Saturday, February 9, 2019

Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) yafanya Kikao kwa mara ya Kwanza | 09.02.2019


Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya  Tanzania (T.I.C), Kikiongozwa na Mwenyekiti bodi hiyo Dr. Muhammad Kanju (wakwanza), leo wamefanya Kikao chao cha kwanza baada ya kumalizika Uchaguzi, uliofanyika mwaka Jana, kikao hicho kimefanyika Makao makuu ya Jumuiya hiyo, Kigogo Post Dar es salaam.



Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdu (kulia) akiwa makini kusikiliza baadhi ya nukta muhimu zinazojaliwa katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikhat Pili Muhammed akijumuika pamoja na baadhi ya wajumbe wenzake katika kikao hicho.
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Abdallah Seif (wapili kulia) ambae pia ni Mjumbe wa bodi ya Wadhani akishiriki pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini katika kikoa hicho.
Mhe. Hoza Maliki (kulia) akiwa pamoja na Mjumbe mwenzake wa bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) wakijumuika pamoja katika kikao leo Makao makuu ya Jumuiya, Kigogo Post Dar es salaam
Sheikh Ghawth Nyambwa Mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Akichangia maoni katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikh Ramadhani Mwelekwa (wapili kushoto) akishiriki katika kikao cha Bodi ya Wadhanimi.

Kikao cha Kamati Tendaji cha Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Taifa | 08.02.2019


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) wakiwa Makini kusikiliza Muhutasari wa Kikoa kilichopita, ukisomwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hii Mhe. Bashiru Nyello, kikao hicho kilifanyika Jana, Makao Mkuu ya Jumuiya hiyo Kigogo Post Dar es salaam.



Katibu wa Elimu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Taifa, Sheikh Muhammed Juma akinukuu baadhi ya Nukta Muhimu katika Kikao cha Kamati Tendaji Taifa.



Makamu Mwenyekiti wa Jumauiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Taifa Sheikh Ramadhani Mwelekwa, akijumuika pamoja katika kikao cha Kamati Tendaji Taifa

Afisa Mtendaji wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Taifa Mhe. Meja Kibido akiwa makini katika kunukuu nukta Muhimu zainazojadiliwa katika Kikao cha Kamati Tendaji Taifa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Mhe. Bashiru Nyello (kulia) akisoma Muhutasari wa Kikao kilichopita, katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Taifa Sheikh Issa Rwechungura.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Taifa, Sheikhat Fatuma Mwiru (kushoto), Sheikh Ramadhani Nkusui (Kulia) wakisiliza kwa umakini yanayoendelea katika kikao.
Katibu wa Uchumi Taifa wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Mhe. Muhammed Zahoor, akinukuu nukta Muhimu katika Kikao cha kamati tendaji cha jumuiya taifa.
Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Mhe. Abdulkarim Shamte akihudhuria kikao cha kamati tendaji tiafa.

Wednesday, February 6, 2019

“Watanzania Msikubali Madola ya Kigeni kuingilia Siasa za Ndani” Balozi wa Iran.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchi Tanzania Mhe. Mussa Farhang akiongea katika Semina ya kuelekea Maadjimisho ya Miaka 40 ya Serikali ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, iliyofanyika Jana katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini Jijini Dar es salaam, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini Mhe. Abbas Farhand.

Na: Twalha Ndiholeye
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mussa Farhang amewataka Wananchi wa Tanzania hususani Wasomi, Wanachuo na Wananasiasa  kutokuruhusu uingiliaji wa Siasa za Madola ya Kigeni katika siasa ya ndani ya nchi na kuwataka wasiwe tegemezi ili kuenzi Uhuru na Amani uliopo.

“Wananchi wa Tanzania, Jamii ya Wasomi, Wanachuo na Wanasiasa wasiruhusu kabisa ule uingiliaji wa siasa wa Madola ya Kigeni katika siasa za ndani,tusiwe tegemezi kwani Uhuru wetu hautakuwa na faida yoyote, dhamani yoyote na nguvu yoyote” alisema Balozi Farhang.
Balozi wa Iran Mhe. Farhang alisema hayo jana katika Semina ya kuelekea maadhimisho ya Miaka 40 ya Serikali ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, iliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar es salaam.

Aidha Balozi Mhe.Farhang amewataka Watanzania kuenzi Fikra za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Imam Khomein katika kuheshimu Sheria ambapo ndio chanzo cha utekelezaji wa maendeleo na udumishaji wa Amani na maelewano uliokusudiwa na waasisi wa nchi.

“Tufate zile fikra za Viongozi wetu waasisi wa Mataifa yetu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na Imam Khomein, lakini wenye Umuhimu sana kwa wananchi wa Tanzania kufuata na kuenzi fikra za Mwl.Nyerere, Ufuataji wa Sheria ni kitu ambacho lazima iheshimiwe kwani ndio chanzo cha maendeleo, Tusaidie Tanzania na Irani ziweze kuendelea kufuata mfumo wa Sheria.”.aliongeza Balozi.

Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanyika mwaka wa 1979, yakiongozwa na Kiongozi wa Kiongozi wa Kidini ajulikanae kwa jina la Imam Khomein ambae alifaniliwa kumuondoa Mfalme Shaah amabe alikuwa Kiongozi wa nchi ya Iran kipindi hicho.




Saturday, January 26, 2019

Serikali na Watanzania watakiwa Kuwa na Mfumo wa Malezi kukabili Swala la Usafi | Sheikh Kasonso

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso wa akitoa Khutba leo Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, huku akizungumzaiUsafi ni katika Imani ya Dini Tukufu ya Uislamu 

Na: Twalha Ndiholeye
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso ameitaka Serikali pamoja na Watanzania kama kweli wanania ya kuhakikisha Miji na chi kwa Ujumla kuwa katika hali ya Usafi ni lazima kujizatiti katika swala zima la Kuwalea Watanzania na watanzania kulea watoto wao katika swala zima la kupenda Usafi.

“Ili sisi tuweze kuwa wasafi katika Majiji yetu na Miji yetu, kitu cha kwanza cha kuangalia ni jambo la Malezi, leo unawza kumkuta Mtu mzima anakula ndizi barabarani kasha anatupa ganda ovyo, hii inamaanisha kwamba hivyo ndivyo alivyolelewa” Amewataka Sheikh Kasonso.

Sheikh Kasonso ametoa wito huo leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, imeyoswaliwa Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam alipokuwa anazungumzai Usafi ni katika Imani ya Dini Tukufu ya Uislamu.

Aidha Sheikh Kasonso amesema kuwa Swala la Malezi huwa inakuwa Tabia, tabia huwa inarithiwa na tabia huwa inaigwa hivyo lazima ianze harakati ya kuwalea watoto wetu kuanzia Majumbani mwetu na Shuleni ili kuweza kusaidia upatikanaji wa Usafi katika maeneo yetu.

“Mfumo wa Kimalezi tabia huwa inakuwa na tabia huwa inaritihishwa na tabia huwa inaigwa, hata sisi hapa tukitaka Dar es salaam yetu iwe safi na miji yetu kuwa safi nan chi yetu ya Tanzania iwe safi, ipendeze, ing’are kila kona ni lazima tuanze kuwalea watoto Majumbani mwetu, Mashuleni, tukiwalea itakuwa kama vile tunavyosifia Bara la Ulaya” Amesema Sheikh Kasonso.

Hatahivyo Sheikh Kasonso amewataka Watanzania na Serikali kuwa wasidhani tabia ya Usafi walionazo Bara la Ulaya na Majirani zetu kuwa ni swala limetokea wamejikuta wanalo sio hivyo bali ni swala la Mfumo wa Malezi walivyojilea katika swala la Usafi.

“Bara la Ulaya leo hii huwezi ukakuta hata chupa ya Maji taka iko barabarani au huweziukakuta chupa ya maji imetupwa barabarani bahati mbaya hapana, yale usifikiri yametokea kibahatimbaya hapana, bali ni Mfumo wa Malezi waliolelewa wenzetu, kwahiyo hata mtoto tayari anajua afanye nini, hata mkubwa amekuwa katika mazingira kama yale” Amesema Sheikh Kasonso.


Waislam AhlulSunna Waungane na Waislamu Shia Ithnasheriya ili kudumisha Umoja | Maulana Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiotoa Khutba ya Swala ya Ijumaa, leo Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam, akizungumzia Je, Usuni na Uwahabi ni kitu Kimoja?

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania  Maulana Sheikh Hemed Jalala amewataka Masheikh na wanazuoni wa Ahlul Sunna Dar es salaam na Tanzania nzima kuungana na Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania ili waendee kuwa wamoja na kuweza kumshinda Adui anaofanya kazi ya kuwagawa.

 “Enyi Ndugu zangu, Wasomi, Masheikh na Wanazuoni wa AhlulSunna Tanzania kuweni macho, Waislamu Shia Ithnasheriya ndio wenzenu, na Mkitaka Usuni uwendelee, ninawaambia Masheikh wa Ahlul Sunna wa Dar es salaam na Tanzania nzima waungane na Mashia Ithnasheriya ndio ndugu zao na wabaki pamoja, na wakitaka wamshinde adui wa Usuni wawe pamoja na Mashia Ithnasheriya” Amewataka Maulana Sheikh Jalala.

Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema hayo leo Khutba ya Swala ya Ijumaa, imeyoswaliwa wiki iliyopita, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam, ambapo katika khutba hiyo alizungumzia Je, Usuni na Uwahabi ni Kitu Kimoja?.

Aidha Maulana Sheikh Jalala amewatahadharisha Wasoni, Masheikh na Wanazuoni wa Kiahalul Sunna kuwa macho na gurupu linalofanya kazi ya kuwagawa AhlulSunna na Shia Ithnasheriya kwa kutofuata maelekezo yao ambayo inaonekana ndio chanzo cha Matatizo mengi katika jamii ya Kiislamu.

“Nataka niwaeleze Ndugu zangu, Wasomi na Wanazuoni wa Ahlul Sunna katika nchi hii wakae wakitambua kwamba hilo gurupu linalowaambia Waislamu Shia Ithnasheriya sio wenzenu, msiwaalike kwenye Maulid zenu, msishirikiane nao, msiende kwenye misikiti yao, hao ndio sio wenzenu katika Ahlulsunna, na hao ndio waliowaletea matatizo mengi” Maulana Sheikh Jalala amesema

Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala amewatoa hofu Watanzania kwa kusema kuwa Dini tukufu ya Uislamu asili unalingania watu kuwa wamoja, kupendana na kutokuunga mifarakano yoyote ambayo itapekekea migogoro yoyote katika jamii ya Kiislamu.

 “Watanzania Mungu amewaletea Uislamu ambao hauwagawi watu, unawatakeni muwe kitu kimoja, unawatakeni mpendane, vipi linakuja gurupu linaanza kuwagaweni huyu ni Shia Ithnasheriya na huyu ni Ahlul Sunna?,huyu ni Ibaadhi huyu ni Ghawarij?, mbona sivyo Uislamu ulivyo?,?” Amesisitiza Maulana Sheikh Jalala


Saturday, January 19, 2019

Waislamu watakiwa Kuitukuza na Kuienzi Qur’an | Sheikh Kasonso.

Khatbu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso akitoa Khutba Jana katika Masjis Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, akizungumzia Kuitukuza Qur'an.

Khtabu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso amewataka Waislamu kuipa kipaumbele kitabu Kitufu cha Qur’an katika kukitunza, kukienzi na kufuata yaliyomo ndani ya Qur’an ili kuweza kupata mahitajio yote ya mwanadamu katika Nyanja zote katika Maisha ya Kila Siku.

Sheikh Kasonso alisema hayo jana katika Khutba ya Swala ya Ijumaa , iliswaliwa Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, katika Khutba yake akizungumzaia Utukufu na Ubora wa Quran tukufu.

“Sisi leo hii Waislamu tujiulize, Qur’an tunaitetemekea katika unyenyekevu na ule kuitukuza Qur’an je tunacho?, na kitendo cha kuienzi na kuyafuata yaliyomo ndani ya Qur’an tunayo? Huku ndiko kunyeyekea kunakotakikana” Alisema Sheikh Kasonso.

Aidha Sheikh Kasonso alionyesha hali ya kusikitisha kwa kuwa hali ya Waislamu wanaishi kinyume na mafundisho ya Kitabu chao kitukufu cha Qur’an na kufanya kila wanaloweza bila ya kuwa na chembe ya Hofu ya kuiogopa Qur’an.

 “Leo hii tunatembea Vingine na Qur’an yetu inatuambia vingine, Kila jambo katika Ulimwengu huu tunalipeleka vile ambavyo tunaona sisi liko sawa, lakini si vile Qur’an inataka, hii ni dalili yakwamba sisi sio wenyenyekevu, sisi hatuheshimu Qur’an, hatuiogopi Qur’an” alisisitiza Sheikh Kasonso.

Hatahivyo, Sheikh Kasonso amewataka wazazi kuweza kuthamini Kitabu kitufu cha Qur’an na kutokilinganisha na Vitabu vingine ambapo baadhi ya wazazi wameonekana wako tayari kumnunulia Daftari mtoto wake kuliko kumnunulia kitabu kitufu cha Qur’an.

“Leo hii mzazi hataile thamani ya kumnunulia mwanae Juzu la Tsh.300/= ni mtihani Mkubwa, angalie Qur’an inavyodhalilika, lakini aende akanunue daftari, atanunua hata Daftari 15 hadi 20, ikiwa Juzu Mzazi yuko tayari mwanae aende hivyohivyo, hii ni dalili Qur’an haidhaminiwi” Sheikh Kasonso alionyesha huzuni.

Friday, January 18, 2019

Waislamu watakiwa kuwa Wamoja katika Amani- Maulana Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislamu wa Tanzania kuienzi amani, Umoja kwa kuacha tofauti ya Mitazamo yao pamoja na kujitenga na makundi yenye lengo la kuondoa Umoja na Mshikamano baina ya Waislamu na Watanzania.

Maulana Sheikh Jalala amesema hayo leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita, iliyoswaliwa Masjid Ghadir, Kigogo Post, Jijini Dar es salaam, huku akizungumzia Je, Uwahabi na Usuni ni Kitu Kimoja?.

“Katika zama hizi ni zama ambazo Waislamu wanahitajia kuwa kitu kimoja,kama kuna kipindi Waislamu wanatakikana waache tofauti zao,na mitizamo zao ni zama tulizokuwa nazo, ni zama ambayo Umoja, kuwa kitu kimoja, kuzungumza pamoja, kukaa meza moja, ni zama muhimu mno” Alisema Maulana Sheikh Jalala.


Aidha Maulana Sheikh Jalala anawakumbusha Waislamu wa Tazania kuwa asili ya Watanzania hata kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru wameleleka katika Umoja, kupendana, kushirikiana, kuelewana, kusaidiana bali hawakuleleka katika kubaguana na kukufurishana.

 “Watanzania wameleleka kwenye Umoja, kupendana, kuelewana, kushirikiana, watanzania hawajaleleka kwenye kubaguana na kuchukiana Waislamu wa Tanzania Ahlul Sunna, Shia Ithnasheriya na Ibaadhi katika nchi hii walikuwa kitu kimoja hata kabla ya Uhuru wa nchi hii,na wala hawakujua kubaguana, wala kukufurishana” alisisitiza Maulana Sheikh Jalala


Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala amewatahadharisha Waislamu na Watanzania kujitenga na makundi yote likiwemo kundi la Kiwahabi yenye malengo mabaya ya kuichafua Tanzania inayosifika nchi ya Amani na Maelewano.

“Malengo la kundi hilo la Kiwahabi ni kutaka kuwagawa na kuwataka kuwafanya kuwa ni makundi tofauti ambayo mwisho wa yote ni kugombana na kuifanya Tanzania sio mahala pa amani, maelewano na mshikamano”aliongeza Maulana Sheikh Jalala