Sunday, December 4, 2016

“Waelezeni watu Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni Uislam wa Huruma” Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akisisitiza jambo juu ya Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Uislamwa Huruma.
TAARIFA KWA UMMA WA KIISLAM
Sikuambii Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa Waumini wa Kiislam mpaka akafikia mahala akasema “Yoyote mwenye kukiri Mungu ni Mmoja, mtu huyo ataingia peponi”hii ndio huruma ya Mtume (s.a.w.w) na Uislam aliotuletea.

Sasa ndugu yangu wewe unapata wapi fatua, unapata wapi Rai, unapata wapi Aya na Hadith za kumuambia mwenzako huyo ni Mtu wa Motoni wakati anasema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo umeipata wapi?

Ni kwa mantiki gani unaetoa fatua ya kuuwawa Yule ambae unaetofautiana nae na yeye anasema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo umeipata wapi?

Unapata ujasiri upi wa kuchukua mkono wako ukamuua mtu anaesema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah)ujasiri  huo umeupata wapi?

Unatoa kwenye Qur’an gani fatua ya kuvaa bomo kwenda kulipua ndani ya Msikiti watu wanaosema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo umeipata wapi?

Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bado haujulikani, Mnayo kazi ya kuwaeleza watu Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Uislam wa Huruma.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala.
Ijumaa, 02-12-2016.





Thursday, December 1, 2016

"Yoyote ambae anafikra ya kwamba Uislam ni dini ambayo haina huruma huyo atakuwa hajautambua Uislam",-Sheikh Jalala.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
MAADHIMISHO KIFO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) MWEZI 28, SAFAR 1438.

Napenda kuanza na mazungumzo yangu katika Qur’an Mungu ansema “Hatujakutuma ewe Muhammad (s.a.w.w) ila ni huruma kwa viumbe wote” siku hii ya leo ya mwezi 28,mfungo tano kwa kalenda ya Hijiria ndio siku ambayo Kiongozi wa watu wote duniani, kiongozi wa Waislam Mtume  wetu Muhammad (s.a.w.w) ndio ameaga dunia.

Weusi huu mnaouona, matembezi haya ya amani mnayoyaona yote ni kwasababu ya kukumbuka kifo cha mtukufu na mtakatifu Mtume Muhammad (s.a.w.w), Lakini lakujiuliza kubwa ni kwanini mtu huyu tumkumbuke katika kifo chake, zaidi ya miaka 1400 iliyopita. 

Sababu kubwa ya kukumbuka kifo cha Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuna sababu nyingi mmno, lakini niseme sababu mbili tatu kwa harakaharaka, Sababu ya kwanza kama anavyosema Mwenyezimungu katika Qur’an kwamba “Wewe tumekutuma ukawe ni huruma kwa watu wote” sio huruma kwa Waislam, 

Sasa unapomuangalia Mtume Muhammad (s.a.w.w) wakati bado yupo hai, akiwa yuko katika mji wa makka na baada ya kuwa madina, tulimpata mtume alikuwa na huruma kwa watu wote, mtume alikuwa huruma kwa wasiokuwa waislam, mtume alikuwa na huruma kwa waislam, mtume alikuwa huruma kwa wtu waliokuwa wanaabudu masanamu, kwa watu waliokuwa wanaabudu lata, wanaabudu manata na wanaabudu hubal,
Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kigogo Round About, Leo Jijini Dar es salaam.Ambayo yalianzia Ilala Boma hai Uwanja wa Pipo Kigogo.

 hawa walikuwa ni waungu wakiabudiwa na warabu, lakini mtume aliishi vizuri na alikuwa ni huruma kwa watu hao, mpaka amana za watu hao aliziweka katika  nyumba yake,
Mtume alipokuwepo maka na madina vilevule alikuwa na huruma kwa Ahlulkitab / Wakristo, yaani alikuwa ni huruma kwa Wakristo, alikuwa na huruma kwa mayahudi na alikuwa ni huruma kwa watu wenye dini zote.

Naamimi ya kwamba huruma hii aliyokuwa nayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) kabla hajaondoka duniani, naamini ya kwamba Watanzania na walimwengu huruma hii wanaihitajia.
Leo hii tunapotembea matembezi haya ya amani kwa ajili ya kukumbuka Mtume Muhammad (s.a.w.w) kifo chake, kubwa la kulienzi ni hili la Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) inahitajika na ni muhimu, 

Naamini yakwamba Watanzania wote wanahitajia huruma aliyokuwa nayo mtume, huruma ambayo haikumfanya Mtume asiwapende wasiokuwa waislam.

Huruma ambayo ilimfanya mtume akae meza moja na Wakristo katika ardhi ya madina, Huruma ambayo ilimfanya Mtume akae meza moja na Mayahudi, huruma ambayo ilimfanya Mtume akae na Wakristo / Ahlulkitabu.

Naamini yakwamba leo hii Waislam watanzania Masheikh na Maimam na Maustadhi wanayonafazi kubwa yakumuenzi Mtume katika kukaa kwao na Wachungaji, wao na Maaskofu, wao na Mapari, wao na wenzi wao ambao wanatofautiana nao kidini, Naamini ya kwamba Matembezi haya yawe ni chachu yakuwafanya watanzania wote waiige huruma ya Mtume,

 ambayo huruma hiyo ilikuwa haimbagui mtu, huruma hii leo hii inahitajika mahala pakubwa.Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa ni huruma kwa watu wote kwanini kwasababu alikuwa na huruma na watu.

Jambo la pili Mtume ambae tunamkumbuka leo hii, ni mtume alieng’ang’ania na alieenzi Umoja kabla ya mtume hajaondoka makka alitengeneza umoja kati ya maswahaba wake, na alipoondoka makka kwenda madina vile vile akatengeneza umoja kati ya wakazi wa madina (Answar) na kati ya watu waliotoka Makka(Muhajirun).

Akatengeneza Umoja kati ya makabila mawili yaliyokuwa yanavutana kabila la Ausi na Azraj, akatengeneza umoja wa Kidini ndani ya ardhi ya madina,naamimi ya kwamba leo hii, uwepo wa umoja wa Kidini ndani ya ardhi ya Tanzania,kipindi hiki ambacho huruma imekosekana , 

kipindi ambaho kuvumiliana kumekosekana, naamimi ya kwamba mafunzo haya Mtume Muhammad (s.a.w.w) yanahitajika leo hii kwa Watanzania na watu wote bila ya kuwabagua waislam wala wakristo wote wanahitajia umoja huu, wanahitajia kuishi huku kwa pamoja ameyoyafunza Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Nimalizie kwa kusema yoyote ambae anafikra ya kwamba Uislam ni dini ambayo haina huruma huyo atakuwa hajautambua  Uislam, yoyote ambae anafikiria ya kwamba Mtume alikuwa ni mtu wa Misimamo ya kutisha ambayo hawezi kukaa na watu hayo hajamtambua Mtume. 

“Kwasababu ya huruma uliyokuwa nayo ewe Muhammad (s.a.w.w) watu wote wameweza kukukubali, umeweza kukaa na Wakristo, umeweza kukaa na Mayahudi,umeweza kukaa na Mapagani na umeweza kukaa na watu wa aina zote”

Jambo la Mwisho Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama alivyoenzi Umoja, ulienzi utulivu, alienzi maelewano na alienzi amani, na ninaamini yakwamba Tanzania leo hii inayohaja kubwa yakuenzi Utulivu, yakuenzi Amani, yakuenzi Mshikamano watu kukaa pamoja, tofauti zetu za kifikra na za kimtazamo zisitufanye kutokuwa wamoja.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wanadini wote walioko Tanzania, wabariki Viongozi wa Dini wahubiri Upendo, Maelewano, Mshikamano pamoja na Amani katika nchi hii,Vilevile Viongozi wetu na Serikali ambayo inatusimamia katika mambo yetu. 

Imetolewa na:
Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
30-11-2016,Jumatano.







Sunday, November 27, 2016

“Wanaofanyiwa Ukatili wa Jinsia wafike Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto” ASP Matarimbo

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Kinondoni ASP Fatuma Matarimbo akitfundisha somo la Jinsia katika Warsha ya Mafunzo katika kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia-Mtaa/ wa Udoe/Masjid Udoe, Kariakoo-Bilal Muslim Mission of Tanzania, leo Dar es salaam.



Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi Kinondoni ASP Fatuma Mitarimbo ameitaka jamii ya Kitanzania kwenda katika Dawati la Jinsia na Watoto ili kupunguza matatizo mbalimbali yanayosababishwa na Ukatili wa Kijinsia.

“Jeshi la Polisi nchini lina vituo 417 vya Dawati la jinsia na Watoto Tanzania nzima, na watu wote wanakaribishwa katika vituo hivyo kuja kutoa taarifa ya matatizo yao ya Ukatili wa Kijinsia ili matatizo hayo tuweze kuyapunguza katika jamii yetu” amesema Mitarimbo.

ASP Mitarimbo amesema hayo leo katika Warsha ya mafuzo kwa Wajane, katika kuadhimisha siku ya 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia, katika Mtaa wa Udoe (Masjid Udoe), Bilal Muslim Mission of Tanzania, Kariakoo Dar es salaam.

Warsha hiyo iliandaliwa na Chama cha Wajane Tanzania / Tanzania Widows Association (TAWIA), ikishirikiana na WilDAF pamoja na Bilal Muslim Mission of Tanzania. ikiwa na Kauli mbiu"Funguka, pinga Ukatili wa Kijinsia, Elimu salama kwa wote"

Kuna aina kuu nne ya Ukatili wa jinsia ambayo ni Ukatili wa Mwili, ukatili wa Kisaikolojia, ukatili wa Kingono na ukatili wa Kiuchumi. “katili wa Kijinsia ni Kitendo chochote kinachoweza kumsababishia mtu mwingine kuwa na madhara, madhara hayo yanaweza kuwa madhara ya kimwili, kingono, kisaikolojia na Kiuchumi” amesema Mitarimbo

Aidha ASP Mitarmbo ametoa wito kwa Jamii kutoa taarifa katika Jeshi  Polisi kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto, Misikitini, Makanisani, kwa Viongozi wa Dini na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na Ukatili wa Kijinsia ili kupunguza ukatili nchini" amesema ASP Mitarimbo

Chimbuko la kuadhimisha siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ni kutokana na mauaji ya kinyama kwa akina dada watatu ambao ni wa Kilamabela ambao walikuwa wanaishi katika nchi ya Dominika, waliuuwa mwaka 1960, chanzo cha kuuwawa kilisababishwa na Wanaume zao ambao walikuwa wanapinga uongozi wa mbaya wa kiongozi wao Leonard Tujilo.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Tanzania tangu mwaka 2009, Jeshi la Polisi liliona kwamba ukatili wa Kijinsia umeshika usikani/ unakuwa, ukatili wa kijinsia ukawa ni chanzo cha makosa, ni chanzo cha watoto wetu kuzagaa mitaani, ni chanzo cha ndoa nyingi kutengana/kuvunjika na ni chanzo kikubwa sana cha kupoteza baadhi ya vioungo.


Hapo jeshi la polisi likasema hapana, likawa linatafuta namna ya kupunguza vitendo kama hivi, kwani mara nyingi vitendo kama hivyo vinafanyika kwa siri,hivyo jeshi la polisi likaona umuhimu wa kufungua Dawati la jinsia na watoto ili kuwapa nafasi akina mama, baba na watoto kuja kulalamika na kutoa dukuduku lao na kunapolisi ambao wamefundishwa vizuri na hawawezi kuja kutoa siri.





Kulia ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Kinondoni ASP Fatuma Mitarimbo akimuelezea mambo ya Kijinsia Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania / Tanzania Wisows Association (TAWIA) Madam Rose Sarwatt.

Thursday, November 24, 2016

"Ukitenda Mema, Haki na Amani utakuwa umemuenzi Imam Hussein (a.s) na Masih Yesu / Issa (a.s)"Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu  wa waislam  dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari nje kidogo ya ukumbi wa Semina wa Threatre One University of Dar es salaam.
Watanzania wametakiwa kuhakikisha kuwa wanadumisha umoja, haki na Amani iliyopo nchini ikiwa ni pamoja na kutenda mambo mema ili kuwaenzi kwa vitendo Immam Husein (a.s) na Masih Issa / Yesu (a.s) ambao walipambana duniani kuhakikisha kuwa wanasimamia haki katika Dunia kwa ujumla.

Wito huo umetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala  wakati wa semina maalum yenye anuani"Jitihada za Imam Hussein (a.s) na Masih Issa / Yesu (a.s) katika kueneza haki na amani Duniani.
 
Semina hiyo ikijadili kwa pamoja Jitihada za wawili hao katika kuleta Amani na utulivu pamoja na kuleta haki na usawa Duniani ambapo Jalala amesema kuwa watu hao ni mfano wa kuigwa kwa sasa hii ikiwa ni semina pia ya kuadhimisha Arobaini ya Mjukuu huyo wa Mtume Muhamad (s.a.w.w).
 
 Sheikh Jalala amesema kuwa Semina hiyo inalengo la kuweka ulinganisho kwa watu hao wawili ambao ni Imam Husein na Nabii Isaa ambaye ni Yesu ambao wote kwa pamoja walikuja Duniani kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye Dunia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Haki kwa watu wote,na kutetea wanyoonge na kufanya watu wapendane katika Jamii.
 
 Ameongeza kuwa ni wakati wa watanzania kuacha mambo mambo mabaya na kuanza kufanya matendo ya kiumpendaza mungu yakiwemo kupendana,kupinga dhuluma,na kutetea wanyonge ili kuhakikisha kuwa wanawaenzi viongozi hao wa Kidini waliopambana kwa ajili ya dunia.

Friday, November 4, 2016

Johnson: Magaidi 130 wa Uingereza wameuawa nchini Syria

Boris Johnson ameliambia Bunge la Uingereza kwamba, karibu Waingereza 850 wamekwenda Syria na kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh tangu mwaka 2011 na kwamba karibu nusu yao wamerejea nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kuwa, idadi ya raia wa nchi hiyo wanaojiunga na kundi la Daesh na makundi mengine ya kigaidi huko Syria imepungua na kuongeza kuwa, propaganda za kundi la kigaidi la Daesh zimepungua kwa asilimia 70 kuanzia mwaka jana wa 2015.
Boris Johnson amesisitiza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh linadhoofika siku baada ya siku na kwamba kundi hilo litaangamizwa kikamilifu baada ya kukombolewa mjini wa Raqqa nchini Syria ambayo ndio ngome kuu ya magaidi hao.
 
  Serikali ya Syria na washirika wake wanapambana na wapiganaji wa makundi ya kigaidi hususan Daesh na Jabhatu Nusra ambayo yaliingia nchini humo kwa msaada wa nchi kama Marekani, Saudi Arabia, Uturuki na washirika wao

Mogherini: Ni haki ya watu wa Ulaya kuisusia Israel

Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya amesema kuwa ni haki ya watu wa nchi za bara hilo kuisusia Israel. 

Federica Mogherini ambaye alikuwa akijibu maswali ya mwakilishi wa Ireland katika Bunge la Ulaya kuhusu harakati ya kuususia utawala wa Kizayuni wa Israel (BDS) amesema kuwa, haki ya uhuru wa kujieleza watu wanaotaka kushiriki katika kuisuia Israel inapaswa kuheshimiwa. 
 
Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, Ulaya inaunga mkono na kutetea uhuru wa kujieleza wa jumuiya mbalimbali ikiwemo ile ya kuisuia Israel.

Federica Mogherini ameyasema hayo akijibu maswali ya mwakilishi wa Ireland katika Bunge la Ulaya, Martina Anderson ambae ni miongoni mwa watetezi wa haki za Wapalestina. 

Anderson alimtaka Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya, Bi Mogherini aweke wazi misimamo yake kuhusu harakati ya kuisusia Israel barani Ulaya maarufu kwa kifupi kwa jina la BDS.
 
Msimamo wa wazi wa Federica Mogherini wa kutetea haki ya watu wa Ulaya kuisusia Israel umekaribishwa kwa mikono miwili na harakati mbalimbali za kupigania ukombozi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel.

Russia: Marekani inalenga makazi ya raia Mosul, Iraq

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa mashambulizi ya ndege za kivita za Marekani na washirika wake yanalenga zaidi makazi ya raia katika mji wa Mosul nchini Iraq.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova amesema kuwa, mashambulizi ya Marekani na washirika wake katika mji wa Mosul katika mkoa wa Neinawa nchini Iraq yanawalazimisha raia kukimbia nyumba na makazi yao. Zakharova amesisitiza kuwa, Russia ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya ya raia wa kawaida katika mji wa Mosul.
 
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Iraq, Haidar al Abadi ameashiria harakati za Marekani na washirika wake huko Mosul na kusema kuwa, licha ya kutumia jina kubwa la eti muungano wa kupambana na ugaidi, Marekani na washirika wake hawajafanya lolote katika operesheni ya kukomboa mji wa Mosul unaoshikiliwa na magaidi wa Daesh.

Al Abadi amesisitiza kuwa, serikali ya Iraq haihitaji muungano wa huo na kwamba Wairaqi wana uwezo wa kukomboa ardhi na nchi yao wenyewe.

Jeshi la Iraq na makundi ya kujitolea ya wananchi tarehe 17 Oktoba yalianza operesheni kubwa ya kukomboa mji wa Mosul ambao unakaliwa na kundi la kigaidi la Daesh. Magaidi wa kundi hilo sasa wanazingirwa kila upande na operesheni hiyo inaendelea kwa mafanikio.