Friday, January 16, 2015

"Kitendo cha Jarida La Charlie Hebdo kumdhalilisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kitendo cha Kifedhuli”.



Harakati ya hawza Imam Swadiq chini ya Uongozi wa Samahat Sheikh Hemedi Jalala inaungana na Waislamu wote duniani na Wapenzi wa Amani kokote walipo kupinga kwa Kauli thabiti hatua zozote zinazochukulia na Serikali za nchi za Magharibi na Marekani kuchochea vitendo venye lengo la kuamsha chuki na machafuko ya Kidini ulimwenguni.


Jalala alisema kitendo cha kumtusi Muhammad (s.a.w.w) ni Kashfa na Matusi ya wazi kwa Mtume wetu Kipenzi chetu Muhammad (s.a.w.w) Waislamu wote bali na wapenda Amani duniani kote. Ni kitendo kisichovumilika na hakuna Musialmu aweze kustahamili ghadhabu zake kwa kitendo hichi.

Kauli hivyo imetolewa baada tu ya Jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris nchini Ufaransa Charlie Hebdo lilisema katika toleo lake la hapo kesho siku ya Jumatano(14/01/2015) litachapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wa mbele, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote”.
Aidha alisema kuwa vitendo hivi vinafanywa na makundi ya Watu waovu, Wasio na Imani ya Dini wala Ubinaadamu, wanaopata kinga ya kulindwa na ufadhili wa Idara za Kijasusi za Mataifa na dola za Magharibi kwa lengo lao ovu la kutaka kuupaka Matope Uislamu na Waislamu duniani.
Samahat Sheikh.Hemed Jalala.




 “Kuheshimu Imani, Mila, Tamaduni na Matukufu ya Imani za Dini tofauti tofauti ni kanuni ya Msingi ya Umoja wa Kimataifa, tunawataka wakuu wa Dola za Magharibi na Amerika kuwa Vinara kuziheshimu na kutekeleza kwa vitendo kanuni na Haki hizi”alisisitiza Jalala. 

Alisema kuwa Maamuzi yasio ya Upendeleo wa kiimani na yenye Maslahi sawa kwa raia wa Imani tofauti tofauti wa Mataifa yao. Kwani ni kwa Maamuzi wanayoyafanya yenye upendeleo wa Makusudi kwa Upande mmoja wa Imani ya Dini na kukandamiza upande mwingine ndio chanzo cha kuzuka makundi yenye misimamo mikali na yenye mikakati ya kulipiza kisasi na kufanya vitendo vya Kigaidi. 

“Wanatumia gharama kubwa kukandamiza maandamano ya Amani yanayoitishwa katika nchi zao kulaani Vitendo viovu na vya kigaidi vinavyofanywa na Taifa ghasibu la Israel? Sambamba na hili tunaungana na Ulimwengu mzima kupinga Vitendo vyovyote vya kigaidi vinavyofanyika duniani kote dhidi ya Nchi na au binaadamu yeyote asiye na hatia”alisema Jalala.

Jalala aliongeza kuwa Hakuna uhuru usio na Mipaka, Matumizi mabaya ya Vyombo vya habari na Mawasiliano, Imani na Misimamo inayokiuka mipaka ya Dini na Sheria za Nchi, Mauaji na Udhalilishaji wa Viongozi wenye kuheshimiwa wa Dini na Nchi, Kukashifu na Kutakana Matukufu ya Dini na uvunjaji wa Alama za dini zinazoheshiwa na waumini wa Dini hizo, ni Vitendo Viovu.

Sunday, January 11, 2015

Grace Mugabe aziacha familia 200 bila ya makazi



Bi Grace Mugabe mke wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametumbukia katika sakata la ardhi baada ya kuzihamisha kwa nguvu familia zaidi ya 200 katika makazi yao bila ya kuzipatia makazi mbadala. 

Grace Mugabe aliwaamuru maafisa polisi waliokuwa wamejizatiti kwa silaha, kuziondowa kwa nguvu familia hizo katika eneo lao la mashamba ya Anold wilayani Mazowe mashariki mwa Harare mji mkuu wa Zimbabwe bila ya kuwapatia sehemu nyingine ya kuishi katika kipindi hiki ambapo mvua nyingi zinaonyesha.

Mkulima mmoja ambaye hakutaka kujulikana alisema kuwa baada ya polisi kufikia katika mashamba yao, waliharibu nyumba zao na kusema kuwa wanaondolewa hapo ili kutoa fursa kwa Grace Mugabe ya kujenga bustani ya michezo. 

Baadhi ya familia hizo zimenukuliwa zikilalamika kwamba, wameamriwa kuondoka katika makazi yao hayo hata hivyo bila ya serikali kuwapatia eneo jingine la kuishi. 

Wakati huo huo Taasisi ya Mawakili wa Haki za Binadamu ya Zimbabwe imetuma timu ya wanasheria huko Mazowe ili kusitisha zoezi la kuzifukuza familia zilizokuwa zikiishi hapo.

Saturday, January 10, 2015

Vijana Mtukuzeni Mtume (s.a.w.w)

Watatu kulia ni Sheikh Hemed Jalala mwalim Mkuu wa Hawza Imam Jafar Swadiq akiwa katika sherehe za mazazi ya Mtume Muhsmmad (s.a.w.w), kigogo-post Dar es salaam.Mtume Muhammad(s.a.w.w) alizaliwa tarehe  17 mwezi wa Rabiiul awwal(Mfungo Sita), mwaka  wa tembo sawa na mwaka  570 H.D

HABARI KAMILI

Sheikh Mkuu wa Tanzania Ithna Ashariyyah Abdallah Seif amewataka vijana kuto rudi nyuma katika kumsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
 
Seif alisema maadui wa Maulid hawajui radha na faida ya kukumbuka mazazi ya mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Wapili Kushoto ni SheikhAbdallah Seif


Hayo alisema jana katika sherehe ya kukumbuka mazazi ya Mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w), mskitini Ghadir, Kigogo-Post, Dar es salaam.


Ameongeza kuwa Waumini wanatakiwa kuwa na moyo wa kuvumiliana baina yao kwani Mtume (s.a.w.w) alikuja duniani kwa ajili ya kuwa rehema kwa viumbe vyote.


Kwa uapnde wake Sheikh Abdullatwif Issa Swalehe wa Hawza Imam Jafar amewataka Waislam kujikita katika utafutaji wa Elimu, ili waweze kumtetea Mtume kwa usahihi


Sherehe hizo zimeandaliwa na Hauza Imam Jafar Swadiq, chini ya Sheikh Hemed Jalala, iliyopo kigogo-Post,jijini Dar es salaam.

Mtume Muhammad(s.a.w.w) alizaliwa tarehe  17 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka  wa tembo sawa na mwaka  570 H.D.


Baba yake ni Abdallah ibn Abdul mutwalib bin hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim  (A.S) Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin zuhra bin kilaab. Alizaliwa katika mji wa makkatul  mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.



Waumini wa Kiume wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la shia, wakiwa makini kusikiliza historia na sifa za mtume Muhammad (s.a.w.w) pindi alipozaliwa na kazi alizofanya kwa walimwengu wote.

Wanafunzi wa Hauza Imam Jafar Swadiq, wakiimba Qaswida za Kumsifu Mbora wa Viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Sherehe za Kuzaliwa Mtume (s.a.w.w)


Watatu kulia ni Sheikh Hemed Jalala mwalim Mkuu wa Hawza Imam Jafar Swadiq akiwa katika sherehe za mazazi ya Mtume Muhsmmad (s.a.w.w), kigogo-post Dar es salaam.Mtume Muhammad(s.a.w.w) alizaliwa tarehe  17 mwezi wa Rabiiul awwal(Mfungo Sita), mwaka  wa tembo sawa na mwaka  570 H.D



Wakwanza kulia ni Naibu Imam wa Msikti wa Ghadir kigogo-post, Sheikh Ghauth Nyambwa, akiperuzi data kwa maandalizi ya kuzungumza mbele ya waumini juu ya sherehe za mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)


Waumini wa Kiume wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la shia, wakiwa makini kusikiliza historia na sifa za mtume Muhammad (s.a.w.w) pindi alipozaliwa na kazi alizofanya kwa walimwengu wote.

Wanafunzi wa Hauza Imam Jafar Swadiq, wakiimba Qaswida za Kumsifu Mbora wa Viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w).


Waumini wa Kike wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la shia, wakiwa makini kusikiliza historia na sifa za mtume Muhammad (s.a.w.w) pindi alipozaliwa na kazi alizofanya kwa walimwengu wote.

Sunday, December 21, 2014

UMIHIMU WA KUKUMBUKA KIFO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)


Viongozi mbalimbali kutoka Hawza Imam Jafar Swadiq chini ya Sheikh Hemed Jalala na Kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania Sayyed  Arif wakiongoza matembezi ya amani.

Tukio la kufishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) mbele ya jamii ni jambo geni sana, kana kwamba katika historia ya ulimwengu tukio hili halikutokea. Ingawa tukio la kuzaliwa kwa Mtume Muhammad limepokelewa kwa nafasi kubwa isiyo kifani.

Kwa hiyo, unaweza kuona hafla mbalimbali za kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zikifanywa Misikitini, Madrasani, Majumbani, na katika Mazawia mbalimbali.

Hili ni jambo jema sana, swali liliopo hapa ni, je, huyu afanyiwae haya yu hai mpaka sasa? Au amekwisha kufa? Ni kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) amekwisha kufa.

Ndio maana katika mwezi huu wa Safar Waislam katika maeneo mbalimbali duniani wamo katika huzuni na simanzi kubwa ya kukumbuka tukio la kufariki dunia Mtume wa rehema, Muhammad (s.a.w.w).

Hapa Tanzania Uongozi wa Chuo Cha Imamu Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala Unaadhimisha Maadhimisho ya Kumbukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ambaye alifariki dunia tarehe 28 Safar mwaka wa 11 Hijria katika mji mtakatifu wa Madina.

Uongozi Huo Unawataka Waislam Wote kuungana Pamoja katika kukumbuka kifo cha mbora wa daraja bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), ili kusadia kuishughulisha jamii ya kiislam katika kukuza maadili na mafundisho sahihi aliyofundisha Mtume Muhammad.

Katika kukumbuka kifo cha mtume uongozi umeandaa Matembezi ya Amani ambayo  yataanzia Karibu na Msikiti wa Kichangani, Magomeni Kichangani Hadi Viwanja Vya Pipo kilichopo Kigogo-Post Jijini Dar es salaam.Yakiwa na Ujumbe “Mtume katuachia Vizito Viwili Tushikamanenavyo”.

Uongozi unawataka Masheikh na Walimu kuihamasisha jamii ya kiislamu kukumbuka matukio muhimu yaliyotokea, ili kuimarisha umoja na mshikamano baina ya waislam na wasiokuwa waislam katika kuishi kwa amani na maelewano.

Pia tunawataka Waislamu wote kufuata mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlulbayt (Watu maalum wa Nyumba ya Mtume) , ili tuweze kufikisha ujumbe sahihi aliotuachia, katika kukuza dini na ushirikiano baina ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu.