Saturday, July 25, 2015

Kujengea Makaburi Kwa Fikra za Kiwahhab (Answar Sunna) Ni Haram

Sheikh Abdullatwif Swalehe akito hotuba juu ya siku ya Huzuni kwa Kubomolewa Makaburi Matukufu
Sheikh Abdullawif Swalehe aliuliza kuwa kama Fatwa ya kupomoa Makaburi ni Sahihi, ni kwanini makaburi ya khalifa wa kwanza Abubakar na wapili Omar hayajabomlewa ambayo yamejengwa ndani ya msikiti?
Amesema kitendo cha Utawala wa Kiwahhabi (Answar Sunna) cha kutoa fatwa za kuhalalisha makaburi na sehemu tukufu za Mkumbusho ya Waislam kupomolewa , ni kitendo ambacho kinachopingana na Qur’an tukufu ya Allah (swt).
Hayo aliyasema Jana katika Maadhimisho ya Siku ya Huzuni (Majonzi) yaliyofanyika Msikitini Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam ambayo huwa yanafanyika kila mwaka katika tarehe kama hii ya Shawwal 8 1344.
“Jamii yoyote huwa inatunza na kudumisha athari za matukio muhimu ili watu wengine waweze kuzitambua kama matukio yalifanywa na Mitume.Maimam, Makhalifa na Waja wema wa Allah (swt) alisema Sheikh Swalehe.

Katikatini sheikh Abdull latwif Swalehe , wa kwanza Kulia ni Sheikh Ammar Maulid na wa mwisho Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Imam Swadiq Kilichopo Kigogo-Post Dar es salaam

Mwanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq akiwa ndie mc mr Iddy Saidi ambaye anasoma Darasa la 4




Wanafunzi wanaharakati pamoja na Waumini wakiwa makini kusikiliza MADA zinazowasilishwa mbele yao kutoka kwa Sheikh Abdullatwif Swalehe juu ya Siku ya Huzuni


Ni wajibu kwa Mwislam Kujiandikisha Kupiga Kura-Sheikh Jalala.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam katika kipindi hiki cha uandikishaji wa daftari la kupigia kura, waumini wajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuja kuitumia haki yao ya msingi ya kumchagu mtu wamtakae.
“Kipindi hiki kinahitajia lugha za busara,na maelewano,ni wajibu wa waislaam kisheria kujiandikisha na kupiga kura, “ni wajibu wako wa kuwachagua Raisi, Mbunge na Diwani watakao leta maelewanao, Mshikamano, Utulivu na Amani”amesema Jalala.
Ameyasema hayo katika swala ya ijumaa leo masjid Ghadiir-Kigogo Post –ar es salaam, na kusema kuwa kitendo cha kumwita mwenzako kua ni kafiri ni kusema kua damu Yake ni halali kumwagwa,na mali yake ni halali, nahii ni hatari jamii kuitana majina mabaya, majina ambayo yatasababisha damu ya mwenzio kumwagwa, na kumuhukumu kuingia motoni.

 “kuitana majina mabaya ni kuigawa jamii, na hakuna sababu ya kuitana majina mabaya wakati waislaam wote wanasema Laailaha Illa Allah, Muhammada Rasuulu llah,”kitendo cha mtu kumkiri mungu na mtume wake ni Heshima kubwa “ amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala amewataka waislaam na watanzania kwa ujumla kuwa kwayale yanayotendeka katika nchi za kiislaam, na Afrika za kuhatarisha amani kwa kujiripua na Kukufurishana na  mtu anaejita muislaam kua huo si uislaam na wala uislaam hauelekezi hayo,

 “Mwenye jina zuri la kiislaam kuingia katika msikiti na kujiripua na kuwaua waislaam Na Wakristo pamoja na watu wasiokuwa na hatia au kukamatwa mateka kwa wanawake na kuuzwa sokoni, ni uislaam upi unaoruhusu wanawake kuuzwa? Tunasoma katika vita ya jamali, uhudi, hivi ni vita gani wanawake waliuzwa? Uislaam gani wanaouonyesha hawa? Aliuliza Sheikh Jalala.

Sheikh Jalala amewausia waumini kuuusoma uislaam halisi wa mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuuhubiri kwa watu, na kuachana na huu uislaam wa chinja chinja na wa kuleta fakra kwa watu na jamii,
Hatahivyo Sheikh Jalala alihoji kuwa hivi hiki kibali cha kuwaingiza watu motoni wamekitoa wapi? Ni mwenendo wa mtume kweli hata wale wasio waislaam kuwaita makafiri? Laa hapana bali mtume (s.a.w.w) alikua akiwaita kwa majina mazuri, ndio maana hata katika mjadala na wakristo wa Najran, mungu aliwaita ya Ahlal kitab, iweje mwislaam mwenzio umuite kafiri?

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayofanyika Julai 25, 2015  Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.

Amesema Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Aidha, amesema  kutakuwa na  Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua kutoka kwa viongozi wa

Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
  
Ameongeza kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo  Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo mbalimbali yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi ya vituo hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.

Akizungumzia baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji wa waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema kuwa Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.

Amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua watumishi hao wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na vurugu zinazoweza kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji wananchi inatakiwa kuanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa tarehe zilizopangwa.

Kuhusu taarifa za uwepo wa baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji wasiohusika kusimamia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji hao kuacha mara moja tabia hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na kwamba hatua kali za kisheria  zitachuliwa dhidi yao.

Pia amevitaka Vyama vya siasa kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au kuvaa mavazi yanayoashiria kampeni za siasa ili kuepusha vurugu.

MAGUFULI Kama ACT-Wazalendo





Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Kibaigwa, Mkoani Dodoma asubuhi hii, wakati akiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Mkoani  Dodoma.


Monday, July 20, 2015

RASMI--MOSES MACHALI WA NCCR KUPOKELEWA ACT KESHO

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,kesho julai 21 atampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses  Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye atajiunga atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.


Machali ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna  wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini.,
Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini  yenye jumla ya kata 15 za uchaguzi
Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti wa matawi  101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648.wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini
Baada ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya jumamosi julai 25.
Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi
Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama tofauti.

Abdallah Khamis
Afisa Habari -ACT-Wazalendo.
 Imetolewa leo julai 20/2015

Darsa la kwanza la Ujue Ushia-Tanga, Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akisalimiana na Waumini katika Mkoa wa Tanga ya Lushoto.
Muhadhara wa UJUE USHIA kwa mara ya kwanza ulianzia
 Mkoani Tanga wiliya ya Lushoto huko Mlalo mwaka 2012 
chini ya Uongozi wa Sheikh Hemed Jalala, kazi hiyo ilileta
 muamko mkubwa mno kwa wafuasi wa dini ya Kiislam 
Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah pamoja na 
Madhehebu ya Sunni, ilipofika tarehe 17/06/2012 Uongozi 
wa harakati za UJUE USHIA chini ya Sheikh Hemed Jalala 
 ulifanikiwa kuitisha mkutano mkubwa wa Mashia 
wanaoishi 
Dar es Salaam kwa ajili ya kutambuana na kujadili 
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Kishia Tanzania.
Tunaweza kuona ni kwa mda mchache sana jamii ya Kishia iliweza kutembea katika sehemu mbalimbali na kufikisha ujumbe halisi wa dini ya Kiislam aliyouacha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunajukumu kubwa la kuitunza kazi hii iliyoanzishwa na waasisi hawa. Tusikubali hata siku moja mtu atushawishi kuivunja kazi hii ambayo imetuletea heshima katika jamii yetu
Kiongozi huyo akiwa katika Darsa la Ujue Ushia na waumini wa Mkoa wa Tanga

Wakwanza kulia ni Alhaji Sheikh Mputa akiwa makini kusikiliza Darsa la Ujue Ushia

Wapili kushoto ni Mwanaharakati wa Afroshia Mr. Ibrahim Mpiripiri akijumuika na wenzake katika kusikiliza darsa hilo

Sheikh Salim Mwamba akiwa msitari wa mbele katika kuwaelewesha waumini wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya

Sheikh Hoza akiteta jambo na wazee wa Mji huo huko Tanga ya Lushoto

Sunday, July 19, 2015

Swala ya Eid-Fitri, (Mashia) Kiwanja cha Pipo

Sheikh Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Abdallah Seif akiwaswalisha Maelefu wa Waumini wa Dini ya Kiislam,Swala ya Eid-Fitri, iliyoswaliwa Siku ya Jumamosi ya Tarehe 18/07/2015, Sawa na 1/Shawaal/1436, katika kiwanja cha Pipo, Kigogo Jijini Dar es salaam.

Wanawake wa Kiislam wa Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania wakiwa mbele katika msitari wa kwanza kuhakikisha wanaswali Swala ya Eid -Fitir kwa pamoja






Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mh.Brigedia Simba akiungana na Waislam Duniani katika Swala ya Pamoja ya Eid-Fitri
Katikati ni Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar es salaam wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Suleimani Sarahani

Katibu wa Msikiti wa Ghadir Kigogo-Post,Kulia Sheikh Salim Swamba akiungana pamoja na Waislam Wengine katika Swala ya Eid- Fitri kwa Pamoja