na Mansoor na kuletwa kileleni na Mamoon, na hatimaye kukoma katika mwaka wa 656 A.H. kwa kuuliwa Khalifa wa mwisho wa Banu Abbas.

Imam Ali Naqi (a.s.) aliishi maisha mafupi ya miaka 42 tu, nusu ya maisha haya akiwa ameyamalizia gerezani kwa aina moja au nyingine, na pia akiwa nchi ya ugenini. Licha ya vikwazo hivyi, Imam (a.s.) alihudumu katika njia ya Allah kwa uzuri sana na akaunganisha maisha ya watu wengi wa hali zote za maisha.

Kwa hiyo alipendwa na kuheshimia na watu wakati alipokuwa hai nakukumbukwa na wengi baada ya kufariki kwake. Ili kuielezea nukta hiitutaleta rejea kwa ufupi ya mtazamo kutoka kwa wanachuoni mashuhuri wachache wa Sunni juu ya mwenendo na mafanikio ya Imam (a.s.).

Ninarudia kutoa Pole kwa Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kwa Imam Mahd (a.s) pamoja na Waislam wote kwa Kifo cha Mjukuu wa Mtume ambae ni Khalifa na Imam Ali Ibn Muhammad al – Naqi (a.s).

Wapenzi wasomaji kwa mara nyingine ninatoa mkono wa pole na Simanzi kubwa  kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Baqir (a.s), Imam wa Tano katika Maimam aliowataja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa Makhalifa baada yake, wakwanza akiwa ni Imam Ali Ibn Abu Taalib (a.s), Wapili ni Imam Hassan Ibn Ali (a.s), watatu ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s), wa nne ni Imam Ali Ibn Husein -Sajjad (a.s) na Wa tano ni Imam Muhammad Ibn Ali al Baqir (a.s).

Imetolewa na
Twalha Zuberi Ndiholeye
Kiongozi Mkuu wa Baqir Media
Tarehe 10/04/2015, sawa na 3, Rajab 1437

Saturday, April 9, 2016

Waislam Hongereni kwa Kuzaliwa Imam Baqir (a.s) Khalifa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Jina : Muhammad
Kuniya : Abu Ja’afar
Lakabu yake : Al-Baqir
Baba yake : Ali Ibn Hussein
Mama yake : Fatimah Bint Hassan
Kuzaliwa kwake : 1 Rajab, Mwaka wa 57, Madina
Nasaba ya Imam Muhammad Ibn Ali (a.s) ni ya kipekee sana, kwa sababu yeye ndie Imam pekee amabe ameunganishwa  na Fatima Zahra(a.s) Bint Muhammad (s.a.w.w) kupitia kwa Baba na Vile vile kwa Mama, Baba yake ni Mtoto wa Imam Hussein Ibn Ali (a.s) na Mama yake ni Mtoto wa Imam Hassan Ibn Ali (a.s). Kwa sababu hiyo alikuwa akijulikana mtoto wa Wema wawili pia akijulikana “Al-Baqir” mchunga (wa Elimu ya Mtume).

Mwaka wa 57 baada ya hijra ya Mtume (s.a.w.w) kuelekea Madina, katika siku ya kwanza ya mwezi uliojaa fadhila wa Rajab, ulimwengu ulipambazuka kwa kuzaliwa nuru. Katika siku hii yenye baraka, mtoto kutoka Nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizaliwa na kama walivyokuwa Ahlul Bayt wengine wa Mtume (s.a.w.w), akawa tawi katika matawi maridadi katika historia ya Uislamu.

Uimamu wa Imam Mohammad Baqir (a.s) ulianza katika kipindi ambacho, ummah wa Kiislamu ulikuwa unakabiliwa na changamoto kubwa za kiitikadi na kifiqhi baina ya makundi mbali mbali ya Kiislamu. Kuwepo Imam Baqir (a.s) katika medani kulipelekea kuchukuliwa hatua muafaka katika kubainisha mitazamo ya Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w.w).

Katika kipindi cha Imam Baqir (a.s), hujuma ya kiutamaduni iliyokuwa imeratibiwa kwa mpangilio maalumu na Bani Umayyah ililenga kuvuruga itikadi za kidini za ummah wa Kiislamu. Aidha katika kipindi hicho, jamii ya Kiislamu ilishuhudia kuibuka nadharia zisizo sahihi za kifalsafa kuhusu misingi ya itikadi.
Licha ya shughuli nyingi za kielimu na kiutamaduni alizokuwa nazo, Imam Baqir (a.s), hakughafilika na masuala ya kisiasa na alikuwa akiwakosoa sana watawala wa kiimla na madhalimu wa zama zake. Katika harakati zake za kuwazindua Waislamu kisiasa, Imam alibainisha sifa za viongozi wema ili kuwafanya watu waweze kuwatia kwenye mizani watawala na kufahamu udhaifu na upotofu wao.
Sheikh Tousi, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu amewataja wanafunzi bingwa wa Imam Baqir (a.s) kuwa ni watu 462. Vigogo na shakhsia wakubwa wa kielimu wa zama hizo wote walifika mbele ya Imam Baqir (a.s) ili kupata angalau tone moja la bahari yake pana ya elimu. Watu kama vile Jabir bin Yazid Ju'fi, Zuhri , Abu Hanifa, Anas bin Malik na Shafi ni kati ya wanazuoni walionufaika na hazina kubwa ya kielimu ya Imam Baqir AS. Muhammad Ibn Talha Shafi'i katika kuelezea sifa za Imam Baqir anaandika: “Alikuwa mwenye kuchana na kunawirisha elimu.
Imam Baqir anasema: “Uongozi wa jamii unamustahiki mtu mwenye sifa tatu. Kwanza ni ucha Mungu ili takwa iweze kumkinga na mitihani na madhara ya madaraka kama vile kutumbukia katika mtego wa ufisadi. Pili awe mstahimilifu ili aweza kuzuia hasira zake. Tatu aamiliane na watu anaowatawala kama baba mkarimu na awe na tabia nzuri”.
Imam anasema katika sehemu nyingine: "Hakuna mja yoyote muumini asiye na nukta nyeupe na yenye nuru kwenye moyo wake. Kila mara anapofanya dhambi nukta nyeusi hudhihiri kwenye nukta hiyo nyeupe. Kwa hivyo iwapo atatubu baada ya kufanya dhambi nukta hiyo nyeusi hutoweka, la sivyo akidumu kwenye maasi nukta nyusi huongezeka na kuenea hadi kufunika kabisa nukta hiyo nyeupe. Baada ya kufunikwa kabisa nukta hiyo nyeupe mtu aliye na moyo kama huo kamwe hatawezi kuona uso wa saada."
Wapenzi wasomaji kwa mara nyingine ninatoa mkono wa pongezi, kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Baqir (a.s), Imam wa Tano katika Maimam aliowataja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa Makhalifa baada yake, wakwanza akiwa ni Imam Ali Ibn Abu Taalib (a.s), Wapili ni Imam Hassan Ibn Ali (a.s), watatu ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s), wa nne ni Imam Ali Ibn Husein -Sajjad (a.s) na Wa tano ni Imam Muhammad Ibn Ali al Baqir (a.s).
Imetolewa na
Twalha Zuberi Ndiholeye
Kiongozi Mkuu wa Baqir Media
Tarehe 09/04/2016, Sawa na 2, Rajab, 1437

Monday, April 4, 2016

Watoto wenye Usonji wanamahitaji kama watoto wa Kawaida Tusiwatenge

Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kutoa elimu bora na Bure kwa watoto wote wa kitanzania bila kubagua rangi,kabila wala dini huku mkazo mkubwa sasa ukielekezwa pia kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanapata elimu sawa.

"Aidha niwatake  wazazi, walezi na jamii bila ya kujali tofauti za kimaumbile kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya elimu, pia jamii inapaswa kuwachukulia watu wenye mahitaji maalumu kama ni sehemu muhimu ya jamii na wanasshirikishwa kikamilifu katika nyanja zote za Maendeleo" amesema Dr. Manyanya

Kauli hiyo hizo zimetolewa na Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dr. Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaamMaandamano hayo yameratibiwa na shule ya Al Muntazar na kushirikisha matabibu, waalimu wanafunzi, Changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo miongoni mwa jamii kuhusu ulemavu huo.

Huku wengine wakiuchanganya ulemevu huo na mtindio wa ubongo, wengine wanauhusisha na imani za kishirikina,jambo ambalo limesababisha ugumu katika matunzo ya watoto wenye Usonji" anasema Dr Stella Rwezaura, rais wa chama cha watu wenye Usonji Tanzania.

Usonji ni upungufu wa kibaiologia anaopata mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake na dalili zake huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea ambapo.

Maadhimisho ya watu wenye usonji huazimishwa kila tarehe 2, ya mwezi april ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE.Picha zaidi Bofya chini.
 
Hatahivyo Dr. Manyanya amesema kuwa Serikali kwa ikishirikiana na sekta binafsi na wadau wa elimu imekuwa ikipanua fursa za upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuandaa walimu, kuboresha miundombinu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika elimu.

"Napenda kuipongeza Taasisi yenu ya Almuntazir kwani imekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia watoto wenye usonji na wenye mahitaji mengine maalumu kwa kuwapatia elimu na huduma nyingine za Kijamii" amesema Dr. Manyanya

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam



Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam

Sunday, March 20, 2016

Iran na Uturuki zasisitiza ushirikiano wa pande mbili

Iran na Uturuki zasisitiza ushirikiano wa pande mbiliMawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Istanbul na kujadili masuala ya uhusiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa.

Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko nchini Uturuki kwa ziara rasmi amefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake, Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki. 

Dakta Zarif amesema, misimamo ya Iran na Uturuki kuhusiana na matukio ya Mashariki ya Kati inakaribiana sana na kwambva, Tehran na Ankara zinasisitiza juu ya kulindwa umoja wa ardhi ya Syria.
Waziri Zarif amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga baadhi ya njama za kutaka kuigawa ardhi ya Syria na kuongeza kuwa, siasa za Tehran zimesimama juu ya msingi wa kuheshimu umoja na mamlaka ya nchi zingine.
Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililotokea leo katika mji wa Istanbul na kubainisha kwamba, shambulio hilo lililo dhidi ya ubinadamu limezidi kuonesha sura mbaya ya ugaidi.
Kwa upande wake Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki sambamba na kuashiria kwamba, Uturuki ina wakimbizi zaidi ya milioni tatu kutoka Syria amesema kuwa, Tehran na Ankara zitafanya hima ya kuhakikisha umoja wa ardhi ya Syria unahifadhiwa.Chanzo irib