Monday, March 2, 2015

Sheikh Jalala "Uislam wa Mtume ni Waamani."


Sheikh Hemed Jalala,akisisitiza jambo juu ya Uislam Sahihi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu kilichopo Kigogo-Post, jijini Dar es Salaam amewataka Waislamu kufuatilia Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa Makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali kutoka kwa Wahadhiri.
Hayo ameyasema katika Mhadhara wa Wazi uliokuwa wa siku tatu kuanzia 28, februal, hadi 01-machi 2015, katika viwanja vya Super Sanifu, Round About ya Kigogo, Dar-es -salaam.

Amesema kuwa Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni uislamu wa Amani, kuvumiliana, kupendana, kuheshimiana, kutokukufurishana ,kutodharau dini ya mwenzio na Wenyekukaa Pamoja na watu wenye mtazamo tofauti.


 Aidha ameongeza kuwa Uislamu wa Mtume ni wa amani, huruma na maelewano na kuwa Uislamu halisi utashinda Uislam wa chinja chinja utafeli kwa kuwa unaenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s).



Hatahivyo amewataka watu wote bila kujali dini zao kushikamana na kusikilizana kwani jamii ambayo aina maelewano itakuwa ipo mbali na maendeleo, taifa ambalo linapata maendeleo ni taifa lenye maelewano na mshikamano.

Katika Muhadhara huo uliyomalizika siku ya J.pili ya tarehe 1/03/2015 kulitolewa vitabu mbalimbali vinavyoonesha athari mbaya ya Madhehebu ya Kiwahhabi (ANSWARU SUNNA) Madhehebu ambayo hii leo yamekuwa tishio kubwa kwa jamii ya Kiislamu Ulimwenguni.

Hawzat Imam Swadiq (a.s) Yahimiza Hijab kwa Bint wa Kiislam.

Waschana wenye umri kati ya Miaka 9 hadi 15 wakisoma Duatul Huja baada ya Kupewa mafunzo ya Dini Kiislam, kwa Mnasaba wa kuzaliwa Bibi Zayanab Bint Ali (a.s).

Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala akiwaswaisha kwa Vitendo waschana waliohudhuria katika kusherekea kuzaliwa kwa Bibi Zaynab Bint Ali.
Hawazat Imam Swadiq imesheherekea mazazi ya Bibi Zaynab Bint Ali (a.s)  kwa kuwachukua wasichana 50 wenye umri wa miaka kuanzia 9 hadi 15, pamoja na wazazi wao kwa kuwapatia elimu na mafunzo juu ya Unuhimu wa Hijabu, Swala na sheria zingine za Kiisalamu.

Katika Mafunzo hayo, Samahat Sheikh Hemed Jalala aliwasalisha swala ya jamaa kwa vitendo na kuwataka waschana hao waishi kwa misingi ya Kiislamu,na Wapambike na hijjab kama walivyokuwa Fatma Bint Muhammad (s.a.w.w) na Zaynab Bint Ali (a.s)

Bibi Zainabu Baba yake ni Sayyedina Ali  Ibn Abutwalib (a.s), Mama Yake ni Fatuma Bint Muhammad, Babu yake ni Muhammad Ibn Abdallah na Bibi yake ni Khadija Bint Khuwailid


Sheikh Hemed Jalala akiwapa neno la umuhimu wa Hijab na Ibada zingine kwa bint wa Kiislam.

Waschana wakiwa pamoja na wazazi wao wakiwa makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali

Waschana wa Kiislam wanatakiwa kupambika kwa kuvaa Stara,Ibada, Elimu na Tabia Njema kama alivyokuwa Bibi Zaynab Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Sunday, March 1, 2015

Hawzat Imam Swadiq (a.s), yafanya Mhadhara wa Wazi

Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa makini katika kusikiliza Wahubiri wa Mhadhara siku ya kwanza.Mhadhara huo ukiwa na ujumbe wa "Uislam ni Dini ya Amani" uliofanyika katika Viwanja vya Round About ya Kigogo, Viwanja vya Super Sanif.



Waumini wa Kike wakiwa makini katika kuandika nukta muhim za Wahubiri wanavyosema.

Vijana mbalimbali wa dini ya kiislamu wakiwa katika ufatiliaji wa mada mbalimbali zinazowasilishwa na masheikh mbalimbali kutoka Hawzat Imam Swadiq (a.s)



Kulia ni Samahat Sheikh Hemed Jalala, pembeni yake ni Sheikh Muhammad Abdi wakiwa katika maandalizi ya kuwahubiria waumini wa Dini ya Kiislam.


Wednesday, January 21, 2015

Sheikh Jalala "Waislam na Wakristo ni Wamoja"



Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Kigogo Post Sheikh Hemed Jalala amesema Taifa la Tanzania linajulikana kama kisiwa cha amani na wakiristo na waislam wanaishi kama ndugu moja. 

Sheikh Hemed Jalala akiwa anaelezea jambo wakati wa kongamano hilo la Takfiri

Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Kigogo Post Sheikh Hemed Jalala amesema kongamano hili limewakusanya viongozi wa dini zote kwa upande wa wakristo hasa wale wenye waumini wengi na kujadiliana  juu ya amani ya nchi na taifa kwa ujumla.

Amesema
Viongozi wa Dini hawatofumbia macho kuona dalili zozote za uvunjifu wa amani kwani .
 
"Wakristo na Waislam ni kitu kimoja na tupo tayari kumpiga vita mdudu hatari atakaye kututenganisha kwani vita vitakapo tokea hasara haitakua ya Dini moja tu bali kwetu sote,"alisema Jalala

Hayo yamesemwa  jini Dar es Salaam na Sheikh Hemed Jalala wakati w a Kongamano la kidini likiwa na Ujumbe, Madhara ya Misimamo mikali ya imani za kidini (Takfiri) katika jamii na Taifa. Kongamano hilo likiwa limeandaliwa na Taasisi ya Imam Bukhary ambyo mwenyekiti wake ni Sheikh Khalfan Khamis.





Askofu wa Kanisa la Galiya Evangilist Asseblies Of God (EAGT) Msasani,Askofu Philbert Mbepera   

 Kwaupande wa askofu wa Kanisa la Galiya Evangilist Asseblies Of God (EAGT) Msasani,Askofu Philbert Mbepera amesema viongozi wa dini zote awapaswi kubezana kwa kile wanacho kiabudu.

Amesema imani ya nchi aiwezi kujengwa kwa chuki na uwasama bali ni kwa kufuata misingi ya vitabu vya Mungu ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na upendo na kuvumiliana kwa imani tofauti.

"Kwaupande wetu sisi tumefunga siku 40 kwa ajili ya kuombea amani ya nchi hasa kutokana na jukumu kubwa la kitaifa linaloikabili nchi yetu kwani viongozi wa kisiasa wanaushawishi mkubwa wa kusababisha upotevu wa amani kwa wale wanaotumia majukwaa ya dini kujinadi,"alisema Mbepera