Sunday, June 18, 2017

Sheikh Jalala awataka Viongozi wa Dini kuwalinda Vijana na Ugaidi

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vijana wa Kata ya Kigogo katika Futari ya pamoja iliyowakusaya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu, iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Viongozi wa dini mbalimbali na serikali wametakiwa kuwa karibu na vijana ili wafundishwe  maadili mema wasije kuwa na fikra za ugaidi  baada ya kukata tamaa ya kukosa kazi. 

Wito huo ulitolewa jan Dar es Salaam na Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithanasheriya Tanzania, Sheikh Hemed Jalala, katika futari ya pamoja na vijana hao wa kiislam na wasiokuwa waislamu wa Kata ya Kigogo wakati  akizungumza nao kutambua lengo la uwepo wao.
 
Hawa ni baadhi ya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu wa kata ya Kigogo waliohudhuria katika Futari ya pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.
Sheikh Jalala, alisema vijana wa sasa wamejitenga na mambo ya kiroho wamekata tamaa ya maisha kwa kukosa kazi hivyo ni wajibu wa viongozi kuwa karibu nao kusikiliza changamoto zao.

"Vijana ni tunu ya taifa, ndio muhibili wa jamii kwani taifa ambalo halina vijana wenye maadili mazuri liko hatarini kuwa na vijana ambao wanaweza kujiingiza na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ugaidi.

Sisi kama viongozi ni wajibu wetu kuwa karibu nao kuwafundisha namna ya kuwa karibu na nyumba za ibada ili baadaye tuweze kuwa na vijana watakaoliendesha taifa letu la Tanzania,’’alisema.
 
Mwl. Kassim Hassan ambae pia ni Mdau wa mambo ya Kijamii kutoka shule ya Sekondari Kibondo akiwapa elimu vijana walioudhuria semina jana Kigogo jijini Dar es salaam.
Alisema vijana  watakapokuwa wamefundishwa kwamba Mungu ni mpenda amani  na kinachokubaliwa ni maelewano mazuri na sio ugaidi.

Hatahivyo Jalala, alisema dini ya kiislam haina mahusiano na masuala ya ugaidi ambayo ni kuuana na kuchinjwa kwani Uislam inafundisha Amani,mshikamano na maelewano kwa kila mtu.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vijana wa Kata ya Kigogo katika Futari ya pamoja iliyowakusaya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu, iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.

Hawa ni baadhi ya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu wa kata ya Kigogo waliohudhuria katika Futari ya pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.

Saturday, June 17, 2017

Sheikh Jalala tuwaonee Huruma Wapaletina, angalia picha za Semina

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Semina ya Quds, imeyowajumuisha Maimam, Masheikh na Maustadhi, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Pot Dar es salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Kiislamu (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) Sheikh Ghawth Nyambwa akiwasilisha mada yake katika Semina ya Quds, imeyowajumuisha Maimam, Masheikh na Maustadhi, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Pot Dar es salaam.
Bango likiwaonyesha Ujumbe mzuri wa Uislamu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni Uislamu wa Huruma. Tuwaonee Huruma Wapalestina, bango limelotumika katika Semina hiyo.
Maimam,Masheikh na Maustadhi wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zimezowasilishwa katika Semina ya Quds, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Semina ya Quds imeyowakusanya  Maimam, Masheikh na Maustadhi kutoka madhehbu mbalimbali ya Kiislamu, imeyofanya Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Maimam, Masheikh na Maustadhi kutoka madhehbu mbalimbali ya Kiislamu,Mkoa wa Dar es salaam wakiwa makini kufuatilia Mada mbalimbali zinazowakilishwa katika Semina hiyo ,imeyofanya Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.

Sheikh Jalala aitaka UN kuhakikisha Palestina inakuwa na Amani

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Semina ya Quds imeyowakusanya  Maimam, Masheikh na Maustadhi kutoka madhehbu mbalimbali ya Kiislamu, imeyofanya Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu  Shia Ithnasheriya Tanzania  Sheikh Hemed Jalala ameitaka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UN) kuiangalia nchi ya Palestina kwa jicho la karibu ili amani iwezekurejea kama ilivyo kwa nchi ya Tanzania.

Sheikh Hemed Jalala ameyasema hayo leo katika semina ya Quds yenye lengo la kuwakumbuka waislamu na Wasiokuwa Waislamu wote wanaoishi kwa kupata taabu nchini Palestina, ambapo ameeleza kuwa watanzania inabidi waoneshwe kusikitishwa na kupinga vikali dhidi ya mambo yanayoendelea nchini humo kwani kinamama wanakosa huduma za afya jambo linalopelekea kujifungua kwa taabu.
 
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Semina ya Quds, imeyowajumuisha Maimam, Masheikh na Maustadhi, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Pot Dar es salaam.
Maimam,Masheikh na Maustadhi wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zimezowasilishwa katika Semina ya Quds, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Sheikh Jalala ametaja hali ya hatari inayoikabili msikiti wa AQSWA ambao ni mali ya Waislamu hiyo na  kueleza kuwa hivi sasa Msikiti huo haumilikiwi na waislamu kwa asilimia miamoja pamoja na mali zake, bali unamilikiwa na Utawala Haramu wa Israel, hivyo umoja wa mataifa ni vyema ikafanyika juhudi kuirejesha haki hiyo kwa waislamu kwa amani.
 
 "Waislam na wasio waislam wamefukuzwa na Utawala haramu wa Israel katika ardhi yao halali ya Palestina kwani mpaka sasa Wananchi halali ya Palestina  hawaishi kwa amani ambapo hadi nyumba zao zinavujwa na wanafariki kwa kukosa huduma za afya" amesema Sheikh Jalala

Siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni siku ambayo Waislam, Wasiokuwa Waislamu na Wapenda amani wameiteua kuwa ni siku maalum ya kuwakumbuka wanyonge wa Palestina na duniani kote na kufikisha ujumbe kwa dunia kuwa wanahitaji kusaidiwa, hivyo hapa Dar es alaam Tanzania tutakuwa na maandamano maalum yatakayo anzia maeneo ya Ilala Boma wilaya ya Ilala mpaka katika kiwanja cha Pipo Kigogo Post, Dar es Salaam.
Maimam,Masheikh na Maustadhi wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zimezowasilishwa katika Semina ya Quds, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam

Sunday, June 11, 2017

Waislamu watakiwa kuwahurumia walemavu na wasiojiweza-Sheikh Abdi

Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akiongea na Waandishi wa Habari katika hafla ya Futari ya Pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
WAISLAMU nchini wametakiwa kuishi karibu na jamii husasan kuwakumbuka watu wenye ulemavu  katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.
 
Mbali na hilo, wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe na kuwafariji watu wenye ulemavu ambao wanahitaji maalum.

Wito huo uliotolewa jana wakati wa hafla ya futari ya pamoja na watu wenye ulemavu ilioandaliwa na msikiti wa Ghadir, kigogo Post, Dar es Saalam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi, alisema ili dhana ya uislamu ikamilike ni lazima kuwa karibu na jamii kwa kuijali kwa kuiongezea amani na furaha.

“Uislamu si kufanya ibada tu bali ni kuitazama jamii tunayoishi ni kwa namna gani tunaijali, tunaishinayo kwa amani jambo kubwa ni kuhakikisha tunaipatie amani jamii yetu”alisema
 Image may contain: 2 people, people smiling
 Aliongeza kuwa katika vitabu vya Quran aya nyingi zinazungumzia kufunya ibada na kufunga lakini nusu ya Quran hiyo inazungumzia namna ya kuishi karibu na jamii.

NaibNaibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi alisema miongoni mwa mambo ambayo vitabu hivyo vitukufu vinaonesha ni namna ya kuwajali watu na kwamba hiyo ndio hali ya uislamu.

“Mtu ambaye anayempendeza Mungu ni yule ambaye anawafariji watu wengi zaidi na kwamba mbele ya Mungu hakuna mkamilifu wala mtu bora  wote ni sawa hivyo ndugu zangu walemavu karibuni hapa na mjisikie nyumbani”alisisitiza.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kigogo, George Manyama, alisema katika bajeti ya serikali ya mwaka huu imewakumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwaondolea kodi vifaa tiba.

Alisema kinachosubiriwa ni utekelezaji wa bajeti hiyo na kwamba ni fursa kwa watu wenye ulemavu kuhakikisha wanapata mahitaji yao yote maalum katika sekta ya afya.

“Mimi ni Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu katika manispaa ya kinondoni hivyo ni wakati mzuri kuwataarifu kuwa kuna pesa zinatolewa na manispaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu kuondokana na hali ya umaskini na kaunza kujikimu”alisema.

Diwani huyo aliongeza kuwa katika fedha zilizotolewa na manispaa hiyo ni zaidi ya sh.milioni 32 kwa ajili ya vikundi 36 ambapo kati yao wapo watu wenye ulemavu.

Manyima alisema miongoni mwa changamoto katika utoaji fedha hizo ni upungufu na kwamba licha ya manispaa kupeleka fedha hizo katika benki kwa ajili ya mikopo kwa watu wenye ulemavu bado kuna masharti magumu ya kukopeshwa.

“Ninashukuru uongozi wa msikiti huu kwa kuwajali na kuwathamni watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika mkusanyiko wa pamoja kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kuwafariji ambapo misikiti mingi  hawafanyi hivi kama mskiti huu nasema nashukuru sana” alisema.
 
Naye Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi wilaya ya Kinondoni, Mussa Geuza, alisema hafla hiyo inasaidia kuwakutanisha watu wenye ulemavu na kutambuana.

Alisema watu wenye ulemavu wanachangamoto kubwa ikiwemo kujaliwa na kuthaminiwa na kwamba idadi kubwa wananyanyapaliwa na kwa utaratibu ambao wanaofanya uongozi wa msikiti huo ni lakuungwa mkono.

Image may contain: 2 people, crowd
Hawa ni baadhi ya Walemavu mbali mbali waliohudhuria katika Futari ya Pmoja iliyofanyika Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Hii ni fursa kubwa kwa sisi kutambuana na kufahamu taarifa rasmi kuhusu watu wenye ulemavu katika maeneo tunamoishi hivyo ninashukuru sana uongozi wa msikiti huu”alisema.

Muft Abubakar: Jamii inatakiwa kukemea vikali wanaopotosha jamii

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber
Jamii imetakiwa kuwakemea watu wenye fikra ya kupotosha ili nchi iendelee kuwa na amani ,utulivu na mshikamano.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber,amesema kuna  baadhi ya watu wanatumia mikusanyiko vibaya katika kupotosha umma hivyo ni busara kila mtanzania kukemea kwa nguvu zote.

Amesema  jamii inatakiwa kujenga  mahaba na nchi yao ili kuepusha migogoro na uvunjifu wa amani usio wa lazima.

“jamii ikijenga mahaba ya dhati itasaidia nchi kuwa sarama na watu kufanya kazi zao kwa amani na utulivu “
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es alaam akiongea kwenye hafla ya futar hiyo.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa amesema kila mmoja wetu aijenge nchi kwa kumtanguliza mungu na kuliombea.

“kujenga nchi yenye amani ni jukumu la kila mtanzania kwani amani ni kimbilio la kila binadamu na ndo maana kila kwenye machafuko maendeleo huwa duni tofautfi na nchi zenye amani”
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaamPadri JOHN SOLOMON akiongea kwenye hafla ya Futari hiyo

Kwa  upande wake Padri JOHN SOLOMON ,amesema amani ndiyo inaleta maendeleo endelevu katika nchi yeyote duniani.

 “amani ni tunu aliyotupa mwenyezi mungu hivyo ni busala kila kiongozi kuitngaza kwa nguvu zake zote  zote ili matunda haya yawe kwa vizazi vyetu”.

Friday, June 9, 2017

Hafla ya Futari ya Pamoja Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika Masjid Ghadir Kigogo Dar es alaam..

Mwinjilist wa Kanisa la #Pentecost Mr.Kamara Kusup akiongea katika Hafla ya Futari ya Pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaam Sheikh #Alhad Mussa akiongea katika Hafla ya Futari ya Pamoja Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Hafla ya Futari ya Pamoja Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Dini ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es alaam wakiwa makini wakisikiliza jambo katika Hafla ya Futari ya Pamoja Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Baadhidhi ya Wageni waalikwa katika Hafla ya Futari ya Pamoja Wajumbe wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, iliyofanyika jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

"Tutaendelea Kuiombea Tanzania yetu Amani "Sheikh Alhad

Sheikh Alha,  Mussa Mwenyeliti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es salaam, ambae pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongwa katika Hafla ya Futari ya Pmoja na Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, Masjd Ghadir, Kigogo Post Dar e salaam.
KAMATI ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, imesema itaendelea kuombea amani ya nchi na kwamba haitamvumilia mtu atakayehamamsisha watanzania wafanye fujo na kuvunja amani iliyopo.
 
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shekhe wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum alisema hayo wakati wa futari ya pamoja ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Chuo cha Kiislamu cha Imam Swadiq kilichopo Kigogo Post.

Alisema mtu anayehamasisha watu kuvunja amani kwa kijana kwa kisingizio cha dini, wanamtilia shaka imani yake kwani sio misingi ya dini.


Alifafanua kuwa dini zote zinaelezea umuhimu wa kuenzi amani iliyopo kwani hata salamu zao kati ya wakristo na waislamu zinatangaza amani kwa kila mtu.

"Waislamu wamekuwa wakizungumzia mahusiano mema kati yao na madhehebu mengine lakini pia mahusiano haya yanahitajika miongoni mwa madhehebu yaliyomo ndani ya dini yetu kama vile Sunni na Shia," alisema Shekhe Salum.

Aliongeza kuwa wapo watu wanaojihusisha na mambo maovu kwa kisingizio cha dini, ukweli ni kwamba hakuna dini inayomtuma mtu kufanya mauaji bali wanahamasisha kuenzi amani iliyopo na kupinga vitendo hivyo.
Image may contain: 2 people, people standing, beard, hat and text
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Hafla ya Futari ya Pmoja na Kamati ya Amani, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Naye, Kiongozi wa Shia Inthasheriya, Shekhe Hemed Jalala alisema malengo ya kuwakutanisha kamati ya amani ni kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla inakuwa na amani.

"Tunataka wakristo na waislamu kuendelea kuishi kwa amani, upendo na maelewano. Pia kwa ushirikiano wetu tutasaidia mkoa huu kuwa na amani na kuombea Taifa letu lizidi kuwa na umoja," alisema Shekhe Jalala.

Pia alisisitiza kuwa ni lazima kuombea amani isipotee kwa kuwa ndio sababu ya kuwa na uhuru wa kuabudu, kufanya kazi na mshikamano.