Friday, July 17, 2015

Hawzat Imam Swadiq yafanya Mashindano ya Qur,an

Katikatini sheikh Muhammed Abd Jiji akishirikiana na wanzake wa Mwisho kulia ni Sheikh Muhammed Yusuf
Hawzat Imam Swadiq Chini ya Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala imefanya leo lMashindano ya Usomaji wa Qur,an katika Msikiti wa Ghadir, Kigogo-Post Dar es salaam
Sheikh Muhammed Abdi akisalimiana na Mzee Machitogo baada ya kumaliza Program ya Mashindano Ya Usomaji wa Qur,an

 Katika Mashindano hayo waliokuwa Majaji ni Naibu Mkuu wa Hawzat Imam Swadiq(a.s) Sheikh Muhammed Abdi, Sheikh Muhammed Yusuf na kadhalika
Mmoja wa Washiriki wa Wanafunzi Wakike wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) akishiriki katika mashindano hayo.

Baadhi ya Wanafunzi, Wanaharakati na Waumini wengine wakiwa makini kufuatilia Mashindano hayo ya Qur,an


Hawa ni baadhi ya washiriki wakiimba Qaswida baada ya Mashindano ya Qur,an


Majaji wakiwa makini kufuatilia waliofanikiwa kuingia katika mashindano ya Qur,an aliyeshika maiki ni Sheikh Muhammed Abdi

Wednesday, July 15, 2015

Sheikh Alhad Mussa aguswa na Siku ya Quds

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Alhad Mussa akitoa hotuba yake juu ya kulaani Uvamizi wa Kimabavu wa Wazayuni.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na waislam wa dhehebu la shia kwa waialam pamoja na watu wote wanaopinga dhuluma na uonevu mbalimbali duniani,semina iliyofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waumini wa dini ya kiislam pamoja na dini zote na wapinga uonevu wote.
Waumini wa Kike wakijitokeza kulaani uvamizi wa Wazayuni huko palestina katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya Quds

Wanaume nao wakiwa msitari wa mbele katika kuongoza matembezi ya amani ya kupinga Dhulma,unyanyasaji na Ukandamizaji unaofanyiwa watu wa palestina na Duniani Kote

Mabalozi kutoka nchi mbalimbali hapa Tanzania nao wakiwa pamoja na wananchi wa Tanzania katika kuwaunga Mkono suala la Siku ya Kimataifa ya Quds, katika Semina iliyofanyika Karimjee

Akizungumza katika semina hiyo mgeni rasmi ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa siku ya QUDS ni siku ya watu wote na madhehebu na dini zote na sio siku ya wapalestina pekee kwa sababu ni siku ambayo inatumika kupinga kwa sauti moja uonevu wowote ambao unaendelea katika mataifa mbalimbali duniani.
Amesema kuwa sisi kama Taifa la Tanzania ni siku muhimu ya kutafakari amani ya dunia ikiwa ni pamoja na kupinga kwa sauti moja dhuluma yoyote inayoendelea dhidi ya watu wa palestina na mataifa mengine duniani.
Waumini hao wameanza kuadhimisha siku hiyo jana ambapo walifanya matembezi ya amani katika jiji La Dar es salaam kuwakumbusha watanzania juu ya kuiombea na kuisaidia nchi ya pelestina kutoka katika machafuko ambayo yanazidi kugharimu maisha ya watu

Tuesday, July 14, 2015

Jambo la Palestina ni Jambo la Ubinaadamu-Sheikh Hemed Jalala.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habarileo  jijini Dar es salaam

 Habari Kamili

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Jambo la Palestina ni Jambo la Ubinaadamu, matatizo wanayowakumba ni kwa watu wote bila kujali dini zao.
“Jambo muhimu la Paletina ni kuuwaunganisha Waislam na Wakristo Duniani na kusema kuwa jambo la Palestina sio jambo la Kidini bali ni jambo la kila mtu mpenda amani na utulivu na maelewano ya Kibinaadamu.” amesema Sheikh Jalala.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo huwadhimishwa kila siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Sisi kama Viongozi wa Dini tumeshaanza harakati kabambe za kuwatembelea baadhi za Maskofu, Wachungaji, makanisani kwao lengo la kuwatembelea Maskofu pamoja na Wachungaji ni kuleta Ukaribu na kuwafundisha watanzania kwamba Uislam hausemi ya kwamba Mkristo ni Adui yetu, bali Uislam unasema Mkristo ni ndugu yetu”amesema Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh Jalala amesema Qur’an imetamka waziwazi kwamba watu waliokaribu mno na waislam ni wale waliuosema sisi ni wakristo.



Sunday, July 12, 2015

QUDS ni siku ya Amani


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari katika Matembezi ya Aamani ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

 Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waisla Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Siku ya Quds ni siku ya amani, ni siku ya kunyanyua sauti dhidi ya Dhulma, dhidi ya watu ambao hawana uhuru.
“Nasema ni siku ya amani kwasababu siku hii ya leo ilitangazwa kimataifa kwamba ni siku ya kukumbuka matatizo yanayowakumba ndugu zetu walioko katika ardhi ya Palestina...
Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh Hemed Jalala akigawa bendera za tanzania na palestina kama ishara ya kuanza rasmi kwa matembezi hayo  jijini Dar es salaam.
Inatambuluka ya kwamba ardhi ya palestina ni ardhi iliyokaliwa kwa mabavu ni ardhi iliyokaliwa pasina ridhaa ya wenyewe, wapalestina wakafukuzwa katika nchi yao ambayo ndio nchi yao ya Asili.
Naleo hii tukiwazungumza wapalestina hawa kama wanaadamu wenzetu wapo katika nchi tofauti wamegawanyika duniani, gurupo wapo mashariki ya kati wengine wapo nchi za ulaya, bali hata katika nchi zetu za afrika,watu hao wamejaa” alisema Sheikh Jalala. 
Jalal alisema Kitendo cha wao kutoishi katika nchi yao ni kitendo ambacho sisi kama Viongozi wa dini, sisi kama watanzania, sisi kama wadu wa amani ni jambo tunaona kwamba kwa kulinyamazia  sio mahala pake na ni jambo ambalo sio la kisawasawa.
“Tunasema ya kwamba ni haki ya mwanaadamu yoyote kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yake, kuzungumza anachoweza kukizungumza,kula na kuishi kama mwanaadamu mwingine, haya yote yamekosekana kwa watu wa palestina.
Waumini wa Dini ya Kiislam na Kiikristo Pamoja na Wapenda amani Duniani wakiungana katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya quds
Siku hii ya leo ndugu zangu ni siku ambayo tunakumbuka sote duniani ya kwamba kama itakosekana amani, basi busara itakosekana, hekima itakosekana, na utulivu utakosekana. Sisi kama Watanzania ni haki yetu kuwaunga mkono wapalestina na kuwaombea mungu kwamba amani iwepo kama iliopo hapa Tanzania, alisema Sheikh Jalala
Aliongeza kuwa Kama ilivyokuwa Tanzania ni mahala pa amani hapamtofautishi mwislam wala mkristo watu wote tumekaa pamoja, amani hii, maelewano haya na utulivu huu , siku hii ya Quds tunaomba Palestina iwe katika hali hiyo na iwe katika mazingira hayo.
Kitendo cha Dhulma kilichowakumba Wapalestina sisi kama watanzania  ni haki yetu kisimama na kusema ya kwamba, kwa kuwa mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere Mwasisi wa Taifa hili alikuwa mtu wa kwanza kuupinga dhulma na Uvamizi wa Palestina.

Thursday, July 2, 2015

SERIKALI YA KIKWETE YAJIKANYAGA UMEME VIJIJINI

SERIKALI imejigamba itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kupeleka nishati ya umeme vijijini. Charles         Mwaijage, naibu waziri wa nishati na madini, ameliambia bunge mjini Dodoma, kuwa serikali inaendelea kukarabati njia za umeme katika wilaya zote nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Mwijage alikuwa akijibu swali lililoulizwa na mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR- Mageuzi), Moses Machali. 
        Katika swali lake la msingi, Machali alitaka kujua kama 

serikali haioni umuhimu kukarabati nyaya, mita na vifaa vingine ili kuhakikisha umeme takribani megawati 2 hazipotei kama ilivyo sasa.
        Machali alitaka kufahamu utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyotoa bungeni katika mkutano wa bajeti wa mwaka 2013 ambako iliahidi kusambaza umeme katika vijiji vya Nyumbigwa, Murufiti, Kidyama, Herujuu Mganza, Ruhita na Kanazi. 
       Mwijage amesema vifaa vya kujenga miundombinu ya umeme vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi na vinaendelea kupelekwa Kasulu ambapo wateja wanaendelea kuunganishiwa umeme.
        Amesema  umeme unaozalishwa haupotei kama ilivyokuwa hapo awali baada ya wateja 4,400 kuunganishiwa umeme hivyo kufanya wateja 4,700 kunufaika na huduma ya umeme kwa sasa kutoka wateja 300 mwaka 2011.

PROFESA MWANDOSYA HAFAI KABISA URAIS

WAZIRI asiyekuwa na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya (pichani)imeeleza ni mchafu na hafai kwenye nafasi ya Urais.(Mtadandao huu unaripoti) anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
   Profesa Mwandosya ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki ni
 miongoni mwa Makada wa chama cha Mapinduzi CCM walijitokeza na kutaka nafasi ya Urais ikiwemo kuchukua fomu na sasa yuko kwenye Mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani Zanzibar –
           Akitafuta Udhamini  imebanika ni mtu ambaye anatajwa kuwa asifikiliwe kwenye nafasi hiyo kubwa ya nchi kutokana na kukumbwa kashfa mbali mbali .
     Miongoni mwa Kashfa ambazo zinatajwa kummaliza Profesa mwandosya ni ile ya Ubinafsishaji Shirika la Ndege (ATC)pindi alipokuwa Waziri Mawasiliano na Uchukuzi kwenye Utawala wa Awamu ya Tatu wakati wa utawala wa Rais Benjamini Mkapa  huku shirika hilo likiwa linauwezo wa kijiendesha lenyewe na kubinafsishaji huo  ikapeleka shirika hilo kufa.
         Mbali na Ubabe wake huo kwenye Shirika La ATC pia Mwandosya anatuhumiwa pia kubinafsisha Shirika la Reli (TRC) wakati wa Ubinasfishaji huo ulioleta maneno mengi,ambapo kwa mijubu wa wachambuzi wa Mambo wanasema Ubisfishaji wa Shirika hilo ulikuwa wakurupuka na ulikuwa unamaslahi Binasfi ya Kiongozi huyo.
          Vilevile Profesa Mwandosya wakati huo huo akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi anatuhumiwa pia Kubinasfisha Kampuni ya Wazawa ya Simu ya (TTCL) Kwa kampuni ya NSI Detecon na Celtel bila kufuata vigezo ambapo mpaka sasa Shirika hilo lipo hoi na mda wowote litakufa kutokana na kuhelemewa na madeni.
         Profesa Mwandosya wakati akitangaza nia ya Urais ndani ya CCM mkoani Mbeya alijisifu na kusema atapambana na Rushwa ambapo pia anaTuhumiwa kwa Kashfa  nyengine ni ile ya kusomeshewa Mwanae  na watu waliouziwa kampuni kwa Bei ya kutupwa  jambo hilo ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya Habari kwenye miaka 2001 hadi 2005.

    “Mimi nilipomsikia akisema yeye atapambana na Rushwa nilicheka sana mtu huyu alipokuwa Waziri wa Uchukuzi alifanya uchafu kama ule yaani mashirika yote ya Umma ameyabinasfisha ambayo yalikuwa bado yanafaa kuendeshwa  na umma harafu anataka urais mimi nakwaambia huyu mtu ni hatari sana”ameeleza Said Ally mkazi wa Ilala.

Tuesday, June 30, 2015

Waislamu waungane dhidi ya magaidi

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuungana na kushikamama Waislamu dhidi ya mirengo hatari ya kigaidi.

Ayatullah Akbar Hashimi Rafsanjani ameashiria suala la kuweko mirengo hatari ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Syria, Iraq, Afghastan, Pakistan na nchi nyingine kadhaa na kueleza kuwa: 
Kushikamana kwa Waislamu na kujizuia na uhasama na mashindano yasiyo na mwelekeo ni moja kati ya njia nzuri za kupambana na mirengo hatari ya ugaidi. Ayatullah Rafsanjani ameongeza kuwa: 
Makundi hayo ya kufurutu ada yanafanya ukatili mkubwa na tunashuhudia namna makundi hayo yalivyouzidishia masaibu ulimwengu wa Kiislamu na kuchochea hitilafu za kidini na migawanyiko kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu.  Chanzo IRIB