Wednesday, November 28, 2018

Michezo ni katika Mafundisho ya Mwenyezi Mungu-Sheikh Abdu


Naibu Mkuu wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Sheikh Muhammad Abdu amewataka Viongozi wa Dini kuhamasisha Vijana kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Mpira wa Miguu, kwani inapelekea Amani katika maeneo yetu tunayoishi pamoja nan chi kwa ujumla.

“Lakini vilevile ni mchezo unaoweza kuleta amani, katika maeneo yetu, leo tuko hapa mambo mengi huko mitaani yamesimama, kama mtaa wetu una vibaka, vibaka wote wako hapa, kama kuna wezi wote wako hapa, inamaana mambo yote machafu hayafanyiki.” Alisema Sheikh Abdu.

Sheikh Abdu alisema hayo jana katika Fainali ya Lingi ya Mtume (s.a.w.w) Cup, kwa kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), uliochezwa katika Viwanja vya Pipo Kigogo Post Dar es salaam.

Sheikh Abdu ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu T.I.C amesema kuwa Michezo ni katika mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake pale ambapo Uislamu unasema Mwislamu mwenye nguvu na mwenye Mazoezi anapendwa zaidi mbele ya Mungu kuliko Mwislamu dhaifu ambae hana nguvu na hafanyi mazoezi.

“Na hii inatupa picha kwambaMichezo sio tukio linalofanywa na watu pengine ni wahuni au ni watu ambao hawana Kazi,Tukio la Michezo ni tukio hata watu wa dini wanatakiwa walitile nguvu na walifanye kwasababu ni moja katika maamrisho Mungu na vilevile ni mafundisho ya Uislamu kwamba, Mwislamu mwenye nguvu na mwenye Mazoezi anapendwa zaidi mbele ya Mungu kuliko Mwislamu dhaifu ambae hana nguvu na hafanyi mazoezi” Alisisitiza Sheikh Abdu.




Tuesday, November 27, 2018

Matembezi ya Kukumbuka Kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) ni Kuonyesha Huruma ya Mtume”-Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa moja ya lengo la kufanya Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya Huruma tuwenayo Binadamu Tanzania na Dunia kwa Ujumla.

“Matembezi haya ya Amani ya kukumbuka Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuweza kuieneza katika mitaa yetu na Sehemu zetu na Tanzania kwa ujumla, kwani Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliletwa kwa watu wote na sio kwa watu Fulani tu” alisema Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alisema hayo jana katika Matembezi ya Amani (ZAFA) YA Kukumbuka Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu T.I.C pamoja na Hawzat Imam Swadiq Kigogo Dar es salaam.

Sheikh Jalala alisema kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) anafundisha huruma kwa watu wote bila kujali tofauti za dini,tofauti za madhehebu, tofauti za Kifikra na Kimtazamo, na tofauti za Rangi na Taifa.

“Mitaa hii ya Kigogo imejaa watu wenye dini tofauti, watu wenye madhehebu tofauti, watu wenye mitazamo tofauti, watu wenye rangi tofauti, matembezi haya ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kumuunga Mkono Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwamba yeye aliletwa kwa ajili ya watu wote”.

Aidha ametataka Viongozi wa dini ya Kiislamu, Kikristo, Wanasiasa na Viongozi wa Serikali kujenga mazoea ya kuwatembelea Wananchi wao bila kujali tofauti za hali ya Kimaisha pamoja na Kipato walizonazo wananchi wao kwani kufanya hivyo ni kumuenzi mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.w).

“Matembezi haya ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya waziwazi ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliingia Mitaani, kukutana na watu, kukutana na watu wa kawaida, kukutana na watu amabo sio matajiri na wala sio watu wenye uwezo mkubwa, malengo makubwa ni kuwaleta watu pamoja na kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja bila kuwabagua dini.”

Kwauapande wake Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikh Ramadhani Mwelekwa amewataka Watanzania kuendelea kuwa na Umoja na Mshikamano kwani kufanya hiyo ni kuenzi Mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu akiwemo Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Nabii Issa/ Yesu Kristo.

“Waislamu wote na wale hawajabahatika kuwa waislamu tumeungana kwa ajili ya kuonyesha Umoja na mshikamano ambao ndio lengo la kutumwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunafurahiya wote bila kujali itikadi zetu za kimadhehebu na wale ambao mnatuona Mitaani lengo kubwa ni kufikisha Ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa watu wote na Ulimwengu wote

Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo, Wanasiasa na Viongozi wa Serikali Tusije Tukalaghaiwa, Umoja tulionao Watanzania tukausambaratisha” Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala ameataka Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo, Wanasiasa pamoja na Viongozi wa Serikali kudumisha na Kuenzi UMOJA huu tuliyonao Watanzania pamoja na kuwataka kutolaghaiwa tukafikiwa mahala Umoja huu ukasambaratika.

“Jambo Muhimu tuondoke nalo, Kikao kinachoweza kuwakusanya Waislamu Shia Ithnasheriya, AhlulSunna, Maibadhi,Wasiokuwa Waislam Wakristo, Mayahudi hili ni jambo la kuenziwa, Waislam, Wakristo na Wanasiasa ambao mpo katika Jukwa Kuu, tusije tukalaghaiwa, tukafikia mahala umoja huu wa Kimadhehebu, Kidini na wa Kitanzania ambao ndio sababu ya utulivu huu unaouona na kujivunia huku tulikokuanako ni jambo la kuenziwa na Masheikh, Maskofu, Wanasiana pamoja na Viongozi wa Nchi” Alisema Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alitoa wito huo jana katika Hafla ya Kusheherekea Kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, iliyofanyika Jana chini ya Usimamizi wa Jumuiya ya Waislamu T.I.C Pamoja na Hawzat Imam Swadiq , Iliyofanyikia jana katika Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam.

Kwa upande wake Mhe. Ali Mkomwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe akiongea kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo aliwataka Waislamu pamoja na Watanzania kudumisha Amani na Umoja wa Waislamu.

“Jambo la Kwanza Mhe.Waziri alichoniagiaza ni swala la Amani, ili tuwehuru katika kufanya Ibada zetu na mambo yetu,kuna watu leo hawapendi kuona utulivu huu uliopo, jambo la pili aliloniambia niseme ni Umoja wetu wa Kiislamu, na kwa bahati nzuri Sheikh Alhad amelizungumza kwa upanda sana” Alisema Mkomwa

Nae Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa amesema Swala ya Umoja wa Kiislamu ni Jambo muhimu Sana na kuwataka Waislamu Kushirikiana kwa yale wanayokubaliana na kwa yale hatukubaliani tusilazimishane ambapo ndio chanzo cha uvunjifu wa Amani na Utulivu tulionao.

“Sheikh Jalala, Mimi siku zote utambulisho wangu ni wa Umoja wa Kiislamu, sitoweza kuwa Shia Ithnasheria nitaendelea kuwa AhlulSunna, nay eye Sheikh Jalala hawezi kuwa AhlulSunna ataendelea kuwa Shia Ithnasheriya, Jambo la Muhimu ni Umoja wa Kiislamu kama hapa tulivyokaa, Masheikh wa AhlulSunna na Masheikh wa Shia Ithnasheria na Watoto wetu tunamsheherekea Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika yale tunayokubaliana tunakuwa pamoja, tusiokubaliana tunaachana tutakutana akhera shida iko wapi?” Alisema Sheikh Alhad Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hatahivyo Nae Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe. Ali Mtulia amemtaka Sheikh Jalala kuendelea kufanya kazi za Kijamii badala ya kujikita tu katika mambo ya Dini pekee, ambapo ndio miongoni mwa kazi alizokuwa anafanya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ndio Kiigizo chetu.

“Sheikh Jalala nakushukuru sana kwa hadhara hii nzuri, nimeonana na wapigakura wangu wa Kinondoni, lakini nikuombe Sheikh Jalala,alikuwa Kiongozi wa Dola yake, lakini alikuwa anafanya Shughuli za Kijamii, akikusanya zaka, wakitoa Sadaka, wakifanya mambo ya Tiba, wakifanya Mambo ya Mahusiano, wakitoa na Ushauri, Sheikh wangu Sheikh Jalala, nakukabidhi Kata ya Kigogo uendelee kufanya Mambo ya Kijamii” Mbunge wa Mtulia


Monday, November 26, 2018

"Watu wakitambuana, Amani, Kukaa mahala Pamoja na Kusaidiana Kunakuwepo"-Maulana Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Kikao na Viongozi wa Serikali wa Kata ya Kigogo,kilichofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.ambapo Wajumbe wa Mashina, Wenyeviti na Makatibu wa Serikali ya Mitaa, Maafisa watendaji wa Mitaa, Polisi wa Kata ya Kigogo,na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata walihudhuria katika Kikao hicho.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala ameitaka Watanzania waweze Kujuana, ili Watanzania waweze kukaa kwa Amani, Kusaidiana na kukaa mahala pamoja.

“Ndugu zangu Viongozi, Watu wasiotambuana ni Vigumu kuelewana, Watu wasiotambuana ni Vigumu kusaidiana, Watu wasiotambuana ni Vigumu kukaa mahala pamoja, hivyo malengo makubwa kwa kweli ya Kikao hiki na Mwito huu, ni Kutambuana” Alisisitiza Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alitoa wito huo wakati akiongea Katika Kikao cha Pamoja na Viongozi wa Kata ya Kigogo kilichofanyika Jana Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, kikiwa na lengo kuu la Kutambuana, ambapo walihuria Wajumbe wa Mashina, Wenyeviti na Makatibu wa Serikali za Mitaa, Maafisa Watendaji wa Mitaa, Polisi wa Kata, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata.

Aidha Sheikh Jalala pia amewataka Watanzania Waislamu, Wakristo pamoja na Wapagani kuwa na Mapenzi ya Kupenda nchi yako, Mahali ulipo zaliwa kwa kufanya hivyo hutoweza kusababisha upotevu wa Utulivu na Amani pamoja na huduma mbovu kuwepo katika mji wako.

“Jambo la kupenda nchi yako, tunapozungumza habari hii ya kupenda nchi yako baadhi ya watu wasioelewa huwa hawatambui kupenda nchi yako, lakini kupenda mahali unapoishi, kupenda mahali ulipozaliwa na kupenda nchi yako maana yake ni nini? Maana yake ni kutaka make vizuri katika mji huo, ni kutaka utulivu uwepo katika mji huo,ni kutaka uchumi mzuri uwepo katika mji huo, ni kutaka maradhi yasambaratike katika mji huo,ni kutaka Ujinga usambaratike katika mji huo, ni kutaka Watu wawe na afya nzuri katika mji huo,Viongozi sisi tunaamini ya kwamba Uislamu tunaoamnini sisi ni Uislamu wa kuipenda nchi yako, wakupenda taifa lako, na ya kupenda Kigogo yako.” Alisema Sheikh Jalala

Kwa Uapnde wake Mkuu wa Kituo cha Kigogo Post  Ndugu Alex Duguza ameishukuru Jumuiya ya Waislamu T.I.C na kuitaka iendelee na kuisadia Jamii ya Kigogo na Watanzania kwa Ujumla pamoja na kuwataka Viongozi kuwalea watoto katika mafunzo ya Dini.

“Mimi niombe Msikiti huu au Jumuiya hii kwa Ujumula waendelee kusaidia, Kigogo ni yakwetu sote, tuliopo Kigogo hatakama hatuishi Kigogo, tukishafanyia kazi kigogo tayari ni kwetu, sisi ndio tutaifanya Kigogo iwe salama” alisema Duguza

“Viongozi niuwatake tuwatake watoto wetu wafuate maadili ya Dini zetu, tunaposema maadili ya dini zetu hatumaanishi kwamba kila mtu awe ni Shia Ithnasheriya Sheikh Jalala ameeleza Vizuri,hakuna dini inayosema nenda ukaue, hakuna dini inayosema mdharau baba yako, Kila Dini inahubiri Upendo, Amani, kuheshimiana, tuwaeleze jamii inayotuzunguka, jamii tunayoiongoza na watoto wetu, tuweze kuishi Maadili ya dini zetu.”

Nae Naibu Mkuu wa Hawza Imam Swadiq Sheikh Muhammad Abdu ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu ya T.I.C amewataka Viongozi kuwatambua watu wanaowaongoza katika Dini zao na kuwasisitiza wasiwe wabaguzi katika kutoa huduma kuangalia Imam ya watu wake.

“Sisi kama Viongozi jambo la kwanza tunatakiwa kuwa na Huruma na Upendo kwa wale tunaowaongoza, kwani Kila kiongozi anaongoza watu wa aina mbili ima atakuwa ni katika imani yake kama ni Mwislamu ana waislamu wenzie, kama ni Mkristo ana wakristo wenzio, na akama sio katika dini atakuwa ndugu yako katika Maumbile, yaani wewe ni binadamu nay eye ni binadamu inamaana kwamba usije kuitumia nafasi yako katika kumbagua mtu yeyote katika wale unaowaongoza” alisema Sheikh Abdu

Thursday, November 15, 2018

“Waislamu Watakiwa Kuondoa Tofauti Zao” Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala ametaka Watanzania kuacha tofuati zao za Kidini, Kimadhehebu na Kimtazamo badala yake wajikite kuwa kitu kimoja kwani ndio mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kauli hiyo aliitoa jana katika Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), matembezi amabayo yalianzia Makutano ya Morogoro Road na Kagera kuelekea Uwanja wa Pipo Kigogo, Jijini Dar es salaam.

“Matembezi haya amani mnayoyaona yaliyogubikwa na huzuni ya kumkumbuka Mtume Muhammad (s.a.w.w) iwe ni chachu kwa waislamu wa Tanzania  na waislamu wa Duniani kuacha tofauti zao walizokuwanazo , tofauti zao za Madhehebu , tofauti zao za Kifikra, na kuwa kitu kimoja kwasababu ndio usia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Sheikh Jalala 

Sheikh Jalala alisema kuwa Tanzania inahitaji Umoja wa Kitaifa ambao unasifa ya kuwaweka Watnzania wote bila kujali Dini zao, Tofauti zao, Fikra zao, kwani wenyewe unazingatia Ubinadamu kwanza.

“Kitabu hiki cha Quran kimehimiza ni chambo la Umoja wa Ktaifa, Umoja wa uwanadamu, umoja wa Watu, wanadamu wote wanahadhi moja, wanadamu wote ni kitu kimoja,dunia inahitajia umoja wa Uwadamu, wanadamu kuwa kitu kimoja,inahitajia wasia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)  aliouacha, wasia ambao unawataka watanzania wote pamoja na dini zao tofauti na mitazamo yao tofauti, na mambo yao tofauti, na ibada zao tofauti, lakini watambue wao wote ni kitu kimoja.”

Aidha Sheikh Jalala alisema kuwa swala la Umuhimu wa Kukaa Vizuri na Watu wote, Kushirikiana, na Umuhimu wa Amani ni miongoni  mwa mafundisho cha Kitabu cha Quran na Wasia alioucha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

“Kitabu hiki cha Quran kinahimiza na kuenzi jambo la umuhimu wa Kukaa vizuri, umuhimu wa Kupendana, umuhimu wa amani, Umuhimu wa mshikamano, umuhimu wa kuamini sisi wote ni ndugu na sote ni watoto wa adamu, naamini yakwamba Tanzania inauhitajia ujumbe huu.” Alisema Sheikh Jalala

Kwaupande wake Mmoja wa Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya (T.I.C) Taifa Mhe.Ramadhani Athumani Lisu amesema kuwa Watanzania wanahitaji malenzi na Muongozo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Nyanja zote katika maisha ya kila siku.

“Tanzania pamoja na Dunia kwa ujumla inahitajia Malezi na Muongozo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika nyanja zote kama Nyanja za elimu, Uchumi, Siasa, afya na Kilimo pamoja na Mahusiano mema ya kiinchi.” Mh.Lisu alisema

Hatahivyo Mh. Lisu alitoa wito kwa watanzania kuwa na imani pamoja na kuitenda kimatendo kuwa Binadamu wote ni sawa na tunatakiwa kudhaminiana kama binadamu wote ni sawa.

"Wito wetu kwa watanzania na Dunia kwa Ujumla kuwa wanadamu wote tudhaminiane, na tuzingatie mafunzo na maelekezo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambayo inakwnda pamoja na umuhimu wa Amani kwa watu wote."

Wednesday, August 8, 2018

“Kukua kwa Uchumi na Biashara msingi wake ni Amani na Utulivu” Maulana Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa kama watazania wanataka kuwa na Uchumi wa Kati na kuhakikisha Biashara zinafanyika ni lazima watanzania wahakikishe kuwa na Amani na Utulivu katika nchi yao.
Maulana Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam, ikiwa ni katika kutoa Ujumbe kwa Wahujaji Watarajiwa na kwa Watanzania kwa Ujumla, Ujumbe ukiwa ni  Hijja ni Mkusanyiko wa Kuienzi Amani na Maelewano.
“Sisi watazania na wasiokuwa watanzania kama tunataka Biashara zetu ziboreke , lazima tuwe na Utulivu, lazima tuwe na amani, kama tunataka Tanzania iwe Tanzania ya Viwanda haiwezekani kuwa ya viwanda lazima Tanzania hii iwe na amani, kama tunataka Tanzania ipigiwe mfano kwa uchumi wa kati kwa uchumi Mkubwa hilo haliwezekani mpaka tuweze kuiboresha amani na utulivu.” Alisema Maulana Sheikh Jalala.
Aidha Maulana Sheikh Jalala Amesema kuwa moja ya mafunzo yanayopatika kwa kuwa na Nabii Ibrahimu  ambae anakubaliwa na watu wote wenye dini tofauti, Fikra tofauti na Madhehebu tofauti ni Jambo la Kuvumilana kati ya dini zote.
“Hijja ni Ibada ya kuenzi Amani na alietangaza ni Mtume Ibrahim (a.s) anaekubalika na Dini zote, kwanini awe ni yeye mtangazaji? Moja ni kitu muhimu sana cha kutambua ni kitu cha kuvumiliana, kana kwamba Mungu alitaka Walimwengu watatofautiana kifikra, Kirai,Kimtazamo, Kimadhehebu na Kidini, lakini akawataka hawa wawe na Nabii mmoja Ibrahimu ambae ni Nabii wa hawo watu wote Mnamkubali, wajifunze kitu kinachoitwa Kuvumiliana katika Dini” Alisisitiza Maulana Sheikh Jalala
“Kwahivyo Falsafa ya Hijja aliyoitangaza Nabii Ibrahimu (a.s) moja yake ilikuwa ni amani, utulivu na kuenzi hali hali ya utulivu, uwe ni utulivu wa Kiroho au uwe ni utulivu wa Kifikra, ambayo hii ni utulivu wa aina ya Pili,” Alisema Maulana Sheikh Jalala
Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala ameeleza baadhi ya Viashiria vya Ufunjifu wa Utulivu na  Amani katika Jamii ikiwa ni pamoja na matukio ya Ubakaji, Matumizi mabya ya Pesa za Umma, wizi,Makosa ya Jinai, Mauaji, Unyanyasaji na Wanaofanya Biashara ya Kuuza Miili yao.

“Jamii yoyote inayowafanyakazi yanaohujumu mali ya Umma, Jamii yoyote ambayo ina wezi, Jamii yoyote ambayo Kubaka ni kitu cha kawaida, Jamii ambayo ndani yake kuna mauaji, kuna ukatili, kuna kuchinjana, Jamii yoyote ambayo biashra ya Madawa ya Kulevya ni jambo la kawaida, Jamii ambayo inamakosa ya Jinai, ijue jamii hiyo ni jamii ya watu wasio kuwa na Utulivu na amani”.Alisema Maulana Sheikh Jalala

Sunday, June 17, 2018

"Mwezi wa Ramadhani ni Mwezi unaotufunza Kutii Sheria na Kanuni" Maulana Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiotoa Khutba ya Swala ya Eid Fitri, inayozungumzia Mwezi wa Ramadhani inatufunza Kutii Sheria na Kanuni, katika Viwanja Pipo Kigogo Jijini Dar es salaam
KIONGOZI  Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala, amesema mwezi Mtukufu wa Ramadhani  unafundisha kutii sheria na kufuata kanuni na taratibu za nchi.
Pia ni madrasa na chuo cha kujifunza na kuacha yale ambayo jamii inayachukia na kila mtu kuwa mtiifu.
Kauli hiyo, ilitolewa jana Dar es Salaam na kiongozi huyo, wakati wa swala ya Idd el Fitr na kupeana mkono wa Eid mubaraka katika viwanja vya pipo vilivyoko Kigogo.
Sheikh Jalala, alisema kufunga ni ngome na kuangalia mambo ambayo ni haramu ikiwemo kufanya usikivu na kuacha maovu.
‘’ Mwezi mtukufu wa ramadhani ni kutii sheria na kanuni ikiwemo kuacha kunywa pombe na kuacha mambo ambayo ni haramu ambayo yanaumiza muumini,’’alisema.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari punde baada ya Kuhitimisha Swala ya Eid Fitri iliyoswaliwa katika Viwanja Pipo Kigogo Jijini Dar es salaam
Alisema Mwenyezi Mungu amelazimisha kuswali lakini ukiangalia swala tano ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani sawabu zake na malipo yake sio kama siku nyingine.
‘’ Mwezi mtukufu wa ramadhani sawabu zake ni tofauti na siku za kawaida, kwani ni chuo kinachowatoa wanafunzi ambao masomo yao ni kutii sheria kanuni,’’alisema.
Vile vile Sheikh Jalala alisema jamii ili iwe na maendeleo ni wajibu wa kila mtu kutii sheria na kanuni kwani bila kufanya hivyo nchi yoyote haiwezi kuwa na maendeleo.
‘’ Tukitii sheria na taratibu za nchi hata vituo vya polisi vitapungua, mahakama ndogo ndogo hazitakuwepo ambapo amani itakuwa imetawala katika majumba yetu na katika jamii zetu, hiyo ndio siri ya maendeleo katika jamii yoyote,’’alisema.

Pia alisema ni wajibu wa kila mmoja kumuomba Mwenyezi Mungu amani na  utulivu ulioko uzidi kuboreshwa na yeyote ambaye anataka amani iliyoko kuipoteza Mwenyezi Mungu amsambaratishe kabla hajakanyaga ardhi hii.
Alitoa ombi kwa jamii kuwa maelewano ambayo yalionyeshwa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani uendelee kudumu bila ya ubaguzi wa dini yoyote wala ukabila.
Kwa upande wa mmoja wa wanakamati mahsusi wa Jumuia ya dhehebu la Shia Ithnasheria nchini, Sheikh Mulaba Swaleh, alisema siku ya Idd el Fitri ni siku tukufu na  takatifu kwani waislamu wote wamemaliza mfungo huu.
 Alisema waislamu walikuwa katika kipindi cha kujifunza namna ya kumcha Mwenyezi Mungu kwani anawataka kila mmoja kutii sheria kuweza kuwa waadilifu.
‘’ Neno uadilifu ni neon ambalo linahusu mambo yote ya kijamii na kiserikali ambapo mwanadamu anatakiwa kuweka kitu mahala pake ambapo panastahili hivyo sote tujifunze uadilifu,’’alisema.