Monday, January 25, 2016

Wakazi Bonde la Mkwajuni wagoma kuondoka

Wakazi wa Bonde la Mkwajuni katika Mtaa wa Hananasifu na Suna, Manispaa ya Kinondoni ambao nyumba zao zilibomolewa, wanaishi kwenye eneo hilo licha ya kuendelea kuathiriwa na mvua.
Wakazi hao ambao hivi karibuni vibanda vyao vilibomolewa kwa amri ya Serikali, wameendelea kubakia na kujenga vibanda juu ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Nicolata Myanga alisema hawataondoka eneo hilo kwa kuwa Serikali haijawapa viwanja.
“Serikali kama inataka tuondoke ije itege bomu tu hapa tufe, tutakwenda wapi? Tunaambiwa tumepewa viwanja viko wapi? Hivi kweli mimi na uzee wangu huu nimepewa kiwanja naambiwa ondoka nitang’ang’ania hapa ili iweje?” alihoji Myanga mwenye umri wa miaka 68.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Magreth Dimoso alisema hali ya maisha yao inazidi kuwa ngumu kila siku, lakini mbaya zaidi ni kuwa kadri mvua zinavyonyesha hawana pa kukimbilia kwa kuwa hata baadhi ya vibanda walivyojenga vimesombwa na maji.
Mwathirika mwingine wa bomoabomoa hiyo, Anastatus Mponda alisema maisha yao ni magumu kuliko hata ya wakimbizi.

Kutokana na hali ngumu waliyonayo, baadhi yao wamegeuka kuwa ombaomba, kwani hata mwandishi wa habari hizi alipofika alilakiwa kwa salamu ya kuombwa Sh1,000 na Jumanne Iddy.
Maimuna Juma aliyekuwa amekaa nje ya kibanda chake akiwa anambembeleza mwanaye aliyekuwa akilia kwa sababu ya njaa, alipomuona mwandishi aliomba msaada wa fedha akamnunulie chakula.
Uongozi wa mtaa wanena
Mwenyekiti wa Mtaa wa Suna, Salumu Hamis alisema kuwa kuna kaya zaidi ya 700 zinaishi sehemu hiyo na kwamba, kati ya jumla ya kaya 900 zilizokuwa zinaishi hapo, 150 pekee ndizo zilipewa viwanja Mabwepande,” alisema.    

Waislamu Nigeria wakumbuka mauaji ya Zaria

Waislamu Nigeria wakumbuka mauaji ya ZariaWaislamu wa Nigeria wamefanya maandamano katika miji mbali mbali ya nchi hiyo kuadhimisha arubaini ya mamia ya ndugu zao waliouawa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria mwishoni mwa mwaka uliopita.
Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika mji wa Kano ambapo waandamanaji wamelaani mauaji ya mamia ya Waislamu wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria, huku wakitoa mwito wa kuachiwa huru mwanachuoni wa Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Aidha maandamano mengine kama hayo yameshuhudiwa katika miji ya Sokoto, Minna na Katsina. Hii ni katika hali ambayo, Binti wa Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, familia yao haina taarifa zozote kuhusiana na hatima ya baba na mama yao wanaoshikiliwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

Badia Ibrahim Zakzaky amesema kuwa, baada ya kupita siku arubaini tangu kutokea maafa ya Zaria ambapo jeshi la Nigeria liliwauwa mamia ya Waislamu, asasi za kimataifa zimeshindwa kuandaa mazingira ya yeye kukutana na baba na mama yake wanaoshikiliwa na vikosi vya usalama vya Nigeria.

Itakumbukwa kuwa, mwezi Disemba mwaka jana, wanajeshi wa Nigeria waliwavamia Waislamu wa mji wa Zaria, kaskazini mwa nchi hiyo na kuwaua kwa umati mamia ya Waislamu.
Vilevile walimpiga risasi kadhaa na baadaye kumkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.chanzo irib

'Kuwakamata wanajeshi wa Marekani ni ushujaa'

'Kuwakamata wanajeshi wa Marekani ni ushujaa'Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, hatua ya hivi karibuni ya jeshi la majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ya kuwakamata wanajeshi wa Marekani walioingia kwenye maji ya Iran kinyume cha sheria katika Ghuba ya Uajemi, ni kitendo cha kishujaa na kilichofanyika kwa wakati unaofaa kabisa.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo Jumapili wakati alipoonana na maafisa wa jeshi la Sepah na sambamba na kuwashukuru wanajeshi hao wa Iran amesema: Kwa hakika inabidi tulihesabu tukio hilo kuwa limefainyika kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu ambaye aliwafanya wanajeshi wa Marekani waingie katika maji ya Iran na wanajeshi wetu wachukue hatua ya haraka na ya kishujaa ya kuwatia mbaroni wanajeshi hao na kuwalazimisha kuweka mikono vichwani.
Itakukumbukwa kuwa, boti mbili za Marekani, tarehe 12 Januari 2016 zilikamatwa na wanajeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah baada ya kuingia kinyume cha sheria katika maji ya Iran na kuwatia mbaroni wanajeshi 10 wa Marekani waliokuwemo kwenye boti hizo.
Wanajeshi hao wa Marekani waliachiliwa huru baada ya kubainika kuwa waliingia kimakosa katika maji ya Iran.chanzo irin

Sunday, January 24, 2016

Sheikh Jalala "Vyombo vya Ulizi na Serikali, Uislam hauna Mahusiano na Ugaidi"

Mmoja wa Viongozi wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala amevitaka Vyombo vya ulinzi nchini pamoja na serikali kwa ujumla kutambua pamojana kuelewa kuwa vitendo vya ugaidi vinavyotokea nchini Poamoja na duniani kwa ujumla havina uhusiano wowote na dini ya kiislam kama jinsi ilivyokaririwa na wengi.
 
“Makundi mbalimbali kama Al shabab, Bokoharam, Daesh na mengineyo yote yanayojinasibisha na Uislam, ambao utawakuta wanabeba bendera imeyoandikwa Laillaha Illa llah, Muhammad Rasulullah, hao sio waislam,kwaniUislam hauruhusu kumwaga Damu ya Mtu.”amesema Sheikh Jalala


Sheikh Jalala amesema kuwa moja ya sababu ya Ugaidi ni kuwa na fikra ya Kukufurishana,ambapo inafikia watu wanaitana majina mabaya,na kukufurishana inamaanakuwa damu yake ni halali,ambapo ni kinyume na mafundisho ya Uislam ambao aliokujanao Mtume Muhammad (s.a.w.w).


“Dini ya Kiislam sio dini inayolingania mauaji bali ni dini inayolingania amani, maelewano,kuvumiliana, kuelewana, kuoneana huruma na mshikamano bila kujali itikadi za kidini, kikabila, kitaifa na wala kirangi, bali Uislam unalingania amani kwa watu wote” amesisitiza Sheikh Jalala.


Haya ameyasema leo katika Semina  inayozungumzia Changamoto zinazowakabili Ummah wa Kiislam nchini na Duniani kwa Ujumla katika Lamada Hotel, ambayo iliyoandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhar Foundation,chini ya Sheikh Khalifa Khamisi.


Aidha Sheikh amesema kuwa nchi ya Tanzania ni moja kati ya nchi chache duniani ambazo zinaishi kwa umoja na mshikamano pamoja na upendo wa hali ya juu hivyo semina hiyo itatumika kuwatahadharisha watanzania kuepuka sana kukaribisha vitendo vya kigaidi katika nchi yao kwani itasababisha hatari kubwa.


“Kuwa semina hiyo imekuja mahususi kuwakumbusha waislam jukumu lao la kujenga umoja miongozi mwao na kwa watanzania kwa ujumla jambo ambalo litasaidia katika kuendeleza umoja na mshikamano wa watanzania uliopo”.ameongeza Sheikh Jalala.

Hatahivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhar Foundation Sheikh Khalifa Khamisi amesema kuwa leo akipatikana mtu mmoja ambaye kavaa kanzu kafanya vitendo vya kigaidi basi inachukuliwa kuwa waislam woote ni magaidi dunian,sio kweli na hatufundishi ugaidi katika dini zetu,tunaomba vyombo vya dola kufuta mawazo haya mabaya juu ya uislam”amesema.


“Kwa sasa waislam wamekuwa Wahanga kwa kutuhumiwa kuwa wao ndio Magaidi kwa kuwa wanafanya mambo ya kumkera mwenyezi mungu kwa kuwafanyia wenzao mambo ya maovu jambo  aliendani na mafundisho ya Dini ya Uislam ambapo jambo hili sio kweli bali ni fikra pandikizi zilizopandwa na maadui wa Uislam”amesema Sheikh Khamisi.


Sheikh Khamis amesema kuwa dini ya kiislam haina mahala popote inapofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi,mauaji,na vitendo vya kinyama vinavyotendeka duniani hivyo ni lazima watanzania na dunia kwa ujumla kuacha kuamini kuwa vitendo vya kigaidi vinafanywa na waislam.







Sunday, January 17, 2016

Kitwanga atangaza vita ya bodaboda

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, CharlesWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema katika kuhakikisha Serikali inapambana na uhalifu, Jeshi la Polisi limeanza ukaguzi maalumu wa bodaboda na kufunga kamera za CCTV katika miji mikuu ili kufuatilia matukio mbalimbali.

“Kutokana na majambazi kubuni mbinu mpya kila siku, ikiwamo ya kutumia bodaboda kuvamia benki na wanaotoka benki na kuwapora fedha, kuanzia sasa bodaboda, hasa aina ya boxer zitasimamishwa wakati wowote na kupekuliwa,” alisema Kitwanga katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam.

Alisema polisi wameweka ulinzi maalumu na waendesha bodaboda watakaooneka kupakia kitu chochote na kukiweka mbele (katika tenki la mafuta) au kiti cha nyuma, watasimamishwa na kupekuliwa kwa maelezo kuwa maeneo hayo ndiyo hutumika kuficha silaha.

“Tunaomba wananchi watuvumilie kipindi hiki tukipambana na bodaboda kutokomeza uhalifu,” alisema.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya wananchi kuvamiwa na kuporwa fedha, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuzichukua benki huku wafanyakazi wa benki wakidaiwa kuhusika kutoa taarifa za wateja.

Mara zote majambazi hutumia bodaboda kufanikisha uhalifu huo, huku wakiwa na silaha ambazo huzitumia kutishia, kujeruhi na wakati mwingine kuua.
 
Tukio la hivi karibuni ni la Desemba 28 mwaka jana, ambako majambazi waliokuwa katika bodaboda walimvamia meneja wa operesheni wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Raphael na kumpora Sh10 milioni na kumuua kwa risasi.

Kuhusu ujambazi huo, Kitwanga alisema watu wanaovamiwa na kuporwa fedha, wengi hutokea katika benki za ndani si za nje.“... Hii inatokana na utaratibu wa malipo katika benki hizi. Kwa mfano, benki za nje ukiwa na hundi inapitiwa na watu wachache tofauti na benki za ndani ambazo hupitiwa na watu wengi.”

“Inawezekana katika mlolongo huo wa benki za ndani kukawa na wafanyakazi wanaoshirikiana na majambazi. Tunachokifanya sasa ni kuongeza ulinzi tu wa askari.”

Kuhusu CCTV, Kitwanga ambaye pia ni mbunge wa Misungwi alisema teknolojia hiyo itasaidia kubaini matukio ya uhalifu na kwamba tayari Serikali imeshazungumza na China kuhusu upatikanaji wa kamera hizo, “Ufungaji wa utaanza mwaka ujao wa fedha unaoanza Julai na tutaanzia Dar es Salaam.”
 
Alisema Jeshi la Polisi lina askari wachache ambao hawawezi kuwapo kila eneo, hivyo mpango wa kuweka kamera hizo ni kuhakikisha kila jambo linafuatiliwa kwa ukaribu.

“Wapo waliokamatwa wakituhumiwa kuhusika katika matukio ya kuwapiga watu risasi na kuwapora fedha. Baadhi yao wamekiri kuhusika na wengine wamekana,” alisema Kitwanga.

Alipoulizwa silaha zinazotumika zinatoka wapi, alisema, “wanazopewa raia kihalali hazitumiki katika matukio haya. Ni zile zinazoingia nchini kinyemela.”

Kuvamiwa vituo vya polisi
Alisema matukio ya kuvamiwa kwa vituo vya polisi yana harufu ya ugaidi: “Tanzania ugaidi haujakomaa na magaidi hawajawa na nguvu. Wanachofanya ni kuvamia kituo cha polisi, kuchukua silaha na kuzitumia kufanya uhalifu kupata fedha ili kuendesha maisha yao. Kuna dalili kubwa kwamba huu ni ugaidi.”

Alisema licha ya Serikali kuwakamata, wapo wanaoendelea kuingia nchini na ili kumaliza suala hilo ni lazima uwekwe mpango wa muda mrefu.

“Kwa sasa tunaendelea kujadiliana kuhusu mpango wa kutambua raia wetu na wanafunzi katika shule mbalimbali. Lazima tujue wangapi wameacha shule na wamekwenda wapi. Ugaidi ukikomaa katika nchi unakuwa tatizo kubwa.

“Magaidi hawatengenezwi nchini, wanatoka hapa (Tanzania) wanakwenda Somalia wanafundishwa na kisha wanarudi kufanya ugaidi. Lazima tutambue raia waliotoka Tanzania walikwenda nchi gani na kwa sababu gani. Bado tunajadiliana tuone tutaliendesha vipi jambo hili.”

Kitwanga alisema ili polisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi, ni lazima iwe na mfumo imara kuanzia makao makuu hadi ngazi ya chini (ulinzi shirikishi), akisema moja ya changamoto alizokumbana nazo baada ya kuteuliwa kuwa waziri ni dosari katika mfumo wa utendaji kazi.

Alisema nchi ina polisi 45,000 na kati yao wanaoishi kambini ni 10,000 tu na kwamba kuishi uraiani kunashusha nidhamu.

“Hii ni changamoto kwa sababu ukitaka kuwakusanya wote hutaweza maana wengi wanaishi uraiani. Rekodi za kimataifa askari mmoja anapaswa kulinda watu 350. Kwa Afrika askari mmoja analinda kati ya watu 500 hadi 700 lakini kwa Tanzania analinda watu 1,000 hadi 1,200,” alisema.

Alisema ili kufikia rekodi za kimataifa, nchi inapaswa kuwa na askari kati ya 95,000 hadi 100,000 na idadi hiyo itakuwa ikiongezeka kila mwaka. Mwaka huu askari 3,600 watahitimu mafunzo katika Chuo cha Polisi Moshi.    

Sunni na Shia Waungana pamoja Kusheherekea Mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Madhehebu ya kiislam Nchini kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,kukaa kwa pamoja na kujadili maswala yanayowahusu jambo ambalo litasaidia kuleta amani baina ya dini ya Kiislam na dunia kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim  wakati wa sherehe ya maalum ya mauled iliyowakutanisha waislam wa Madhehebu ya SHIA na SUNNI kwa ajili ya kusherekea na kukumbaka kwa pamoja siku ya kuzaliwa kwa mtume muhammad (s.a.w.w), Masjid Udoe  Jijini Dar es salaam.

“Sisi sote ni wana wa Mungu, na tuna muabudu Allah, kwa hiyo kuna mambo ya msingi yanayotuunganisha na kututenga ndiyo maana unaona masheikh wa Kisuni wanashirikiana na Washia,” alisema Sheikh Mkuu.

Sheikh Salim amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea kujenga chuki na uhasama baina ya madhehebu hayo bali jambo sahihi  ni kukaa kwa pamoja na kujadili mambo yanayowahusu na yale yatakayoshindikana kutokana na itikadi za kidini yaachwe ili yasiwe ni chanzo cha chuki mbalimbali.

“Licha ya tofauti tulizonazo ni tofauti zitaendelea kuwepo, lakini sisi sote ni Waislam kwa sababu sote tunaunganishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Upweke wa Allah (swt), Malaika, Siku ya Mwisho na Kusimamisha Swala,hivyo hakuna ulazima wa kulumbana na kutoshirikiana” amesema sheikh Mkuu.
Kwa upande wake Sheikh MSABAHA SHABAN MAPINA (SHIA) amesema kuwa sherehe ya kukutana kwa madhehebu hayo mawili yenye imani Tofauti tofauti ni jambo la kuigwa na Tanzania nzima pamoja na dunia kwani ni njia nzuri ya kujenga umoja wa kidini ambao ilikuwa umeanza kutetereka .

Sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zimeandaliwa Taasisi ya Kidini ya Kiislam ya Bilal Muslim Mission of Tanzania na Ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka BAKWATA TAIFA NA MKOA WA DAR ES SALAAM. Muft wa Tanzania Abubakar Zuberi, Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salim






Wednesday, January 13, 2016

Sheikh Jalala "Kitendo cha Serikali ya Saudia Arabia kumuua Sheikh Nimr ni jambo haliusiani na Dini ya Uislam"

Pichani ni Sheikh Hemed Jalala  ambaye ni Kiongozi wa chuo cha kiislam  cha Kiislam (Hawaza) Imam Swadig (a.s),  pia   ni mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa  wailsamu dhehebu la shia Ithna asherri ya Tanzania akizungumza na wahanabari hawapo pichani akilaani mauaji ya Mwanazuoni wa kiislam kutoka nchini sauda Arabia
"Katika Uislam na katika Maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Uislam unaruhuru Uhuru wa fikra, Uhuru wa kuzungumzo,Uhuru wa kuabudu, uhuru,na ndio maana Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakuwaua wale wote wapinzani wake ambao walikuwa watatofautiana katika Imani"

WAISLAM  nchini wamelaani vikali kitendo cha serikali ya Saudi Arabia cha kumuua mwanadhuoni  Ayotollah Sheikh Bagir Nimr ambaye alikuwa anawatetea wanyonge na waislam nchini humu.
 
       Akisoma  tamko la kulaani kitendo hicho, Sheikh Hemed Jalala  ambaye ni Kiongozi wa chuo cha kiislam  cha (Hawaza) Imam Swadig, Sheikh huyo pia  ambaye ni mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa wailsamu dhehebu la shia Ithna asherriya Tanzania
     Ambapo amesema waislam nchini wamepokea kwa masikitiko makubwa kwa  kitendo cha kinyama cha watu kumuua kwa kumchinja  hadharani mtetezi huyo baada ya kuhukumiwa kifo na serikali ya nchi hiyo.
 
     Amesema adhabu ya kifo aliyopewa mwanachuoni huyo ni ya kionevu kwani haendani na mafunzo ya dini ya kiislam.
      “Yaani huyo Sheikh Nimr amehukumiwa baada ya kutetea haki ya waislam ikiwemo kupata  haki ya kusari mara tano kwa siku ambayo nchini Saudi Arabi hawapati nafasi hiyo,amekuwa anatetea haki ambayo serikali yake ilikuwa haiwatendei haki wananchi wake,lakini leo serikali hii ikaona njia sahihi ya kumyamazisha ni kumhukumu kifo “amesema Sheikh Jalala.
Waislam wa msikitiwa Kigogo Post Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye sara ya kulaani unyama huo
     Sheikh Jalala akiongea kwa uchungu amesema inasikitisha kuona nchi kama Tanzania ambayo inamuunganiko wa dini mbali mbali lakini bado waislam wanapata haki ya kuaabudu mara tano kwa siku lakini nchi ya Saudi Arabia ambayo ni ardhi yake imetaliwa na dini hiyo lakini waislam hawapati nafasi ya kuabudu mara tano kwa siku jambo analosema linakwaza mtume Muhamed ambaye alitaka kila mtu apewa haki ya kuabudu.
 
     “Makosa yalitajwa na serikali ya Riyadhi juu ya Ayatollah Nimr na wenzake kwamwe hayakustahili adhabu hiyo,kumuua kiongozi mwenye wafuasi kwa kosa la kudai haki za wanyonge  ni kuchochea vurugu”amesema Sheikh Jalala.
 
    Sheikh Jalala amebainisha kuwa binadamu ni kiumbe aliyehuru kutokuwa na  minyororo ya ukandamizaji na utumwa katika Nyanja zote,yuko huru kutokuwa  na utumwa wa kifikra, huku akihoji ni kuwa ni kivipi karne hii ambayo uelewa juu ya masuala ya binadamu na maswala ya kielimu yameshika kasi kwanini yatokea mambo kama haya.


 
      Vilevile Sheikh Jalala ameitaka Dunia kuingilia kati vitendo vya kinyama vinavyofanywa na serikali ya Saudi Arabia kwa kunyima uhuru wa haki za kuishi pamoja na kutoa maoni.
   Mwanazuoni Ayatollah Sheikh Bagir Nimr aliuwa tarehe 2/1/2016 baada ya kutolewa hukumu na serikali ya  Saudi Arabia baada ya kuhukumu kwa kosa la kushiriki kudai hakiiii ya uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wao kwa kura badala ya kuongozwa kifalme,
 
Kosa jengine ni  kudai haki za binadamu ziheshimiwe kwa kuwa kuna matabaka  ndani ya nchi ynanyima haki zao za msingi,pamoja na kutolewa na kuachiwa huru wafungwa wakisaisa waliokamatwa kwa kudai mabadailiko ya kiungozi katika serikali na haki ya kuchagua viongozi wao.