Monday, November 3, 2014

Hawza Imam Jafari Swadiq wasafisha Barabara

Sheikh Hemed Jalala akiwapungia mkono wanannchiwa kigogo, jijini Dar es salaam, kulia kwake ni Sheikh Zuberi Kabwe

Sheikh Hemed Jalala akionesha mfano wa kufanya usafi katika maendeo ya barabarani, kigogo

Sheikh Hemed Jalala akiwa ana Wanaharaati wake maeneo ya kigogo wakikusanya uchafu

Sheikh Hemed Jalala akielekea katika eneo la usafi bunde baada ya mvua kunyesha

Sheikh Hemed Jalala akiongoza msafara kwenda kuanza usafi.







Hawza Imam Jafar Swadiq chini ya Sheikh Hemed Jalala katika kukukmbika kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni Imam Hussein (a.s) wamefanya shughuli mbali mbali za Kijamii kama Kuwatembelea Wafumgwa, ambapo walikwenda katika Mahabusu ya Watoto Upanga, Dar es salaam, Kusafisha Barabara na Kujitolea Damu katika Hospitali ya Muhimbili

Thursday, October 30, 2014

Hawza Imam Jaafar Swadiq yatembelea Mahabusu ya Watoto


Meneja wa Hawza ya Imam Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala, amewataka watu kutoa misaada ya hali na mali kwa watu wanaoishi Magerezani kwa kuzingatia wao ni Binaadam wanahitaji mahitaji kama watu walio huru.

Hayo yamesemwa leo na Sheikh Salim Mwamba wakati walipotembelea Mahabusu ya Watoto, Upanga Jijini Dar es salaam, wakikumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Imam Hussein (a.s).

 “Sio kila aliye Gerezani ni mkosa,kwani wao wanahitaji huduma za kijamii kama chakula na mavazi kama watu walio huru” alisema sheikh Mwamba.

“Imam Hassan Askari na Nabii Yusuph walifungwa Gerezani na hali ya kuwa hawana makosa”ameongeza Sheikh Mwamba.

Sheikh Mwamba amewataka askari magereza kuwa na moyo wa ubinaadam, kwa kuwatendea Haki na Uadilifu wafungwa waliopo gerezani kwa kuwa ni watu kama wao na wanamahitaji kama yao.

Wanaharakati wa Imam Jafar Swadiq wanafanya shughuli mbalimbali za kijamii kama Kusafisha Makaburi, Kutembelea magereza, kusafisha barabara na kujitoea damu, kwa ajili ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni Imam Hussein ibn Ali.


Imam Hussein (a.s) alizaliwa tarehe 15, mwezi wa Shaaban Mwaka 4 A.H na Fatma bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Amirul Muuminina Ally na aliuwawa tarehe 10 Muharram katika mji wa karbala nchini Iraq.

Sunday, October 26, 2014

'Vitisho havitazuia maombolezo ya Imam Hussein AS'


Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah
Habari Kamaili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kuna udharura mkubwa wa kutumiwa vyema siku hizi za maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi huu wa Muharram na kuwataka viongozi wa Lebanon kuwa makini katika kuzima njama zilizopangwa za kuzusha fitina na mifarakano kaskazini mwa nchi hiyo.
 
 Akizungumza kwa mnasaba wa kuanza mwezi wa Muharram na kukumbuka masaibu ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake watiifu katika ardhi ya Karbala.


Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea matukio mbalimbali  katika nyanja za kisiasa, kiusalama, kifikra, kidini, kiuchumi kiimani na kijamii na kusisitiza kwamba, leo hii umma wa Kiislamu unapaswa kuwa macho katika kukabiliana na changamoto kubwa ya makundi ya kitakfiri na kigaidi  katika eneo la Mashariki ya Kati na hasa katika nchi za Lebanon, Iraq na Syria. 


Sayyid Nasrullah amelielezea tukio la Karbala na kusisitiza kwamba, tukio hilo litaendelea kubaki katika historia ya mwanadamu kwani limepelekea kuhifadhiwa Uislamu na watu wote wanajukumu la kubainisha kilichojiri katika ardhi ya Karbala.


Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa, watu wanaofikiri kwamba kwa kuanzisha vita vya kisaikolojia na vitisho wataweza kuzuia kufanyika maombolezo ya Aba Abdillah Imam Hussein AS wanajidanganya, kwani  vitisho hivyo havitawatenganisha na Imam Hussein AS.


http://kiswahili.irib.ir/habari/mashariki-ya-kati/item/44010-nasrullah-vitisho-havitazuia-maombolezo-ya-imam-hussein-as

Hawza ya Imam Jafar Swadiq Wasafisha Makaburi ya Kintiku, Kigogo.



Wanafunzi na Wanahakati wa Imam Jaafar Swadiq wakisafisha makaburi.


Sheikh Salim Mwamba wa Hawza ya Imam Jafar Swadiq akisafisha makaburi ya Kintinku,kidogo dar es salaam. 





Habari Kamili
Hawza ya Imam Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala imewataka Wananchi pamoja na Serikali kusimamisha Haki na kuifanyia kazi haki ili kupata jamii bora.
Hayo ameyasemwa Sheikh Salim Mwamba wakati Wakifanya Usafi katika Makaburi yaliyopo Kintiku, Kigogo, Jijini Dar es salaam, wakikumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Imam Hussein (a.s).
“Imam Hussein (a.s) alitoka Makka akaenda Iraq kwa ajili ya kusimamisha haki aliyosimamisha Babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwataka watu waitekeleze haki”alisema Sheikh Mwamba.
Sheikh Mwamba ameongeza kuwa Jamii na Serikali wanatakiwa kutoa haki kwa usawa bila ya kuegemea katika udugu, ujirani wala udini, ili kujenga jamii yenye kupenda Haki.
“Jamii na Serikali ikitoa haki kwa usawa bila kuegemea upande wowote, itajenga jamii yenye kupenda haki na kuisimamia haki kama alivyoisimamia Imam Hussein ( a.s) mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliongeza Sheikh Mwamba.
Waislamu kote ulimwenguni huadhimisha mwezi huu kwa huzuni kubwa kwa kukumbuka kifo cha Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).
Imam Hussein (a.s) alizaliwa na Fatma bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Amirul Muuminina Ally tarehe 15, mwezi wa Shaaban Mwaka 4 A.H na aliuwawa tarehe 10 Muharram katika mji wa karbala nchini Iraq.

Friday, October 24, 2014

BILAL MUSLIM MISSION YA TANZANIA YALAANI HUKUMU YA KIFO KWA SHK. NIMR

aasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania inaungana pamoja na watafuta haki na usawa wote duniani kuonesha mshituko wao kwa hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqr Al-Nimr kwa madai yake ya kutaka haki na usawa kwa wananchi nchini Saudi Arabia 


Tunaomba muungano wa wapenda haki na usawa duniani kote kuitaka mamlaka ya Saudi Arabia kufuta hukumu ya kifo kwa Sheikh Al-Nimr. Na kuwa serikali nchini humo imuachie kwa moyo wa kidemokrasia, maadili na kanuni kama zilizoanishwa katika tangazo la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa.

Kusiwe na Taifa katika Umoja wa Mataifa ambalo litajiwekea utawala wa kisiasa ambao si wa Jamhuri ya kidemokrasia. Vinginevyo ni uvunjwaji wa haki za binaadamu. 

Asibughudhiwe mtu kwa kusimama kwake na kutete haki za binaadamu kwa kiasi cha uhuru wake wa kidemokrasia, kujitegemea na usawa wa watu na haki zao. 

Binadamu wawe ni familia moja katika kuhifadhi haki ya utu wao, Haki ya uhuru wa kujieleza, Haki ya Kidemokrasia, Matakwa binafsi na Utawala wa kujitegemea. Chanzo cha habari.
chanzo afroshia.

JA'FARI: TANZANIA NI LANGO LA KUINGIA AFRIKA MASHARIKI.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema kuwa, Tanzania ni lango la kuingizia bidhaa za Kiirani katika eneo la Afrika Mashariki.
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania Mehdi Agha Ja'fari
 
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amezungumzia uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi muhimu mno kwa ajili ya kusafirisha na kupeleka nje bidhaa za Iran zisizo za mafuta na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa lango la kuingiza bidhaa za Kiirani huko Afrika Mashariki.
 
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amesema, Tanzania na bandari ya Dar es Salaam kuwa pambizoni mwa bahari ya Hindi na kuwa kwake karibu na maeneo ya kiuchumi ya magharibi mwa Asia hususan Ghuba ya Uajemi ni sifa nzuri zinazotayarisha mazingira bora ya kufanyika biashara kati ya Tanzania na Iran. 
 
Balozi wa Iran mjini Dar es Salaam amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa, usafirishaji wa bidhaa zisizo za mafuta za Iran kuelekea Tanzania umeongezeka mno katika kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni. Chanzo cha habari:
chanzo Afroshia
Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania inaungana pamoja na watafuta haki na usawa wote duniani kuonesha mshtuko wao kwa hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqr Al-Nimr kwa madai yake ya kutaka haki na usawa kwa wananchi nchini Saudi Arabia
Tunaomba muungano wa wapenda haki na usawa duniani kote kuitaka mamlaka ya nchini Saudi Arabia kufuta hukumu ya kifo kwa Sheikh Al-Nimr. Na kuwa serikali nchini humo imuachie kwa moyo wa kidemokrasia, maadili na kanuni kama zilizoanishwa katika tangazo la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa.
Kusiwe na Taifa katika Umoja wa Mataifa ambalo litajiwekea utawala wa kisiasa ambao si wa Jamhuri ya kidemokrasia. Vinginevyo ni uvunjwaji wa haki za binaadamu.
Asibughudhiwe mtu kwa kusimama kwake na kutete haki za binaadamu kwa kiasi cha uhuru wake wa kidemokrasia, kujitegemea na usawa wa watu na haki zao.
Binadamu wawe ni familia moja katika kuhifadhi haki ya utu wao, Haki ya uhuru wa kujieleza, Haki ya Kidemokrasia, Matakwa binafsi na Utawala wa kujitegemea.
- See more at: http://www.dunialeo.com/sw/posts/browse/local-news/bilal-muslim-mission-ya-tanzania-yalaani-hukumu-ya-kifo-kwa-shk-nimr-1#sthash.M7BGl1Aw.dpuf

Thursday, October 23, 2014

Mamia ya Waislamu Waandamana

Mamia ya Waislamu jana walifanya maandamano makubwa mkabala wa Ubalozi wa Saudi Arabia mjini London, Uingereza wakipinga adhabu ya kifo iliyotolewa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo dhidi ya Sheikh Nimr Baqer al Nimr mwanachuoni mashuhuri wa nchini Saudi Arabia. 
Sheikh Nimr Baqer al Nimr. 

Waandamanaji hao walipiga nara za 'Mauti kwa utawala wa Aal Saud' na ' Sheikh Nimr aachiliwe huru' sanjari na kubeba mabango na maberamu yaliyo dhidi ya utawala wa kifalme wa Saudi Arabia, walisisitiza juu ya kuachiliwa huru mwanachuoni huyo.

 Waandamanji hao sanjari na kuutaja utawala wa Saudi Arabia kuwa mvunjaji mkuu wa haki za binadamu na unayaunga mkono makundi ya kigaidi, wameitaka serikali ya Riyadh kumuachilia huru Sheikh Nimr Baqer al Nimr. 

Kijana mmoja wa Kimarekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo amelalamikia jinsi nchi zinazojinadi kuwa watetezi wa haki za binadamu kama vile Marekani na Uingereza kwa kunyamazia kimya hukumu hiyo ya kidhuluma 

Na kusisitiza kwamba kimya hicho kinaonyesha wazi kuwepo mashirikiano kati ya madola hayo ya Magharibi kwa utawala huo wa kifalme katika kutenda jinai na kuwakandamiza wananchi wa Saudia. Kijana huyo amesema na hapa tunamnukuu:

 ' Mimi siyo Muislamu na wala Mwarabu, lakini naamini kwamba Sheikh Nimr ni kiongozi huru ambaye amedhulumiwa na utawala katili na wa kifalme wa Saudi Arabia', mwisho wa kunukuu. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yamelaani vikali hukumu hiyo ya kidhuluma iliyotolewa dhidi ya mwanachuoni huyo. Chanzo cha habari: