Monday, November 20, 2017

Tumetoka kwa Matembezi ya Amani ili kuoyesha Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)-Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala (wapili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar es salaam la Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania (T.I.C) Sheikh Suleiman Serehani (wakwanza kulia) wakiongoza Matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), jana Jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Sababu kubwa inayowafanya Waislamu, hususani Waislamu Shia Ithnasheria Kutoka na kufanya Matembezi ya Amani  kuadhimisha kifo cha mtume ni kuionyesha jamii huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na huruma kwa watu wote.

“Miaka zaidi ya 1400 leo bado tunakumbuka Kifo cha Mtume Muhammd (s.a.w.w), kwanini tutoke katika matembezi haya ya amani tunayoyaonyesha katika ardhi yetu ya Tanzania, kwasababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitumwa kuwa na huruma kwa watu wote” Alisema Sheikh Jalala.
 
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari, jana katika Matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), matembezi yaliyoanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Kigogo Jijini Dar es salaam.
Sheikh Jalala alisema hayo mwiho wa wiki wakati wa matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Mbora na mtukufu kwa watu wote ambae ni Muhammad (s.a.w.w), katika matembezi yaliyoanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam.

“Siku ya Kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni siku ya kukumbuka Utu, Busara,Uwanadamu, kuwaheshimu wasiokuwa na Dini,kukaa vizuri pamoja na Wakristo, Mayahudi, wanaoabudu Masanamu na Mapagani  aliokuwa akiujali katika maisha yake” aliongeza Sheikh Jalala.
 
Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar e salaam la Waoslamu Shia Ithnasheria Tanzania (T.I.C) Sheikh Suleiman Serehani akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani yaliyofanyika jana kuanzia Ilal Boma hadi Viwanja vya Pipo Kigogo Jijini Dar e salaam
Aidha Sheikh Jalala alisema Mtume Muhammd (s.a.w.w) aliuwezi Waislamu kwa waislamu, Umoja wa Watu wote na alitengeneza Umoja kati yake na Wakristo, Mapagani na Mayahud , umoja huu ulikkuwa ni wa kumsaidia mtu yoyote ambae atashambuliwa hatimae akatengeneza Mazingira asiekuwa Mwislamu akishambuliwa Waislamu watanyanyuka kumsaidia na Waislamu wakishambuliwa watu wa Dini nyingine na Madhehebu nyingine watanyanyuka  kuwasaidia Waislamu.

“Napenda kuwaelekeza Viongozi wa Kidini Masheikh, Maustadhi, Makasisi, Maskofu, na Mashemas  kwamba Mimbari au Madhabahu yao Siku za Ijumaa au Siku za Jumamosi na Jumapili, Madarasa zao, Vyuo vyao vitumike katika kuleta na kuboresha Amani ya watanzania wote, katika kuleta maelewano, Mshikamano ya watanzania wote na Tiafa hili liendelee kuwa kisiwa cha Amani” Alisisitiza Sheikh Jalala

Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki Dunia tarehe 28, Mwezi wa Safar, Mwaka 11 Hijiria kwa Mujibu wa Kalenda ya Kiislamu, Mtume alikufa akiwa na Umri wa miaka 63.

Wednesday, November 15, 2017

40 ya Imam Husein (a.s) tusimame kutetea haki za Binadamu na Kupinga Ugaidi –Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika kuadhimsisha Siku ya 40 ya Imam Hussein (a.s), Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka Watanzania Waislamu na Wasiokuwa Waislamu kusimamia na kutetea haki za Binadamu yoyote na kupina aina yoyote ya Ugaidi kwani kufanya hivyo ndio  moja ya mafunzo yanayopatikaka katika kuadhimisha 40 ya Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

“Tukio la 40 ya Imam Hussein (a.s) katika funzo la kwanza linabeba darasa la Ubinadamu, Mwanadamu anahadhi, anaheshima, ni mtakatifu,nilazima aenziwe,ndio Uislamu umekataza kumdhuru, kumnyanganya na ni haramu kumwaga Damu ya mwanadamu yoyote, Mwanadamu awe Mwislamu, awe Mkristo, awe Pagani” Alisema Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alisema hayo wiki ilipita wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam na kusema kuwa 40 ya Imam Hussein inatoa funzo la kupinga aina yoyote ya Ubaguzi,uwe ubaguzi wa Rangi,uwe ubaguzi wa kidini,uwe ni ubaguzi wa Kifikra, ndio maana ukiangalia katika msafara wake wa kiulekea katika Mji wa Karba nchini Iraq utakuta mtu anaeitwa John ambae ni Mkristo.


Aidha Sheikh Jalala amewataka Watanzania kutowanyanyapaa na kuwatenga watu ima katika Umasikini wao, ima kwa ufakiri wao, ima kwa magonjwa yao, ima kwa mapungufu yao walioumbwa nayo, walemavu wa ngozi, macho, masikio, miguu, mikono, na waadhirika wa Madawa ya kulenya.

“Tukitaka tufaidike na Rasilimali alizotupa Mungu ni lazima tuwe Wazalendo, Watanzania tutakaposifika na Uzalendo, tutafaidika na Gesi yetu, ardhi yetu,Madini yetu, mafuta yetu, Tanzania itajulikana kwamba ni Moja katika nchi inayotoa misaada kwa nchi zingine, hii ni funzo tunayopata katika 40 ya Imam Hussein (a.s)” Alisema Sheikh Jalala

Hata hivyo Sheikh Jalala amesema kuwa unapowaona Waislamu wananyanyuka huku wakisema Labayka ya Hussein (a.s) maana yake wanamuambia Hussein (a.s) wewe ulitoka kupambana na aina yoyote ya Ugaidi, sisi tupo tayari kupambana na kuusambaratisha aina yoyote ya Ugaidi, Ugaidi wa Kifikra, Kimtazamo, pia waislamu na Wakristo tunahakikisha mafunzo tunayowafundisha watoto wetu hayabebi fikra yoyote ta Ugaidi.


Imam Hussein (a.s) ni Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), yeye ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s) Baba yake ni Imam Ali Ibn Abutwalib (a.s), Mama yake ni Fatuma Bint Muhammad (a.s), Kaka yake ni Imam Hassan Ibn Ali (a.s), Dada yake ni Zaynab Bint Ali (a.s), 40 ya Imam Hussein (a.s) ni siku ya arobaini baada ya kuuliwa yeye Imam Hussein (a.s) na Maswahaba zake katika ardhi ya Karbala, nchini Iraq, mwaka wa 61 H.

Thursday, November 9, 2017

Waislamu Nchini waondolewa shaka katika kujiandikisha Sensa

Waislamu watakiwa kumuunga mkono Muft Abubakar kwa kushiriki zoezi la sensa
Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi akizungumza leo Masjid Ghadir, Kigogo Dar es salaam juu ya Umuhimu wa Sensa na kumpongeza Mh. Muft wa Tanzania Abubakar Zuberi.
“Kama umoja wa Vijana wa Kiislamu BAKWATA Taifa tunaomba kuwatoa hofu wale wote ambao wanaoona zoezi la Sensa, kwa Wiaslam linaweza kugeuka kuwa chanzo cha mfarakano wa Taifa Kiimani, haiwezi kuwa hivyo tunavyomfahamu  Mhe. Muft wetu Abubakkar Zuberi ni mwenye kuongozwa na Qur’an na hadith za Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Katibu wa Umoja huo Sheikh Zuberi

Sheikh Zuberi amesema kuwa dhima kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanahesabiwa, makatibu wanapaswa kumsaidia mufti katika hilo ili kuweza kuwa na Idadi kamili ya Wailsamu hapa nchini na kufahamu wako wapi, wanafanya nini, wangapi hawana kazi, wazee wangapi, nguvu kazi ikoje taarifa ambazo ni muhimu kwa mustakabali wa Waislamu.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika eneo la Masjid Al Ghadir Kigogo Post, Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi alisema tangu alipochaguliwa Muft Abubakar mwaka 2015 ameweza kufanya mambo mbalimbali baada ya kutoa maelekezo kwa viongozi wa dini ikiwemo kudumisha amani, kuunganisha jamii,  kuleta maendeleo, ushirikiano mzuri wa Baraza na Mashirika ya Dini ya ndani na nje ya nchi.

Aidha Sheikh Zuberi ameendelea kusema kuwa Mh.Muft kaamrisha mema na kukataza maovu, uboreshaji wa elimu ya dini na secula, kusisitiza kujitambua, mahusiano mazuri kati ya Baraza na viongozi wa nchi, kukataza kufanya kazi kwa mazoea, na sensa kwa maendeleo ya waislamu ambapo ameagiza kupatikana kwa takwimu sahihi kwa waislamu kupitia misikiti mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo Sheikh Zuberi ameongeza kuwa Mh. Muft katika kuonyesha umakini Mkubwa katika kuwatumikia Waislamu, hivi karibuni aliwaagiza makatibu wa Baraza la BAKWATA kujiandaa na Sensa ya waislamu, Misikiti na Madrasa kote nchini, ni zoezi lenye lengo jema la kutoa huduma kwa usahihi kwa watu unaowatumikia.
Waandishi wa Habari, Vijna wa Umoja wa Kiislamu BAKWATA Taifa na baadhi ya wageni waliohudhuria katika kikao hicho kutoka Chuo cha Kiislamu (Hawzat) Imam Jafar Swadiq (a.s) wakifauatilia kwa ukaribu jumbe mbalimbali zinazotolewa na Umoja huo, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es salaam.

Sunday, October 8, 2017

Sheikh Jalala Na Askofu Banza Wamuenzi Imam Hussein kwa kuzindua Mpango Wa Kugawa Maji Na Vipeperushi Bure.

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akigawa maji kwa baadhi ya wakazi wa kata ya kigogo Mbuyuni mara baada ya kuzindua programu ya kugawa maji na vipeperushi bure jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala, Mchungaji kanisa la Tanzania Outreach Ministries Banza Suleiman na Mwenyekiti wa Kata ya Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani wakikata utepe kuzindua programu ya kugawa maji na vipeperushi burejijini Dar es salaam. 
 
Habari Kamaili
 
Waislam wa dhehebu la shia katika kuelekea siku ya Ashura Leo tarehe 10 ya muharram ambao ni sawa na mwezi wa kwanza katika kalenda kiislam wamezindua program ya ugawaji maji na vipeperushi bure iliyofanyika katika msikiti wa kigogo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo msikitini hapo Sheikh Jalala amesema kuwa zoezi hili la kugawa maji linaendana sambamba na kumuenzi Imam Hussein ambaye ni mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Mohamad ambaye alifariki kwa kuwatetea wanadamu bila kuangalia itikadi zao za kidini, kikabila wala maumbile.
Sheikh Jalala alisema imam hussein amekuwa ni alama kwa dunia kwa kukubali yeye kufa ili watu wapate amani pamoja na kutendeana mema ikiwemo kupendana, kuhurumiana kuheshimiana na alithubutu kuyafanya hayo wakati huo ambao mema yalipungua katika dunia na hakukuwepo amani miongoni mwa wanadamu hao na matokeo yake yalikuwa ni ugomvi na chuki ndani ya kizani hicho.
Alisema Imam Hussein anatufundisha watanzania kuwa ni watu wenye huruma, upendo ushirikiano na amani tuliyopewa kama nuru yetu Watanzania, ndiyo maana msikiti huu umeamua kuanzisha program kama hizi ikiwemo kuwatembelea wagonjwa, kujitolea damu kwa hiari, kwenda kuwapa moyo wafungwa pamoja na kuwaona na kuwapa misaada watoto yatima ikiwa ni miongoni mwa njia za kumuenzi Imam huyo aliyejitoa kwa ajiri ya wanadamu.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Christian Outreach Ministries Mchungaji Banza Suleiman alisema kitendo kilichofanywa na msikiti huo ni chema na kinapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania anaependa maendeleo kwani maisha yetu wanadamu yanategemea maji kwa kiasi kikubwa, hivyo ili kumuunga mkono Rais Magufuli kufikia kuwa na uchumi mzuri wa viwanda ni lazima watu wawe na maji ya kutosha ili waweze kufanya kazi ipasavyo.

alisema mungu anambariki anaetoa hivyo kwa kujitolea huko mungu awabariki sana na hata serikali itafurahi kwa kuona taasisi za kidini zipo kwa dhumuni la kuwajari wananchi wake kama kitendo kilichofanywa na msikiti huo, pamoja na wananchi wa maeneo hayo wataona ni jambo jema kutokana na maisha ya mwanadamu yanategemea maji hivyo bila maji hakuna maisha.
Nae Mwenyekiti wa Mtaa Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani alisema wanaishukuru taasisi Shia kwa kuchangia maendeleo ya kata hiyo kwa kiasi kikubwa kwani imekuwa ikijitolea mambo mengi kama matibabu bure kwa wagonjwa, kusaidia watoto yatima katika kata hiyo kama madaftari na vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi na huduma nyingine nyingi.
Aidha Bw.Nguogani aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za kimaendeleo kama kupanda miti, kufanya usafi maeneo ya kata hiyo, kuchangia ujenzi mbalimbali katika kata hiyo.
Alisema taasisi hiyo imekuwa itatoa misaada na kusaidia kufanya majukumu mengi ambayo kimsingi mengine utekelezwa na sreikali lakini taasisi hiyo wamekuwa wakijitolea hivyo kuwanufaisha wakazi wa kigogo na nifahari sana kwa uwepo wa msikiti huo mahali hapo.

Monday, October 2, 2017

Matembezi ya Amani ya Siku ya Ashura -Dar es salaam-Tanzania

Mabadiliko aliyoyaleta Imam Hussein (a.s) ambayo alikubali kuuwawa yeye pamoja na kizazi chake,pamoja na watoto wake pamoja na wanawake aliokuwa nao, msiba huo mkubwa uliomkumba kwaababu ya kuleta mabadilko, 

Mabadiliko hayo makubwa yalikuwa ni kuiteneneza jamii,jamii aliyoihi ilikuwa ni jamii iliyokuwa na mapungufu mengi mno akatoka na akakubali yeye auwawa pamoja na wanawe kwa ajili ya jamii ibadilike.katika mabadiliko makubwa aliyopambana nayo Imam Hussein(a.s) ni kuwa na mabadilioko ya umoja, 

Watu walikuwa wamepoteza kuwa kitu kimoja, Imamu husein (a.s) akakubali afe yeye na wanawe ili jamii alipokuwa anaishi ikamatane na kitu kinachoitwa umoja,na mimi naamini ya kwamba matembezi haya ya amani yaliyoko leo katika mkoa wa dare s salaam na ambayo yako katika nchi za wailamu husuani wailamu wa dhehebu la shia ithnasheriya.

Naamini ya kwamba matembezi haya yatakuwa ni chachuya kuwaleta watanzania waislamu kwanza kuwa kitu kimoja wenyewe kwa wenyewe lakini pili matembezi hayo yatakuwa chachu ya watanzania  wote kuwa kitu kimoja. Imam Husein (a.s) katika mambo amabyo alitoka kwa ajili yake na akafa kwa ajili yake ilikuwa ni kutetea uwanadamu ni kutetea utu, 

Leo ninaamini yakwamba dunia inahitajia utu,leo naamini ya kwamba  si Tanzania tu bali mahala popote pale dunianai wanautafuta utu wa mwanadamu urudishwe, kwa hivyo naaminiya kwamba matembezi haya ya amani huzuni hii tuliyokuwa nayo itakuwa ni chachu kubwa mno katika ardhi ya Tanzania kuhakikisha utu unarudi katika ardhi ya watanzania,

Watanzania itakiuwa ni sababu ya husein huyu itakuwa sababu kubwa ya sisi kutokubaguana, itakuwa ni sababu kubwa ya sisi kupendana na kuelewana, kwahovyo ninaamini ya kwamba imam Hussein(a.s) anahitajika leo katika ardhi ya Tanzania , 
 Image may contain: 6 people
Imam Hussein (a.s) moja katika malengo yake na katika maelekezo yake makubwa mabadiliko yake makubwa ilikuwa ni amani iliyopotea wakati wake imesambaratika, Hussein akakubali yeye na watoto wake wadogo wauwawe wengine wenye chini ya umriwa miezi 6, 

kwanini kwa sababuya kuboresha amani , utulivu na maelewano kwa wakati ule.ninaaminiya kwamba dunia leo umegubikwa na machafuko, kila mahala vita, makundi ya magaidi naamini ya kwamba vilevile Tanzania nayo inauhitajia utulivu, inahitajia amani, na inahitajia mshikamano.

Naamini yakwamba matembezi haya ya amani leo yaliyotoka katika nchi hii ya Tanzania yatakuwa ni chachu ya kuboresha amani tuliyokuwa nayo  katika nchi ya tanzania matembezi haya ya amani yatakuwa ni chachu ya kuboresha umoja na mshikamano na mashirikiano yaliyoko kati watanzania amabao hawabaguani dini zao hawabaguani rangi zao hawabaguani kabila zaowatanzania wote wanakusanywa na lugha yao ya Kiswahili, wanapendana wanaelewana na wanashikamano, wakristo waislamu hawabaguani kwa dini zao, bali wanaheshimiana na kupendana, 

Naamini yakwamba matembezi haya yatazidi kuiboresha Tanzania kuwa kisiwa cha amani kuwa mji wa maelewano, kuwa taifa amabalo watu wake wanapigiwa mfano kwa kupendana na kwa kushirikiana na haya ni mafunzo tunayoyapata katika msafara wa imam Hussein (a.s) mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w.w). Poleni kwa msiba wa Imam Husein (a.s).

Na:Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.
Matembezi ya Amani, Siku ya Ashura, 01/10/2017.
Kuanzia Ilala Boma hadi Kigogo, Dar e salaam.