Monday, October 2, 2017

Matembezi ya Amani ya Siku ya Ashura -Dar es salaam-Tanzania

Mabadiliko aliyoyaleta Imam Hussein (a.s) ambayo alikubali kuuwawa yeye pamoja na kizazi chake,pamoja na watoto wake pamoja na wanawake aliokuwa nao, msiba huo mkubwa uliomkumba kwaababu ya kuleta mabadilko, 

Mabadiliko hayo makubwa yalikuwa ni kuiteneneza jamii,jamii aliyoihi ilikuwa ni jamii iliyokuwa na mapungufu mengi mno akatoka na akakubali yeye auwawa pamoja na wanawe kwa ajili ya jamii ibadilike.katika mabadiliko makubwa aliyopambana nayo Imam Hussein(a.s) ni kuwa na mabadilioko ya umoja, 

Watu walikuwa wamepoteza kuwa kitu kimoja, Imamu husein (a.s) akakubali afe yeye na wanawe ili jamii alipokuwa anaishi ikamatane na kitu kinachoitwa umoja,na mimi naamini ya kwamba matembezi haya ya amani yaliyoko leo katika mkoa wa dare s salaam na ambayo yako katika nchi za wailamu husuani wailamu wa dhehebu la shia ithnasheriya.

Naamini ya kwamba matembezi haya yatakuwa ni chachuya kuwaleta watanzania waislamu kwanza kuwa kitu kimoja wenyewe kwa wenyewe lakini pili matembezi hayo yatakuwa chachu ya watanzania  wote kuwa kitu kimoja. Imam Husein (a.s) katika mambo amabyo alitoka kwa ajili yake na akafa kwa ajili yake ilikuwa ni kutetea uwanadamu ni kutetea utu, 

Leo ninaamini yakwamba dunia inahitajia utu,leo naamini ya kwamba  si Tanzania tu bali mahala popote pale dunianai wanautafuta utu wa mwanadamu urudishwe, kwa hivyo naaminiya kwamba matembezi haya ya amani huzuni hii tuliyokuwa nayo itakuwa ni chachu kubwa mno katika ardhi ya Tanzania kuhakikisha utu unarudi katika ardhi ya watanzania,

Watanzania itakiuwa ni sababu ya husein huyu itakuwa sababu kubwa ya sisi kutokubaguana, itakuwa ni sababu kubwa ya sisi kupendana na kuelewana, kwahovyo ninaamini ya kwamba imam Hussein(a.s) anahitajika leo katika ardhi ya Tanzania , 
 Image may contain: 6 people
Imam Hussein (a.s) moja katika malengo yake na katika maelekezo yake makubwa mabadiliko yake makubwa ilikuwa ni amani iliyopotea wakati wake imesambaratika, Hussein akakubali yeye na watoto wake wadogo wauwawe wengine wenye chini ya umriwa miezi 6, 

kwanini kwa sababuya kuboresha amani , utulivu na maelewano kwa wakati ule.ninaaminiya kwamba dunia leo umegubikwa na machafuko, kila mahala vita, makundi ya magaidi naamini ya kwamba vilevile Tanzania nayo inauhitajia utulivu, inahitajia amani, na inahitajia mshikamano.

Naamini yakwamba matembezi haya ya amani leo yaliyotoka katika nchi hii ya Tanzania yatakuwa ni chachu ya kuboresha amani tuliyokuwa nayo  katika nchi ya tanzania matembezi haya ya amani yatakuwa ni chachu ya kuboresha umoja na mshikamano na mashirikiano yaliyoko kati watanzania amabao hawabaguani dini zao hawabaguani rangi zao hawabaguani kabila zaowatanzania wote wanakusanywa na lugha yao ya Kiswahili, wanapendana wanaelewana na wanashikamano, wakristo waislamu hawabaguani kwa dini zao, bali wanaheshimiana na kupendana, 

Naamini yakwamba matembezi haya yatazidi kuiboresha Tanzania kuwa kisiwa cha amani kuwa mji wa maelewano, kuwa taifa amabalo watu wake wanapigiwa mfano kwa kupendana na kwa kushirikiana na haya ni mafunzo tunayoyapata katika msafara wa imam Hussein (a.s) mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w.w). Poleni kwa msiba wa Imam Husein (a.s).

Na:Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.
Matembezi ya Amani, Siku ya Ashura, 01/10/2017.
Kuanzia Ilala Boma hadi Kigogo, Dar e salaam.

Thursday, September 7, 2017

"Amani na Utulivu lazima vilindwe" Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na waandishi wa Habari leo Dar es salaam.
 Habari Kamili.
Kiongozi Mkuu wa #Waislam Shia Ithnasheria Tanzania Maulana Sheikh Hemed #Jalala ametoa Wito kwa Waislamu na Watanzania kuwa ni lazima kuhakikisha kwamba Amani na Utulivu lazima vilindwe.

Sheikh Jalala amesema hayo leo katika Kikao na Waandishi wa Habari, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. Ikiwa na Ujumbe "Ibada ya Hijja ni Suluhisho la Matatizo kwa Mwanadamu "



Monday, June 26, 2017

Sheikh Jalala atoa Salam za Eid Fitri, awataka Watanzania kudumisha Amani na Umoja.

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika kutuma Salama za kheri na fanaka za Eid fitri, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar e alaam. 
 Dar es salaam
Sisi kama Uongozi wa Masjid Ghadir, sisi kama Uongozi wa Chuo cha Imam Swadiq vilivyopo Kigogo Post Dar es salaam, vilevile sisi kama Viongozi, Maimam katika Madhehebu ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.

Tunawatakia Watanzania wote kwa Ujumla, pasina kujali dini zao, pasina kujali madhehebu zao, tunawatakiwa kheri ya Eid, tusheherekee Eid hii kama wafuasi wa Dini tofauti tukiwa na sifa nzuri ambazo anazipenda mwenyezimungu (swt).

Katika kuipokea Eid napenda niiseme falsafa kubwa ya fungu anayoizungumzia mwenyezimungu ndani ya Qur’an, anaema malengomakubwa ya funga ili watu wawe wachamungu,ndio falsafa kubwa ya funga.

Sasa funga yetu hii ya mwaka huu ya 2017, funga hii itupelekee watanzania wale tuliofunga kuwa wachamungu, na nitaongea sifa tano kwa harakaharaka ambazo sifa hizi ni sifa za mchamungu.

Sifa ya kwanza ya jamii inayomcha mungu wanakuwa na mapenzi yaani wanapendana, kwahiyo funga yetu tulioifunga kwa mwaka huu iwe ni chachu ya watanzania wale waliofunga na wale ambao hawakufunga iwe ni chachu na sababu ya wao kupendana.Iwe ni sababu ya wao kushikamana, iwe ni sababu ya wao kuelewana.

Watanzania waislamu na wasiokuwa waislamu Wakristo na Madhehebu mengine watakapo pendana, watakapo shikamana, watakapo kuwa kitu kimoja, watajaribu kuondoa matatizo mengi yaliyopo katika jamii yao. 

Katika matatizo hayo watajitahidi kuhakikisha ufakiri, Umasikini unasambaratika katika jamii yaliyomo, kwa sababu waswahili wanasema seku zote kwamba kidole kimoja hakivunji chawa, kwa hivyo mapenzi yao baina yao, mapenzi yao, mshikamano utasababisha wapambane waondoe ufakiri, umoja wao utasababisha  wapate suluhisho la wajane tuliokuwanao Tanzania.

Umoja wao na mapenzi yao utasababisha watafute suluhisho na dawa ya mayatima, vilevile watatafuta dawa ya kuwasaidia walemavu, watu wanaoishi katika mazingira magumu, nasisi kama Waislamu wa Tanzania na waisokuwa waislamu wa Tanzania tutakapo leta mshikamano huo, basi ninauhakika haya yote tutaweza kuyafanya na itakuwa ile funga anayokusudia Mungu (swt) imefikia malengo.

Jambo la pili funga inasababisha kuleta kuvumiliana, mungu anaposema kwamba ameleta funga ili muwe wachamungu, moja ya sifa ya wachamungu wanatabia ya kuvumiliana, kwa hivyo watanzania wanaombwa na kitabu cha mwenyezimungu (Qur’an) ambacho kimeshuka katika mwezi wa ramadhani kwamba funga ifikie mahala watu wanavumiliana.

Tofauti zao za Madhehebu, tofauti zao za dini, tofauti zao za mitazamo, zinawafanya hawawezi kubaguana, hawawezi kugombana, hawawezi kupigana, wala hawawezi kusutana, hii ni sifa ya watu waliofunga na matarajio ya funga ya athiri kwa namna hiyo.

Jambo la tatu mungu anaposema ametufaradhishia kufunga ili tuwe wachamungu, moja ya maana ya uchamungu, ni watu kuwa kitu kimoja, na umoja hapa napenda niuzungumzie umoja wa aina mbili:
Kwanza Umoja wa Waislamu wenyewe kwa wenyewe, kamataneni na kama ya mwenyezimugu yote kwa pamoja wala msifarikiane, nyote muwe kitu kimoja kuwakitu kimoja ni dalili ya uchamungu.

Kuwa kitu kimoja ni dalili ya kuwa mnamuabudu mungu wenu mmoja, kwahivyo  ili funga yetu ikubaliwe, na ili funga yetu ilete athari katika jamii, lazima waislamu ni watu wanaokusanywa na mwamvuli mmoja Lailah ilallah, Muhammad Rasulullah, wafanye kila bidii kuhakikisha kwamba wamekuwa kitu kimoja na siki zote umoja ni sababu ya nguvu  katika jamii.

Pili ni Umoja wa kati ya Watanzania pasina kujali na kujali dini zao, pasina kujali madhehebu zao, mwenyezimungu anapotutaka tuwe wachamungu moja ya sifa ya wachamungu ni watu wanopenda kuwa kitu kimoja.

Watanzania waliofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na wale ambao hawakufunga wanaitwa wawe kitu kimoja wungane , washikamane,  umoja tuliokuwa nao ambao hatujuani kwa makabila yetu, hatujuani kwa madhehebu zetu, hatujuani kwa dini zetu,bali tunajuana kwa anuani ya utanzania.

Mwisho naitakia Tanzania yenye kheri na Baraka na fanaka , naitakia Tanzania izidi kuwa kisiwa cha amani na maelewano na pale ambapo panakosa amani basi mwenyezimungu aparudishe pawe na amani kwa haraka iwezekanavyo, nawatakia Eid njema, yenye Baraka yenye kheri, yenye mafanikio na Eid ipite kwa salama salmini na zile sifa nzuri tuliokuwa nazo kipindi cha swaum ya ramadhani ziendelee kuwepo katika jamii ya watanzania ili ziweze kuwaathiri watu wote na nje ya mipaka yetu, namshukuru mungu .Asanteni sana.

Imetolewa na:
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Itnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
Waandhisi wa Habari wakiwa makini katika majukumu yao katika salamu za fanaka zinazotokewa na Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

Sunday, June 25, 2017

VITA YA UCHUMI TANZANIA: LHRC YAIPONGEZA SERIKALI…YATOA UKUMBUSHO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Anna Henga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo hicho, Bw. Ezekiel Massanja
KITUO CHA SHERIA na haki za binadamu (LHRC) kimepongeza juhudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kwa kupambana na mafisadi, ikiwamo hatua ya kuundwa kwa kamati mbili za Rais zilizokuwa na lengo la  kuchunguza thamani halisi ya madini yaliyomo katika makasha ya mchanga wa madini (makinikia) na ile ya kuwafikisha viongozi waandamizi wa kampuni ya IPTL mbele ya vyombo vya sharia.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Anna Henga amesema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hatua za serikali ya awamu ya tano hususani katika suala zima la uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za Nchi, na kusema wamebaini kuwa serikali inapaswa kuungwa mkono ili vita hiyo ya uchumi iweze kufanikiwa.
 
Amesema ukiangalia maamuzi makubwa yanayochukuliwa na Mh. Rais yote yamelenga kurudisha hadhi ya Taifa ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi walio wengi hivyo kuna kila sababu ya kuumunga mkono ikiwemo kutoa ushauri mbalimbali.
 
“Ikumbukwe mnamo Juni 9 mwaka 2017 kituo cha sharia na haki za binadamu kilitoa tamko hapa mbele yenu kupinga kusudio la mamlaka ya udhibiti wa nishati na madini (EWURA) kuiongezea muda wa kuzalisha umeme kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwa muda wa miezi 55” na kuanzia hapo tulishuhudia hatua ambazo zilichkuliwa na serikali kama kituo tunapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwapeleka mahakamani wahusika wakuu wa kashfa ya Tegeta Escrow ambao ni zao la kampuni ya IPTL.
 
Amesema hatua zinazochukuliwa sio tu zinaleta heshima katika Taifa lakini pia zinarejesha Imani ya Watanzania kwa serikali yao kwani wanaona kumbe dhana ya uwazi na uwajibikaji inawezekana na pia inafuta dhana ambayo imejengeka kuwa viongozi wanalindana.
 
Licha ya kuwepo kwa pongezi hizo lakini kituo cha sharia pia kimetoa angalizo kama kweli tunahitaji kuwa na vita ya uchumi yenye mafanikio katika Taifa la Tanzania lazima yafuatayo yakafanyika.
 
…YAKUMBUSHA YAFUATAYO KUFANYIKA
Kuundwa kwa mamlaka kamili ya madini; Kituo cha sharia na haki za binadamu kimeishauri serikali kuunda Mamlka kamili ya Madini itakayokuwa inafanya kazi ya uratibu wa shughuli zote za madini Tanzania kama zilivyo Mamlaka ya hifadhi ya Jamii. Mamlaka ambayo itakuwa na dhima ya kushughulika na mikataba yote ya madini, mapato ya madini, kuidhinisha leseni (vibali), kuratibu soko la madini ambapo madini yote yatauzwa hapa Nchini ili kupata fedha za kigeni.
 
Waliotajwa katika kamati zote mbili kuchukuliwa hatua, Pia kituo kimeshauri kuwa wale wote waliotajwa katika ripote zote mbili za Rais wachukuliwe hatua ikiwamo kuwafikisha katika vyombo vya sharia kujibu tuhuma zao.
 
Waitaka bunge kubadilika Kituo cha sharia kimetaka Bunge kubadilika kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya awamu ya tano, lisiendeshe mijadala kisiasa bali kwa lugha za kibunge na kutanguliza maslahi ya Nchi mbele.
 
“Tumefika hapa na kashfa hizi ambazo zimedumu kwa miongo kadhaa kwa sababu ya kuwa na bunge dhaifu lisiloweza kuisimamia serikali kwa dhati hususani katika mambo makubwa ya kitaifa. Sasa kila hoja inayowasilisha katika bunge ipewe uzito unaostahili pasipo kujali itikadi ya vyama ambazo kwa kiasi kikubwa imechangia kwa kashfa hizi kuendelea kudumu kwa miongo kadhaa” Alisema.
 
Mambo mengine ni pamoja na kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo, serikali kuheshimu misingi ya haki za binadamu, serikali kuheshimu na kulinda demokrasia pamoja na serikali kuwachukulia hatua watu wote waliohusika katika miamala ya Tegeta Escrow. 
 
Pia imeitaka serikali kuchukua hatua katika kashfa zingine ambazo zimesababisha Serikali kupata hasara ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, kashfa inayohusishwa na Kampuni ya Lugumi, kashfa ya Richmond, kashfa ya uwepo wa harufu ya rushwa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii …mathalani mradi wa NSSF kigamboni pamoja na suala la Vitalu vya uwindaji na umiliki wake

Serikali imetakiwa kuwaangalia Wajane kwa Chicho Pevu


Hawa ni Baadhi ya Wanawake Wajane walioshiriki katika hafla ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, jana Kigogo-Post Dar es salaam.

Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wajne Tanzania Wilaya ya Ubungo Dar es salaam Mh Josephine Chale amemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kuwaangalia Wajane kwa jicho la pili ili aone namnagani anaweza kuwasaidia katika Nyanja ya sheria ambayo itazuia wajane kuonewa kwa kudhulumiwa haki zao

Chale amewaomba Wajane nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa Mjane haina maana ndio mwisho wa Maisha,kwani  haliya kuwa maisha yanaendelea

Aidha Chale ameushukuru Uongozi wa Msjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kuweza kuwaalika Wajane katika futari ya pamoja ili Wajane wajisikie kwamba na wenyewe wanatakiwa katika jamii, ili wasijitenge kama vile kwamba wamefiwa basi ndio maisha yamefika mwisho.


Hayo alisema jana katika halfa ya futari ya pamoja na Wajane,iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq Vilivyopo Kigogo Post Dar es salaam.

“Napenda tena kuwashukuru Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kwa kutualika sisi wajane, tumepata faraja kubwa sana, kwani na sisi tutaenda kufanya kama wanaofanya wenzetu ili tuwape amani wajane.Tunashukuru sana sana,tunamuomba Mungu awape Moyo wa upendo, awape riziki na awape maisha marefu.”
 
Mtumishi wa Chuo cha Imam Swadiq (a.s) Bi Fatma Mwiru akisilisha mada yake mbele ya Wanawake Wajane waliohudhuria katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uomgozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, Kigogo Post Dar es salaam.
Kwa upande wake Mtumishi wa Imam Swadiq Bi.Zaynab Ndete alisema lengo la hafla hii ya Futari ya Pamoja na Wajane, ni Tumewaalika wanawake Wajane kutoka  Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam, lengo kubwa ni kuzungumza nao na kuwapatia muongozo wa Kisheria, hususani zinazowahusu wao baada ya kufiwa na waume zao.

“Kwa kweli swala ya Ujane ni swala zito ni swala gumu, kwasababu ni swala linalomuhusu mwanamke, kama tunavyoangalia katika jamii yetu ya Kitanzania wajane wengi wanapokuwa wametoza wame zao, wanakuwa ni watu ambao wanakuwa katika matatizo makubwa sana, miongoni mwa matatizo wanayokumbananayo ni kutengwa au kunyanyapaliwa na familia ya mume ,kunyang’anywa haki zao za msingi, kunyang’anywa mali zao ambazo wameachiwa kama urithi na wame zao” alisema Ndete

“Sisi Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq tumewaita hapa kwanza kuwasaidia waweze kuzifahamu haki zao, wamama wajane hawatakiwi wawe wanyonge pale wanapoondokewa na wame zao,kuondokewa na mume ni jambo Mwenyezimungu (swt) ameliandika kuwa ni lalazima kwani anaweza kuondoka Mume au Mke” aliongeza Ndete.

“Dini ya Kiislam imesimama kidete juu ya kuwatetea wanawake wajane, kwani ukiwa mjane unahaki ya Kuishi kama wengine,anahaki ya kuwa na mali,unahaki ya kuwa Kiongozi,unahaki ya kuwa Bosi, anahaki kuwana amani na upendo, anahaki ya kuwa Muajiriwa, anahaki ya kuolewa na Mwanaume mwingine,anahaki ya kumiliki” alisisitiza

Hatahivyo Mtumishi Ndete aliwaomba Wanawake wajane wasiwe wanyonge na wasimame kidete kuweza kusimamia malezi ya familia zao kwani jukumu la kuwalea watoto aliokuwachia mumewe iko mikononi mwako.

Saturday, June 24, 2017

Siku ya Quds:Sheikh Jalala,Prof Lipumba walaani dhulma Wanayofnyiwa Wapalestina

Waaumini wa Dini ya Kiislam na Wapenda Amani Duniani wakitembea ktika Matembezi ya Amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds,leo Dar es salaam
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnsheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala  amewataka watanzania kuunga mkono harakati za kupinga vitendo vya dhuruma na unyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya wapalestina.
Image may contain: 3 people, crowd
Kiongozi Mkuu wa Wislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Wndishi wa Habari katika Mtembezi ya Amni ya Siku ya Kimataifa ya Quds.leo Dar es salaam.
 Amesema ikiwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yanasifika kuwa ni kisima cha amani hivyo ni wajibu wa kuipigania amani kwa nchi zingine ambazo imetoweka.
Sheikh Jalala amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika  matembezi ya amani ya kuwakumbuka wapalestina ambao wamepoteza amani waliokuwanayo, matembezi hayo yalioanzia Ilala Boma hadi Viwnj vya People Kigogo jirani na Msjid Ghadir, Dar es salam

Sheikh Jalala, amesema kuwa kuna haja ya kuhakikisha watanzania wanafanya juhudi za makusudi za  kupinga vitendo vinavyoendelea nchini Palestina ili nao wae na amani kama iliokuwa awali.
 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani ya Siku Kimataifa ya Quds
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa ameshiriki kwenye matembezi hayo kwa ajili ya kuashiria sauti ya pamoja ya kudai hali ya amani na kupinga dhuluma inayofanywa dhidi ya wapalestina.

Amesema Tanzania ina kila sababu ya kupinga vitendo hivyo kutokana na kuwa hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa kiongozi wa taifa alipinga hali hiyo ya vitendo vinavyofanywa dhidi ya wapalestina.

“Mwalimu Nyerere alikuwa karibu na wapalestina katika kudai haki yao hivyo bado Tanzania inatakiwa kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na mwasisi wa taifa katika kudai hali ya amani nchini humo”alisema.
Wanawake wa Kiislam na Wapenda Amani Duniani wkishiriki katika Matembezi ya Amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaameyofanika leo Dar es salaam
Siku ya Kimataifa y Quds ni siku ya kuwakumbuka Wapalestina na Watu wote ulimwenguni wanaoonewa, Siku ya Kimatifa iliasisiwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Imam Khomein (r.a), ambae aliteua Siku ya Kimatifa ya Quds kuwa kila siku ya Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.