Thursday, July 30, 2015

Umeskia Alichosema LISSU

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.

Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.

Sunday, July 26, 2015

Mwanamuziki 'Bongo Fleva' Khadija Shabani 'Keisha' ashinda CCM

MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya 'Keisha' ameibuka mshindi kwenye kura za maoni za Ubunge wa viti maalum kundi la Walemavu MKoa wa Dodoma na kuwa mshindi wa kwanza.
Keisha amepata kura 340 huku Stella Fueda akiibuka na kura 112, Anna Fungo kura 100 na Graceana Kavishe kura 54.

Jumla ya kura 721 zilipigwa ambapo kura 75 ziliharibika na kura za halali zilikuwa 646.

Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari na kubainisha kuwa japo ni mlemavu wa ngozi lakini anajikubali anajipenda kujiamini na amekuwa akipigania amani ambayo wanastahili kuipata kutoka nchini.

Alisema alipoanza kuweka picha zake za siasa kwenye mtandao kuna baadhi ya watu walimpongeza na wapo waliosema kuwa hana uchungu na wenzake kwani waliamini anaingia kwenye siasa kwa nia ya kujinufaisha “Wapo wanaohisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi
ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu” alisema.

Alisema fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa akimaanisha kuwa lazuima kusimamia sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima kuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.
  • Taarifa ya Sifa Lubasi, Dodom 
  • Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu mashabiki zangu na media zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia kitu.

    Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.

    Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.

    this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza kuchangia humo na kwa upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo ahsanteni shukrani.

Saturday, July 25, 2015

Kenyatta Amgomea Obama Kuhusu Ushoga

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametofautina mtazamo kuhusu ushoga na ndoa za jinsia moja na mgeni wake ambaye ni Rais wa Marekani, Barack Obama mbele ya waandishi wa habari. 

Akiongea mbele ya idadi kubwa ya waandishi wa habari katika eneo la Ikulu ya Kenya, Rais Obama alipinga kwa nguvu ubaguzi dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini Uhuru Kenyatta alikuwa ngangari na kumueleza kuwa utamaduni huo hauna nafasi nchini Kenya. 

Rais Kenyatta alifafanua kuwa suala la ushoga sio suala muhimu nchini humo na kwamba nchi hiyo inahitaji kujikita katika maeneo mengine ambayo ndiyo maisha ya kila siku ya wananchi. 

Obama aliingia nchini Kenya Julai 24 usiku na kupata mapokezi ya kihistoria katika nchi hiyo inayomchukulia kama mtoto wa nyumbani aliyerudi na taji la ukuu wa nchi kubwa yenye nguvu zaidi duniani.

Waislamu Marekani waandamama kuipinga Saudia

Waislamu wanaoishi Marekani wameandama mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington wakilalamikia jinai za nch hiyo na hatua ya nchi hiyo ya kuunga mkono ugaidi. 
Shirika la habari la Tasnim limeripoti kutoka Washington kuwa, maelfu ya Waislamu wanaoishi katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa Marekani jana walikusanyika kwenye maidani ya Watergate mjini Washington na kisha kuandamana hadi mbele ya ubalozi wa Saudia na kupiga shaari dhidi ya serikali ya Riyadh. 
Wafanya maandamano hao walikuwa wakipiga nara na shaari kama 
"utawala wa Aal Saud si tu si mwakilishi  wa Uislamu, bali ni muungaji mkono wa kundi la kigaidi la Daesh, machafuko na misimamo ya kufurutu ada.” Katika maandamano hayo, Hujattul Islam wal Muslimin Sheikh Abduljalil Imam wa msikiti wa Jaafariya huko Maryland Marekani ametoa hotuba na kulaani jinai za Saudi Arabia. 
Sheikh Abduljalil ameendelea kuhutubia kwa kusema wamekusanyika ili kuwaambia walimwengu kwamba iwapo wanatafuta chanzo cha magaidi basi wanapasa kukipata ndani ya utawala wa Aal Saud. 
 Amesema chimbuko la ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, huko Iraq na Syria ni utawala huo wa Aal Saud.
Chanzo Irib.

Angalia Obama alivyowasili Kenya

Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na dada yake Auma Obama huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwaangalia.

Mtoto Joan Wamaitha, 8, ndiye Mkenya wa kwanza kumkaribisha Rais Barrack Obama nchini humo kwa kumpa shada la maua na kupiganae picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya kwenda kulakiwa na mwenyejiwake Rais Uhuru Kenyatta.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Obama aliwasili nandege yake ya Air Force One.

Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.

Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.

Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.

Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.

Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiria mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.

Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi.

Siku yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani.

Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia. Source:BBC Swahili & AFP

Kujengea Makaburi Kwa Fikra za Kiwahhab (Answar Sunna) Ni Haram

Sheikh Abdullatwif Swalehe akito hotuba juu ya siku ya Huzuni kwa Kubomolewa Makaburi Matukufu
Sheikh Abdullawif Swalehe aliuliza kuwa kama Fatwa ya kupomoa Makaburi ni Sahihi, ni kwanini makaburi ya khalifa wa kwanza Abubakar na wapili Omar hayajabomlewa ambayo yamejengwa ndani ya msikiti?
Amesema kitendo cha Utawala wa Kiwahhabi (Answar Sunna) cha kutoa fatwa za kuhalalisha makaburi na sehemu tukufu za Mkumbusho ya Waislam kupomolewa , ni kitendo ambacho kinachopingana na Qur’an tukufu ya Allah (swt).
Hayo aliyasema Jana katika Maadhimisho ya Siku ya Huzuni (Majonzi) yaliyofanyika Msikitini Ghadir Kigogo-Post, Dar es salaam ambayo huwa yanafanyika kila mwaka katika tarehe kama hii ya Shawwal 8 1344.
“Jamii yoyote huwa inatunza na kudumisha athari za matukio muhimu ili watu wengine waweze kuzitambua kama matukio yalifanywa na Mitume.Maimam, Makhalifa na Waja wema wa Allah (swt) alisema Sheikh Swalehe.

Katikatini sheikh Abdull latwif Swalehe , wa kwanza Kulia ni Sheikh Ammar Maulid na wa mwisho Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Imam Swadiq Kilichopo Kigogo-Post Dar es salaam

Mwanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq akiwa ndie mc mr Iddy Saidi ambaye anasoma Darasa la 4




Wanafunzi wanaharakati pamoja na Waumini wakiwa makini kusikiliza MADA zinazowasilishwa mbele yao kutoka kwa Sheikh Abdullatwif Swalehe juu ya Siku ya Huzuni


Ni wajibu kwa Mwislam Kujiandikisha Kupiga Kura-Sheikh Jalala.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam katika kipindi hiki cha uandikishaji wa daftari la kupigia kura, waumini wajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuja kuitumia haki yao ya msingi ya kumchagu mtu wamtakae.
“Kipindi hiki kinahitajia lugha za busara,na maelewano,ni wajibu wa waislaam kisheria kujiandikisha na kupiga kura, “ni wajibu wako wa kuwachagua Raisi, Mbunge na Diwani watakao leta maelewanao, Mshikamano, Utulivu na Amani”amesema Jalala.
Ameyasema hayo katika swala ya ijumaa leo masjid Ghadiir-Kigogo Post –ar es salaam, na kusema kuwa kitendo cha kumwita mwenzako kua ni kafiri ni kusema kua damu Yake ni halali kumwagwa,na mali yake ni halali, nahii ni hatari jamii kuitana majina mabaya, majina ambayo yatasababisha damu ya mwenzio kumwagwa, na kumuhukumu kuingia motoni.

 “kuitana majina mabaya ni kuigawa jamii, na hakuna sababu ya kuitana majina mabaya wakati waislaam wote wanasema Laailaha Illa Allah, Muhammada Rasuulu llah,”kitendo cha mtu kumkiri mungu na mtume wake ni Heshima kubwa “ amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala amewataka waislaam na watanzania kwa ujumla kuwa kwayale yanayotendeka katika nchi za kiislaam, na Afrika za kuhatarisha amani kwa kujiripua na Kukufurishana na  mtu anaejita muislaam kua huo si uislaam na wala uislaam hauelekezi hayo,

 “Mwenye jina zuri la kiislaam kuingia katika msikiti na kujiripua na kuwaua waislaam Na Wakristo pamoja na watu wasiokuwa na hatia au kukamatwa mateka kwa wanawake na kuuzwa sokoni, ni uislaam upi unaoruhusu wanawake kuuzwa? Tunasoma katika vita ya jamali, uhudi, hivi ni vita gani wanawake waliuzwa? Uislaam gani wanaouonyesha hawa? Aliuliza Sheikh Jalala.

Sheikh Jalala amewausia waumini kuuusoma uislaam halisi wa mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuuhubiri kwa watu, na kuachana na huu uislaam wa chinja chinja na wa kuleta fakra kwa watu na jamii,
Hatahivyo Sheikh Jalala alihoji kuwa hivi hiki kibali cha kuwaingiza watu motoni wamekitoa wapi? Ni mwenendo wa mtume kweli hata wale wasio waislaam kuwaita makafiri? Laa hapana bali mtume (s.a.w.w) alikua akiwaita kwa majina mazuri, ndio maana hata katika mjadala na wakristo wa Najran, mungu aliwaita ya Ahlal kitab, iweje mwislaam mwenzio umuite kafiri?