Friday, March 11, 2016

MBUNGE KUBENEA AKAMATWA,NI MWENDELEZO WA POLISI KUPAMBANA NA VIONGOZI WA UPINZANI NCHINI,SIRI YA KUKAMATWA KWAKE YAVUJA NI HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA

Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la UbungoSEAD Kubenea Mbunge wa Ubungo amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki 
kushisha vurugu kwenye uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Kubenea amemueleza Mwandishi wa Habari hii  baada ya kumuona tena mahakamani Muda Mchache baada ya kusikia kuwa amekamatwa,
 Kubenea alijibu kwa ufupi kuwa ni 
"kweli nimekamatwa na hapa bado nipo chini ya ulinzi baada ya mwakili wangu kuiomba polisi waniachie kwa muda ili nihudhulie kwenye kesi ambayo natuhumiwa na Poul Makonda Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Baada ya kumalizika kwa kesi inayomkabili"
 Waandishi walimtaka Kubenea aeleze kinachoendelea ambapo amesema

“Narudi Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwani nina tuhumiwa kuanzisha vurugu” amesema Kubenea

Kubenea amesema kuwa alikamatwa leo Saa Tatu asubuhi na Askari Sita  alipokwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuti kwenye kesi inayomakabili nahakamani hapo.
 
Kubenea amesema kuwa Askari hao walikuja mahakamani hapo kwa kudai kuwa wameagizwa kumkamata kwa tuhuma za kuhusika kwenye kuanzisha vurugu kwenye uchaguzi wa Meya ulikuwa haujakamilika.  
 
Kubenea amesema kuwa kukamatwa kwake ni njama za zilizopangwa na Serikali ya Chama Chama Mapinduzi kutokana na kugundua kwake kwa hati ya kughushi ya Zuio la mahakama lililotengenezwa na CCM ambalo ni Bandia
Baada ya kumalizika Kwa kesi Kubenea Alirudi Mahakamani
Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la Ubungo   UCHUNGUZI WA BAINIKA,
Kwa mujibu wa vyanzo vya kauminika kutokana ndani ya CCM ambazo mtandao huu umezipata zinasema hatua ya jeshi la Polisi kuwakamata madiwani na Wabunge wa UKAWA ni njama za kutaka kushinda kirahisi uchaguzi wa Meya wa jiji ambao unatarajiwa kufanyika wakati wowote toka sasa,
 
“Yaani hili Jeshi la Polisi linafanya kazi ya ukatibu uenezi wa CCM,kwani aliyefoji hati ya mahakama yupo nje ajakamatwa,na hapo wanachokifanya kama njia waliotumia CCM kushinda Halmashauri ya kilombero walitumia njia ya kuwakamata Wabunge na Ukawa siku ya kupiga kura ili akidi ipingue na  kuisadia CCM ishinde kirahisi “

SIMAMIENI SHERIA NA TARATIBU KWA UADILIFU MKUBWA – KAIRUKI

pi1Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki  amewataka Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kusimamia Sheria na Kanuni kwa uadilifu na kutoa fursa sawa kwa watumishi ili kuleta tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi.Mhe. Waziri alisema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya maadili kwa makatibu wakuu na Manaibu katibu wakuu yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 
Amewataka viongozi hao pia kuendesha shughuli zao kwa kushirikisha watendaji wanao wanaongoaza na kuachana na tabia za upendeleo ili kufanya kaingira ya kaazi yanakuwa bora na yenye kuleta ufanisi.

“Muwe na uongozi shirikishi , mtende haki na msimamie Sheria na Taratibu na kuacha tabia za kufanya maamuzi kwa upendeleo kwani kufanya hivyo kutafanya kuwe na mazingira bora ya utendaji kazi ndani ya Serikali”, alisema Mhe. Kairuki

Amesema wao kama viongozi wakifanya na kuzingatia hayo watakuwa wametekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria na hivyo kuwa na utendaji uliotukuka.
pi1
Aidha amezitaka Wizara na Idara za Serikali kuanzisha vitabu vitakavyosajili zawadi ambazo viongozi na watumishi wa umma wanapewa wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ili kuwa na usimamizi mzuri wa suala hilo.

 Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inawataka Viongoai kukabidhi zawadi wanazopewa wanapotekeleza majukumu yao zenye thamani ya zaidi ya sh 50,000 kwa maafisa masuuli wao ili kuepuka mgongano wa maslahi

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Katibu Mkuu Kiongozi mhe. Balozi John Kijazi aliwasisitizia watendaji hao wakuu wa Serikali kusimamia maadili ili kufaniksiha utendaji uliotukuka ndani ya Serikali.

Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuwaleteae maendeleo ya kweli wananchi kwa kuwaondolea umasikini na kusisistiza kama wote walivyotia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu siku waliyoapishwa ni wajibu wao kuhakikisha wanaishi kwa mujibu wa viapo hivyo.

Aliwataka Makatibu wakuu na Manaibu hao kuhakikisha wanasimamia sheria na taratibu zilizotolewa na Serikali na ni imani yake kuwa watasimamia hiyo kama walivyoapa,

RAIS DK. MAGUFULI AIAGIZA BENKI KUU KUSIMAMISHA MALIPO ILI YAHAKIKIWE


Tangu Oktoba, Wapalestina 200 wameuliwa shahidi

Tangu Oktoba, Wapalestina 200 wameuliwa shahidiAsksari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina 200 tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba mwaka jana hadi hivi sasa.

Jumuiya ya kitaifa ya familia za mashahidi wa Palestina leo imetoa ripoti inayoeleza kwamba tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, Wapalestina 200 wameuliwa shahidi katika maeneo tofauti ya Ufukwe wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na vilevile katika mji wa Baitul Muqaddas.

51 miongoni mwa mashahidi hao ni watoto wadogo na 20 ni wanawake.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika muda wa saa 48 zilizopita Wapalestina saba wameuawa shahidi, watano huko Baitul Muqaddas na wawili katika eneo la Ufukwe wa Magharibi.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2015 hadi sasa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yamekuwa yakishuhudia wimbi la malalamiko ya upinzani dhidi ya siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni na njama za utawala huo za kupotosha utambulisho wa Baitul Muqaddas pamoja na mpango wake wa kuugawa kiwakati na kimahali msikiti mtukufu wa Al-Aqsa. Wimbi hilo la malalamiko limekuwa maarufu kwa jina Tangu Oktoba, Wapalestina 200 wameuliwa shahidila Intifadha ya Quds.chanzo irib

Kiongozi: Vita vya Mashariki ya Kati ni vya kisiasa tu

Kiongozi: Vita vya Mashariki ya Kati ni vya kisiasa tuKiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, wananchi wa Iran wameonesha kivitendo imani yao kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi uliofanyika nchini hivi karibuni.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo katika mkutano wa mwisho na Mkuu pamoja na wajumbe wa Baraza la nne la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu. 

Amewasifu na kuwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Februari 26 na kueleza kwamba: Wananchi waling'ara vizuri katika uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu kutokana na asilimia 62 ya waliotimiza masharti kushiriki katika upigaji kura; na hicho ni kiwango cha juu kulinganisha na nchi nyingi zinazojigamba kuwa za kidemokrasia.

Huku akibainisha kuwa wananchi wametimiza wajibu wao kwa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi, Kiongozi Muadhamu amesema sasa ni zamu ya viongozi kutekeleza majukumu yao.
Ayatullah Khamenei amesema jukumu la Baraza la Wanazuoni Wataalamu ni 

 "Kubakia katika hali ya Kimapinduzi, Kufikiri Kimapinduzi na Kufanya Kazi Kimapinduzi", na akafafanua kwa kusema, kuzingatia sifa hizo tatu maalumu katika namna ya kumchagua Kiongozi Mkuu wa baadaye wa nchi ni miongoni mwa mas-ulia makuu liliyonayo baraza hilo, na kwamba katika kumchagua Kiongozi wa baadaye ni lazima kuweka kando ucheleaji, muhali na Kiongozi: Vita vya Mashariki ya Kati ni vya kisiasa tukufikiria mambo kimaslahi.

Katika hotuba yake hiyo mbele ya wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu, Ayatullah Khamenei ameashiria pia majukumu ya viongozi wa serikali na kusema: Katika mazingira ya hivi sasa viongozi wazingatie na kuvipa umuhimu vipaumbele vitatu ikiwemo uchumi wa muqawama, kuendeleza kwa kasi harakati ya kielimu na kuipa kinga kiutamaduni nchi, taifa na vijana.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuwa na maelewano na ulimwengu mzima isipokuwa Marekani na utawala wa Kizayuni.

Aidha amevielezea kuwa ni vya kisiasa tu vita vinavyoendelea hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati na kutahadharisha kwa kusema: Maadui wa Uislamu wanajaribu kuzigeuza hitilafu hizi kuwa za kimadhehebu ili zisiweze kuhatimishwa kirahisi, hivyo haipasi sisi kuwasaidia kufikia lengo hili hatari"chanzo irib

Thursday, March 10, 2016

Serikali kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa

KADASerikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Hayo yamesemwa leo Jijini  Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa  akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.

“ Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda  Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
KADA
Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo  katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.

Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo  hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.

WAZIRI MKUU: TANZANIA YAPIGA ​HATUA KIUCHUMI

TIH4WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

“Kumekuwa na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa mfumuko wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa limekua kwa wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 5.3 mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka 2013,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumatano, Machi 9, 2016) wakati akihutubia kongamano la biashara baina ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Bw. Troung Tan Sang.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema mbali ya mabadiliko ya kiuchumi, Tanzania pia imefanya mabadiliko kwenye sheria, mifumo ya kifedha na sekta za kuhudumia jamii za umma.

“Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita tumefanya mabadiliko ya kisera na kwenye sheria zetu ili kuboresha hali ya uwekezaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi,” alisema.
TIH4
Alitoa mwaliko kwa wafanyabiashara walioambatana na Rais wa nchi hiyo kwa kuwaeleza kwamba faida kubwa ya kuwekeza nchini Tanzania ni uwepo wa soko la uhakika kwa wakazi zaidi ya milioni 300 waishio Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.

“Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya za Kikanda katika SADC na EAC. Uwepo wake katika taasisi hizi ni fursa tosha. Pia Tanzania ni lango kwa nchi sita ambazo hazipakani na bahari. Inasaidia kufanyika biashara katika nchi za Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Uganda,” alisema.

Akizungumzia kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo, Waziri Mkuu aliwakaribisha wafanyabiashara hao wawekeze kwenye kilimo cha biashara na viwanda vya usindikaji ili waweze kusaidia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

“Tuwakaribisha kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani za mazao yanayozalishwa nchini, kujenga viwanda vidogo vya kutengeneza vifungashio kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Pia mnaweza kuwekeza kwenye utengenezaji wa zana za kilimo ambazo ni za bei nafuu kwa wananchi wetu,” alisema.