Monday, May 8, 2017

Sheikh Jalala atoa pole, awataka Wazazi wafiwa kuwa na subira na Uvumilivu kwa kuwapotea watoto wao Wanafunzi wa Lucky Vicent, Arusha

Kiongozi Mlkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania akitoa salamu za polena rambirambi kwa msiba wa wanafunzi 32 wa lucky Vicent leo Majid Ghadie,Kigogo Post Dar es salaam.
Kikao na Waadishi wa Habari, Kimechofanyika leo, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, Msiba wa Wanafunzi 32 pamoja na Walimu, Wa shule ya Lucky Vicent, Mkoani Arusha.

Kwa jina la Mwenyezimungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu.

Innalilah Wainna lilah Rajiiun
Sisi sote tumetoka kwa Mungu na sisi sote mwisho tutarudi kwa Mungu.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa na kwa huzuni ya hali ya juu, isiyokuwa na kifani, ajali ya basi ya shule ya Lucky Vicent ya mjini Arusha iliyotokea katika eneo la mrima Rotia, Karatu na kusababisha vifo vya baadhi ya wanafunzi waiopungua 32 ikiwemo baadhi ya walimu,

Sisi kama Watumishi wa Imam Swadiq (a.s) makao makuu yapo hapa Kigogo Post Dar es salaam, sisi kama Waislamu, vilevile sisi kama waislamu wafuasi wa madhehebu ya Shia Tanzania tunaungana na watanzania wenzetu wote  waslamu na wakristo wanaoishi Tanzania kutoa mkono wa Pole kwa wazazi, kwa wanafunzi wote waliofiwa,na uongozi mzima wa shule ya Lucky Vicent na wanafunzi wenzao ambao bado wapo shuleni hapo.
 Image may contain: 4 people, people sitting and camera
Na vilevile tunatoa mkono wa pole kwa taifa letu takatifu kwa ujumla na vilevile tonatoa pole kwa muheshimiwa Raisi wa Taifa hili la Tanzania Dr. John Magufuli.

Napenda kusema hili limetugusa kwa dhati kama waumini, kama watanzania, kwasababu tunaposoma katika quran ndio kitabu chetu waislamu, inatuambia yakwamba “Waumini wote ni ndugu”  kwahivyo lililotokea limewakumba waumini wenzetu,ni wajibu wetu kama watanzania pasia kubaguana  kidini,  kiitikadi kimadhehebu,kupendana kuelewana na kuwa pamoja wakati wote waraha na wakati wa majanga kama hili limetukumba  katika kipindi hiki.
 Image may contain: 1 person, sitting and on stage
Mtume Muhammad (s.a.w.w) anaema; hakika sifa ya waumini wanatabia ya kupendana na kuhudhumiana  kama vile unavyoona mwili mmoja,  kiungo kimoja kinapougua na viuongo vingine vinakesha kwa kuugua haviwezi kubakia salama salmini.

Mwisho Mungu awape wafiwa subira uvumilivu, na wote waliotangulia mbele ya haki Mungu wapokee roho zao kwa mikono miwili na awaweke mahala pema  ndani ya pepo takatifu, na sisi tuliobakia hapa nchini Tanzania Mungu atupe upendo, atupe mshikamano, atupe umoja, atupe kuvumiliana, atupe kuenzi amani na utulivu tuliokuwa nao , Mungu ibariki Tanzania wabariki watu wake wote  wabariki viongozi wake, amiin amiin amiin,Asateni sana.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

“Amani, maelewano na masikilizano kwa watu wenye Dini zote Tanzania lazima itunzwe kwa hali yoyote” Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwasilisha mada yake mbele ya hadhira katika Ukumbi wa Nkurumah, University of Dar es salaam, jijini Dar es salaam.
   Na Twalah Ndiholeye

Amani ya Mwenyezimungu iwe kwenu
Semina “Dini na Maadili  ya Ubinadamu Ulimwenguni”
Ukumbi wa Nkurumah, Univesity of Dar es salaam.
06/05/2017

Semina hii imeyowekwa mahala hapa Chuo Kikuu malengo yake makubwa ni malengo ya kumuangalia Mwanadamu, madhumuni makubwa ni kuangalia nafasi ya mwanadamu, katika maisha ya kila siku, na vile vile malengo makubwa  ya Semina hii kuwekwa katika ardhi ya Tanzania katika Mkoa wa Dar es salaam,

Bila shaka leo hii duniania inakabiliwa na Vita vya wenyewe kwa wenyewe, dunia inakabiliwa na kukosa amani, dunia inakabiliwa namauaji ya kinyama, dunia inakabiliwa na matatizo ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya kuumbwa mwanadamu.

Na kwa bahati mbaya yanayotokea leo hii wakati mwingine yanatokea kwa jina la dini, yanatokea kwa jina la Uislamu,kwamba anaefanya ni Mwislamu, yanatokea  anaefanyiwa ni Mwislam, vilevile kwa hivyo malengo makubwa ni kutaka kuleta mwanga na kuleta maelekezo, ya kwamba dini zote ikiwemo dini ya Uilamu, zikiwemo dini ya Ukristo pamoja na Uyahudi, dini zote malengo yake makubwa ni kukaa vizuri na mwanadam, 

malengo yake makubwa ni kuleta amani, malengo yake makubwa ni kuleta mshikamano, malengo yake makubwa ni kuleta kuvumiliana katika jamii, ya watu wanaoishi wenye mitazamo tofauti, na fikra tofauti na rai tofauti kuweza kukaa pamoja, ndio malengo makubwa ya kutumwa mitume wote mnaowatambua, ndio malengo ya makubwa ya vitabu vya mwenyezimungu vyote vilivyotoka minguni,kwanzia taurati,injiri, zauri mapaka kufikia Quran tukufu,

Nukuta ya pili kwanini semina hii yenye lengo ya mwanadamu wote kumtengeneza mwanadam,kumnyosha mwanadamu katika hali ya Tanzania,  Mtakubaliana namimi ya kwamba Tanzania imekuwa ikijulikana katika historia  ni kisiwa cha amani, Dar es salaam, ukijulikana ni mji wa amani, Tanzania imekuwa na sifa tofauti na nchi zingine, Tanzania inasifa ya watu wake wanaishi katika amani, inasifa  watu wake hawajui kubaguana kidini, kimakabila,kimadhehebu, 


na kifikra ,
Watanzania wamekuwa wakikaa pamoja bila ya kubaguana, kwa aina yeyote, bali hadi makabila yao hawajuiani wakati mwingine, inawakusanya pamoja lugha ya Kiswahili.
Kwahiyo semina kama hii kufanywa katika sehemu kama hii ya Tanzania ni kutoa maelekezo na kutoa funzo kwa vijana haswa,

 kwamba utulivu huu, busara hii, hekima hii, kukaa huku pamoja kwa watu wenye dini zote lazima kuweziwe, lazima kubakishwe, lazima watu wafanye bidii yoyote inayowezekana hali kama hii ya utulivu iweze kuendelea. Aanteni sana.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

Monday, April 3, 2017

Dr. Bilal "Watoto wenye Usonji wapewe fursa kama watoto wengine"

Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne,, akiongea Mbele ya Hadhira  katika Shule ya Al-Muntazir Girls. kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani.
Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Mohammed  Gharib Bilal amewataka wadau mbalimbali kuwapa fursa watoto wenye usonji ili waweze kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zitakazo wafanya wasijione wapweke.

Makamu wa Rais  Mstaafu Dk. Bilal alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na Taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir ambapo ameipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha kitengo maalum kinachotoa mafunzo kwa watoto wenye usonji na kufafanua kuwa siyo kazi rahisi kwani inahitaji rasilimali watu.
 
 wataalamu, fedha kuwa na moyo na uthubutu hivyo wadau na serikali kwa pamoja waunge mkono jitihada hizo na atafikisha kilio hicho kwa serikali ili kuunga mkono jinsi ya kuwasaidia watoto hao.
 Matembezi hayo yalikuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE” ikiwa na maana ya kuwapenda na kuwapatia ulinzi watoto wenye mahitaji maalumu.  
 
 Dkt bilal aliongeza kuwa kwa kutambua athari za ugonjwa huo wa asonji ipo haja kwa jamii kujitoa kwa hali na mali hili kuwafanya na wao kujisikia kuwa ni sehemu ya jamii kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
 
Mgeni Rasmi Dr. Bilal aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja taslimu alizo zitoa hapo akimkabidhi Mwenyekiti wa Khoja Shia Itha ashel Jamaat central board of education Mr Intiaz Lalji kwa kuweza kuongeza nguvu katika zoezi la kuwasaidia vijana hao. Huku akiwasilisha mchango Makamu wa Raisi wa sasa Mama Samia suluhu aliyeweza kutoa mchango wa million 5.
 
Imtiaz Lalji Mwenyekiti wa KISJ Central Board of Education akiongea mbele ya hadhira kwenye Maadhimisho ya Watu wenye Usonji Duniani katika Shule ya Al-Muntazir Boy, Dar es salaam.
 Kwa upande wake Mwenyejkiti wa Taasisi ya KSIJ Center of education bwana Imtiaz Lalji alitoa wito kwa  jamii kuwa karibu na watu wenye ugonjwa wa usonji sambamba na kuwasaidia kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Alisema kupitia taasisi ya KSIJ  Center of education tayali wameshatoa mafunzo kwa wanafunzi watatu wenye usonji na mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo wamewaajilikama walimu wasaidizi shuleni hapo hivyo kutoa wito serikali pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuanza kutoa nafasi za ajila kwa watu hao.
Imtiaz Lalji Mwenyekiti wa KISJ Central Board of Education akipokea zawadi ya Pesa Taslim kutoka kwa Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne, wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani.

Dr.Bilal awa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Usonji Duniani

Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne,(alievaa miwani meusi), akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Matembezi ya Amani kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani, jana katika Shule ya Almutazir Boy Primary School, Upanga Dar es salaam.
Imtiaz Lalji Mwenyekiti wa KISJ Central Board of Education (kulia) akiwa na Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne (watatu kulia), akiongea Mbele ya Hadhira  katika Shule ya Al-Muntazir Girls. kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani


Imtiaz Lalji Mwenyekiti wa KISJ Central Board of Education akipokea zawadi ya Pesa Taslim kutoka kwa Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne, wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani
Mr.Azim Dewji-Raisi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Ashery Jamaat (kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne, katika Shule ya Al-Muntazir Girls. kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani

Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne,, akiongea Mbele ya Hadhira  katika Shule ya Al-Muntazir Girls. kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani

Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne,, akiwapungia Mgono ikiwa ni ishara ya kuwaaga hadhira katika Shule ya Al-Muntazir Girls. kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani

Mgeni Rasmi Dr.Mohammed Gharil Bilal Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitafu awamu wa nne,akimsukuma mtoto mwenye mahitaji maalumu, kwenye Maadhimisho ya siku ya watu wenye Usonji Duniani





Tuesday, March 21, 2017

Sheikh Jalala “Mwanamke anahaki ya Kufanya Kazi, Kuongoza, Kuajiriwa, Kuajiri, Kurithi,kuwa Kiongzozi kama Raisi, Waziri, Ubunge na Uwakilishi”

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habaei jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Napenda kuanza Mazungumzo yangu kwa kuanza maneno kutoka katika Quran suratul Kauthar, Mwenyezimungu aliposema “Hakika sisi tumekupa kheri nyingi” kheri nyingi hizi Wasomi wa Kiislam wametafsiri kwamba makusudiwa hapa ya kheri nyingi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupewa Binti anaeitwa Fatuma (a.s) akijylikana maarufu kwa Jina la Fatuma Zahra (a.s) .

Siku hii ya leo tunakumbuka kuzaliwa kwa binti yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), Bi Fatuma (a.s) alizaliwa tarehe 20 Rabil Akhiral mwaka wa 615 AD, Siku ya kuzaliwa Mama huyu ni siku kubwa ambayo sisi Waislamu tunapenda kumuenzi huyu mwanamke na kuieleza jamii na Walimwengu vipi Waislamu wanamuangaliwa MWANAMKE, vipi waislamu wanamtazama Mwanamke.

Mtakubaliana na mimi kabla ya Uislamu mwanamke kwenye makabila tofauti na kwenye dini tofauti alikuwa hana dhamani, bali tunakumbuka baadhi baadhi ya dini zilikuwa hazimruhusu mwanamke hata kuingia msikitini kuswali , hata kuingia kwenye nyumba ya Ibada iwe ni Sinagogi au iwe ni kanisa au iwe ni Msikiti.

Lakini Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuja kusomesha tofauti akaja Mtume akamuonyesha Mwanamke kwamba ni Mwanadamu kama mwanadamu mwingine, Mtume akamuonyesha Mwanamke  kwamba kama vile Mwanaume kuwa na haki vile vile mwanamke ana haki, Mtume akaonyesha usawa kati ya Mwanaume na Mwanamke “Tumewaumbeni kwa Mwanaume na Mwanamke”.

Kwahivyo Mtume akaonyesha usawa kati ya Mwanamke na Mwanaume kwamba hakuna tofauti kwa haki zinazowastahiki kutoka kwa Mwenyezimungu (swt) si hilo tu Uislamu kupitia Mtume Muhammad (s.a.w.w) na katika Quran tukufu, kwamba la si kama watu wanavyomtafsiri Mwanamke, Mwanamke ni Mwanadamu aliekamilika kama alivyokuwa Mwanaume amekamilika.
 
Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Kikao hicho cha Kumzungumzia Nafasi ya Mwanamke katika Uislamu katika jamii kwa mtazamo wa Kiislamu.
Uislamu ukatupa mafunzo makubwa zaidi na kutuonyesha Mwanamke ndie anaetengeneza Umma, mwanamke ndie anaetengeza watu, ndie alietengeza wanaume waliofanya mabadiliko, maeneno mashuhuri “Jambo lolote kubwa unaloliona ujue nyuma kuna mwanamke, hivi ndivyo mwanamke uislamu unavyomuangalia.

Kila jambo kubwa unaloliona nyuma yake yupo Mwanamke, Nabii Mussa (a.s) mmoja katika mitume wa Mungu, ni kwanini aliweza kumshinda Firauna au Farao, ni kwasababu nyuma yake kulikuwa na Mwanamke ambae ni Mama Asia (a.s), Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwanini aliweza kuueneza Uislamu, kwasababu nyuma yake kulikuwa na Mwanamke amabe ni Mama Khadiha (a.s).

Kwahivyo unapoangalia watu wakubwa duniani nyuma palikuwa na Mwanamke, Mwanamke ndie alieleta mabadiliko , lakini sio hivyo tu, unatambua wewe ili uwe Raisi ili kuwa waziri,ili uwe mtu wa Kitaifa au Kimataifa inahitaji malezi kwanza, Msimamizi wa Malezi hakuna isipokuwa ni Mama amabe ni Mwanamke tu.

Kwahivyo Uislamu unamuangaliwa Mwanamke ndie anaetengeneza watu, ndie anaetengeneza wanaume, ndie anaetengeza ushindi, na tumemuona Mtume Muhammad (s.a.w.w) alivyohamiliana kwake na watu, katika kuhamiliana na wanawake na akionyesha mfano wa ajabu, tunamuona mtume Muhammad (s.a.w.w) akifanya mbele ya huyu Fatuma (a.s)  amabae tunakumbuka leo kuzaliwa kwake.

Mtume Muhammad (s.a.w.w) huyu Bint Fatuma (a.s) anaingia nyumbani kwake, anapoingia Fatuma (a.s) Mtume Muhammad (s.a.w.w) anamsimamia bint Fatuma (a.s), na sio kumsimamia tu, bali anamsimamia pamoja na kukamata mkono wake na kuubusu alafu anamkalisha karibu yake, jambo ambalo kipindi hicho katika jamii ile ilikuwa ni jambo halipo.

Nukta Maranyingi hujadiliwa Sana duniani kwamba Uislamu mbona unaaina fulani ya dhulma kwa mwanamke, tunasema la au Hapana,Bali katika dini ambazo zimempa haki  mwanamke hakuna kama vile Dini ya Uislamu, na kama zipo bali ninasema Uislamu ni dini ya kwanza kwa taratibu nzuri, na kwa mbinu nzuri na kwa namna nzuri.

Kwa mfano haki ya Kumiliki, Je, Mwanamke anaruhusiwa kumiliki ndani ya Uislamu? Uislamu kupitia Quran inajibu wazi wazi kama vile mwanaume anavyoweza kumiliki mali yake pia Mwanamke anaouwezo wa kumiliki mali yake, kwahivyo haki ya kumiliki ni haki ya Mwanaume na Mwanamke ndani ya Uislamu.
Uislamu haukufanya anaemiliki ni Mwanaume tu, hapana,anaemiliki ni Mume anaemiliki ni Mke. Wote wawili wanayohaki ya kumiliki.


Haki ya Uongozi, Je mwanamke katika uislam anayohaki ya kuwa Kiongozi? Uislamu unasema ndio. Mwanamke anayohaki na nafasi ya kuwa Kiongozi kuanzia ngazi ya Uwakilishi, ngazi ya wizara, ngazi ya usimamizi wa mambo katika ngazi hizi zote mwanamke anaouwezo wa kusimamia na mwanamke anaouwezo wa kuongoza.

Haki ya Kufanya Kazi, Mwanamke katika dini ya Uislamu anayohaki ya kufanya kazi awe ni Bosi, iwe ya kuajiri, iwe ni kuajiriwa haki hiyo anayo katika uislamu kama alivyokuwa nayo Mwanaume.Bila shaka Uislamu umeweka utaratibu ni nguo gani anatakiwa kuvaa mwanamke, bila shaka ni kwa maslahi na heshima ya mwanamke. Kwasababu Uislamu unamuangalia Mwanamke kwamba ni mtu mtakatifu, Uislamu unamuangalia Mwanamke ni mtu anaetengeneza watu.

Kwahivyo Mwanamke hazuiliwi kufanya kazi yoyote ambayo ipo ndani ya misingi ya Uislamu na ambayo ipo ndani ya Misingi ya Sheria.

Na katika jambo linguine dunia inajiuliza , je mwanamke anayohaki ya kuendesha gari? Ndio mwanamke anayohaki ya kuendesha gari, mwanamke anayo haki kama aliyonayo haki Mwanaume, haki ya kuendesha gari, iwe gari ya kuajiliwa, gari binafsi muda wa kuwa hajatoka katika mipaka ya Kiislamu.

Haki ya kusimama mbele ya Wanaume, Mwanamke katika Uislamu anayo haki kutoa Mada mbalimbali, anayohaki ya kuzungumza mbele ya watu wa aina yoyote muda wa kuwa hilo halivunji taratibu na misingi ya Dini ya Uislamu, tumeona wanawake katika Uislamu waliosimama mbele za watu wakawa wahubiri, wakasema, Bi Fatma (a.s) ninaemzungumza leo hii, amabe tunakumbuka kuzaliwa kwake, tunamkuta katika historia vipi ametoka nyumbani kwake ameenda mpaka msikitini kutoa Khutba , kuongea na watu,
Si hivyo tu tunamuona Bi FATMA (a.s) akizungumza kwa watu aina tofauti waliokuwa wanamzunguka, sio yeye tu wapo wanawake wengi kama Bi Zaynab (a.s), Bint wa Sayyidina Ali (a.s) tunamkuta nay eye anatoa Khutba mbele za Wafalme, mbele za watawala, na mbele za watu toafauti.

Haki ya kurith, je mwanamke anaweza kurith? Ni katika maneno yanayotumika kuuzungumza vipaya Uislamu. Naema hapana, Uislamu umemrithisha mwanamke, mwanamke anayohaki ya kuruthi katika namna mbili, upande wa kwanza, mwanammke anayohaki ya kurithi upande wa familia yake, kwa ibara nzuri mwanamke anayohaki ya kumrithi Baba yake, Mama yake, Kaka yake na Mtoto wake awe wa kiume au wakike,upande wa pili anayohaki ya kurithi upande wa Mume wake pindi mume wake anapofariki dunia.


Katika siku kama ya leo tunapokuwa tunakumbuka kuzaliwa kwa Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Bi Fatma Zahra (a.s)  ni siku ya kuwaeleza watu, Umma na Dunia Nafasi ya Mwanamke katika Jamii kwa mtazamo halisi wa Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) vipi umemuweka Mwanamke.

Mwisho napenda kutoa hongera kwa ndugu zangu wote, Waislamu na Watanzania na wasiokuwa Watanzania na watanzania wote kwa kuzaliwa Mama huyu, Bint wa Mtume (s.a.w.w), ni siku ya sisi ya kumueleza mwanamke haki alizopewa na vipi Uislamu ulivyomnyanyua Mwanamke na kumuweka daraja kwamba ni mwanamke Muheshimiwa ni mtu kama mtu wa kawaida na wala hana mapungufu yoyote ambayo unaweza kusema. Asanteni sana Alhamdulillah Rabil aalamiiin.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
20/03/2017 sawa na 20 Rabil Akhir 1438

Wednesday, March 15, 2017

Jeshi la Syria lakomboa misikiti mitatu toka mikononi mwa Daesh

Jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Syria vimekomboa misikiti mitatu iliyokuwa chini ya udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, mashariki mwa mji wa Damascus.


Duru za kijeshi zimeripoti kuwa, misikiti iliyokombolewa na jeshi la Syria ni ile ya al-Noman, al-Hussein na al-Qassem, iliyoko katika eneo la al-Qaboun, mashariki mwa Damascus.


Habari zaidi zinasema kuwa, magenge hayo ya kigaidi yamekuwa yakiitumia misikiti hiyo kupanga njama na harakati zao za kigaidi.


Wakati huo huo, jeshi la Syria limefanikiwa kutibua shambulizi la kigaidi ambalo Daesh ilikuwa inataka kutekeleza katika mkoa wa mashariki wa Dayr al-Zawr. Mashambulizi ya mabomu yalitokea mjini Damascu Jumamosi ikliyopita na kuua na kujeruhi makumi ya raia wasio na hatia. 


Haya yanajiri katika hali ambayo, duru ya tatu ya mazungumzo ya Astana inatazamiwa kuanza leo Jumatano kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa Iran, Russia na Uturuki pamoja na mwakilishi wa Jordan, Bashar al-Jaafari anayeiwakilisha serikali ya Syria na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa.


Duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria ya Astana ilifanyika tarehe 23 na 24 Januari na ile ya pili ilifanyika tarehe 15 na 16 Februari katika mji mkuu wa Kazakhstan.

Wednesday, March 8, 2017

Snowden: iPhone na Android zinatumiwa na CIA kunasa mazungumzo ya watu

Afsia wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) amesema mifumo ya simu za iPhone na Android inatumiwa na vyombo vya ujasusi vya Marekani kudukua na kunasa sauti na mazungumzo ya watu katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Edward Snowden amesema maelfu ya nyaraka za siri za shirika la ujasusi la Marekani CIA zilizofichuliwa na mtandao wa WikiLeaks zimethibitisha tena kwamba mashirika ya ujasusi ya Marekani yanadukua na kunasa mazungumzo ya simu za kiganjani hususan zile zinazotumia mfumo wa iOS wa simu za  iPhone na ule wa Android.

Jumanne ya jana mtandao wa WikiLeaks ulichapisha sehemu ya kwanza ya nyaraka na mafaili ya siri ya shirika la ujasusi la Marekani CIA katika majmui iliyopea jina la Year Zero. Nyaraka hizo za siri zinafichua kuwa, CIA imekuwa ikifanya ujasusi wa kunasa na kusikiliza mazungumzo ya watu wanaotumia simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple na zile zinazotumia mifumo wa Android  na Microsoft na vilevile televisheni za Samsung kwa ajili ya kufanya ujasusi na kudukua sauti na mazungumzo ya watu katika pembe mbalimbali duniani.
Afisa wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) Edward Snowden anasema kufichuliwa nyaraka hizo kunathibitisha tena kwamba, mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo yanajasisi na kunasa sauti za watumiaji wa simu za kiganjani.

Afisa huyo wa zamani wa NSA alikimbia Marekani mwaka 2013 akiwa na rundo kubwa la nyaraka za siri za mashirika ya ujasisi ya nchi hiyo na kwa sasa amepewa hifadhi nchini Russia.