Friday, March 21, 2014

TFF Na Benki Ya CRDB Zimeunda Kikosi Kazi Kwa Ajili Ya Kushughulikia Ya Tiketi Za Elektroniki




Afisa Mawasiliano Shirikisho la Soka Tanzania Boniface Wambura  amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB zimeunda kikosi kazi (task force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi za elektroniki ambayo yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza.

Amesema TFF na CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya uboreshaji matumizi ya mfumo huo.



Aidha amesema Kikosi kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.



Hatahivyo amesema Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao akiongoza timu yake.





amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.


Sunday, March 16, 2014

Bodaboda 400 waandamana hadi ofisi za Chadema Kinondoni

Zaidi ya waendesha pikipiki na bajaji 400 wameandamana kuelekea Makao Makuu ya Chadema, yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kupinga kitendo cha kukatazwa kuingiza vyombo vyao vya moto katikati ya Jiji. 
 
Vijana hao wakiwa na vyombo vyao vya usafiri pamoja na mabango yenye ujumbe tofauti walifika kwenye ofisi hizo jana asubuhi wakitokea maeneo tofauti jijini.
 
Baadhi ya mabango yao yalisomeka hivi ‘ubakaji, wizi utaongezeka.
Baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo, madereva hao walianza kuimba ‘tunamtaka Rais wetu, tunamtaka Rais wetu, peoples power”, wakiimaanisha Dk. Wilbroad Slaa.
 
Wakati nyimbo hizo zikiendelea nje ya ofisi hizo, Dk. Slaa alikuwa hayupo na alipowasili alipokelewa na kelele ‘Rais wetu, Rais wetu, Rais wetu’. Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema, mara baada ya kushuka kwenye gari lake aliwatuliza vijana hao na kuwaeleza kuwa baada ya kupata taarifa zao aliwasiliana na vyombo vya dola.
 
“Nimewasiliana na ngazi zote za polisi akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, kamanda wa jeshi la polisi mkoa na mkuu wa upelelezi na kukubaliana nao hakuna mabomu,” alisema na kuongeza:
 
“Mtu anapokimbilia hapa maana yake yupo katika usalama, Chadema isiyopenda kumwaga damu tunaweza kupata suluhu bila mabomu,” alisema.
 
Dk. Slaa alisema amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na kwamba amekubali kukutana nao Jumatatu wiki ijayo

7 Wafariki katika msongamano wa kutafuta kazi Nigeria

Watu wasiopungua saba wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kufuatia msongamano wa maelfu ya watu. 

Msongamano huo ulijiri Jumamosi wakati watu walipokusanyika kuajiriwa katika idara ya uhamiaji. Zoezi hilo lilikuwa likifanyika katika uwanja wa kitaifa wa michezo Abuja. 

Walioshuhudia wanasema mkanyagano ulijiri pale watu walipojaribu kufika katikati ya uwanja ambapo kulikuwa na mlango moja tu uliokuwa wazi katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu 60,000. 

Bado haijabainika idadi ya watu waliokuwa ndani ya uwanja wakati wa msongamano huo. Idara ya uhamiaji Nigeria ilikuwa inaendesha zoezi hilo katika maeneo kadhaa nchini humo.

Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta ya petroli  magharibi mwa Afrika ambapo imearifiwa kuwa asilimia 37.5 ya vijana walio chini ya umri wa
miaka 25 hawana kazi.irib

Tuesday, January 21, 2014

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

MZUNGUKO WA VPL KUANZA JUMAMOSI
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa uwanja mwingine.http://twalhanews.blogspot.com/

Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.

Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyazi zake ambazo zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.

Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.

Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.

TWIGA STARS KUIVAA ZAMBIA FEB 15 LUSAKA
Tanzania (Twiga Stars) itaivaa Zambia katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano ya mchujo ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Februari 15 mwaka huu jijini Lusaka.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma kuanzia saa 9 kamili kwa saa za Zambia na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda.

Mukansanga atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake; Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na Angelique Tuyishime. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka Namibia.

KISHONGOLE, KESSY KUSIMAMIA MECHI ZA CAF
Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 mwaka huu
Kishongole ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana Rakotojaona.

Naye Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali.

Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. PEREIRA SILIMA AELEZEA MAFANIKIO YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YALIYOFIKIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA NNE.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(katikati) akitoa taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es as Salaam(kulia) ni Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve(Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo, Bw. Assah Mwambeni.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwa pamoja na Viongozi Wengine Wakuu wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akitoa taarifa rasmi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne(wa pili kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Pius Nyambacha.

Baadhi ya Wakurugenzi mbalimbali wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Prereira Silima kwa Waandishi wa Habari leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam

Monday, January 20, 2014

Hali ya uchafu katika soko la Kitumbini,jijini Dar es salaam





Hiiindio chemba inayomwaga maji machafu kutoka katika eneo kuchinjia mifungo aina ya kuku katika soko la kitumbini liliopojijijni Dar es salaam


Hawa ni Baadhi ya Wafanya Biashara katika Soko la Kitumbini liliopo Jijini Dar es salaam, wakiendelea kufanya Bishara zao za kila siku bila ya kujali hali iliyopo katika eneo hilo.

Sunday, January 19, 2014

Matembezi ya Amani juu ya Kukukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w)


Hawa ni baadhi ya Wanafunzi wa Hawzat ya Imam Swadiq (a.s) iliyopo Kigogo,Jijini Dar es salaa,wakiwa katika mstari wa mbele katika kukumbuka mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye alizaliwa tarehe 17, Rab bil awal, mwaka wa 570 (AD),http://twalhanews.blogspot.com/


Na hawa ni mabinti paomoja na kinamama wakishirikiana kwa pamoja katika kukukmbuka mazazi ya mtume ambao walitoka maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Shekh Muhammad Abdi mwalimu msaidizi wa Hawzat ya Imam Swadiq (a,s) akiwa akifafanua kazi ya Mtume Muhammad(s,a,w.w) katika kupigania ,Amani,upendo na ushirikiano bila ya kujali itikadi, ukabila na jinsia, pembeni yake ni mwanafunzi wa Hawzat ya Imam swadiq..